Kapteni Ibrahim Traoré, kashaanza kulewa madaraka

Kapteni Ibrahim Traoré, kashaanza kulewa madaraka

Umesoma kichwa kimekariri demokrasia, sisi afrika hatutaki huo upumbavu..Tuko huru sasa
 
Kama ilivyokuwa kwa Magufuli, aliua upinzani akiamini kuwa ndiyo maadui wake kumbe maadui alikuwa anakula nao meza moja(Paul Makonda) matokeo yake wakamuua na nchi ikarudi kwa mafisadi papa(wanamtandao).
Inasikitisha sana
 
Wengi waliambiwa lakini hawakusikia. Rais wenu aliyekuwa ''mfano wa kuigwa wa Afrika'', tayari keshalewa madaraka.

Nukuu: ''Demokrasia inaua na watu wa Burkina Faso lazima wasahau kuhusu hilo” Kapteni Ibrahim Traoré, ameiambia televisheni ya serikali ya nchi hiyo.

Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi miaka mitatu iliyopita, alidai kwamba Wafrika wengi hawataki mfumo wa demokrasia na kwamba Burkina Faso ina njia yake mbadala, lakini bila kutoa maelezo zaidi ni njia ya aina gani

Traoré awali aliahidi kurejesha utawala wa kidemokrasia ifikapo Julai 2024, lakini miezi miwili kabla ya tarehe hiyo, alitangaza kuwa junta itaongeza utawala wake kwa miaka mingine mitano.
Lakini kama kuonyesha kuwa mwafrika hajafikia level ya kujiongoza, mnamo Januari, mamlaka ilitangaza marufuku ya vyama vyote vya siasa kama sehemu ya mpango wa “kujenga upya taifa.”

Katika mahojiano aliyfanya Alhamisi usiku, Traoré alisema: “Watu wanahitaji kusahau suala la demokrasia. Demokrasia si kwa ajili yetu. Tazama Libya, hii ni mfano halisi,” alisema huyo kiongozi ambaye anajiona kama kama kiongozi wa mapinduzi anayepigana dhidi ya ukoloni wa Magharibi. (mabeberu).
My take: Huu ni mwanzo tu siku si nyingi ataanza mauaji ya wapinzani wake na wananchi wenye mawazo mbadala hawatasalimika!

Source: Captain Ibrahim Traoré says Burkina Faso must 'forget' about democracy
Viongoz wa afrika huwa wanaanza kwa nia njema and then tamaa hushika hatam
 
Back
Top Bottom