muyakb24
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 412
- 299
.
Sent using Jamii Forums mobile app
MKASA WA KWELI
KAONDOKA NA MOYO WANGU
MWANDISHI; ZUBERI MARUMA
WHATSUPP 0759427653
Sehemu ya kumi na moja
Kijana Ramadhan Maulidi anaendelea na mkasa wa maisha yake alokumbana nayo,sehemu ilopita tuliishia, baada ya kutua jijini Dar es sallam na kuyaanza maisha anajikuta akitokea kumpenda Salma Walokutana Kazini,je nini kiliendelea twende pamoja uendelee kujifunza...
"Hivi Rama unanipenda kweli na una malengo ya kuishi na mimi au lengo lako ni kunichezea tu mimi!"
Salma aliniuliza kwa sauti ya upole,sauti tamu!
"nakupenda sana tena sana Salma nawe nadhani unalijua hilo!"
"unan'danganya Rama,kama Wanipenda Kwa nini utaki kunitambulisha kwenu?,kwanin hutaki tuuoane kwa nin lakini?"
Dah niliishiwa pozi nikabaki kimya,unajua toka Salma aamie pale nyumbani ninapoishi ilikuwa ni siku ya tatu,alinambia yupo kwenye 'period' ivyo hakukubali ni mguse,wiki ile ikakatika,wiki ilofatia ilikuwa ikifika jioni anakosa raha ule uchangamfu wote anaupoteza na hata pale ninapo mgusa anakuwa mkali mara najisikia vibaya mara naumwa na tumbo,mpaka sasa nikawa siuoni umuhimu wake kuishi naye pale,japo kupika alinipikia,kufua alinifulia ila tatizo likawa kwenye tendo la ndoa!
"hivi unajua Salma mimi nimechoka?!,hivi mimi na wewe ni ni mtu na dada yake au?"
"kwa nini?!"
"sijaridhia aya maisha tunayoishi bora tu uondoke zako kama uwezi kunikidhia aja zangu"
"Kama ni Ivyo Rama mi ntaondoka ila siwezi kuikurubia zinaa hakuna mtu anayetuona ila Malaika na hata Mungu Pia wanatuona tulivyofanya huko nyuma vinatosha mpaka unioe ndo utaujua mwili wangu"
Nilicheka Kwa dharau,
"niujue mara ngapi huo mwili wako kipi hasa nisichokijua hapo"
"kama unaujua kwanin sasa unauhitaji!"
"kwa kuwa ni haki yangu!"
Nikajikuta naropoka,
"haki yako wapi? umenioa mpaka uniite mimi haki yako? kama una la kuongea bora tu unyamaze ulale zako!"
"ahaaa unajifanya ustadhat siyo,swala tano etie basi usingekuja kuishi na mwanaume kesho usepe zako una maana kabisa wewe"
"sawa mi ntaondoka kama ndo unahitaji ivyo,kama umenileta kwako kukidhi haja zako unitumie uniache mi ntaondoka ila sipo tayari kufanya unachotaka abadani asilani"
Kila mtu akalala kivyake tukiwa tumenuniana,Salma ghafla alibadilika akawa mtu wa ibada nilimchukia kwa kweli
Asubuh jumamosi hiyo niliamka zangu atukusemeshana, baada ya kunywa chai mi nikaelekea kwa jamaa angu mwenye banda la movie palepale matumbi nikawa nikitazama,kupoteza poteza muda
Ilipotimia mida ya saa sita ghafla simu yangu ikaita kumcheki ni Salma,kwa kuwa nilimnunia sikutaka kuipokea ikaanza kuita tena,
Nikaikata...
Sikukaa Sana nikapigiwa kwa namba ya ba mkwe,hii ni namba ya baba yake Salma huyu alikuwa muhabi yani wale waislamu wenye itikadi Kali na ndo maana hata walikuwa wakinilazimisha nimuoe mtoto wao
'mmh kuna nini tena!'
nikawaza nikatoka nje ya banda lile kuipokea hiyo simu katu sikujuwa nilichopangiwa au ninachoenda kuambiwa...
"Asalam aleykum mzee"
Nilimwamkia kwa adabu
"walekumssalam kijana nakuomba hapa nyumbani mara moja kuna kitu nahitaji tuzungumze"
Nilishtuka!,nikajua Lazima Salma hatakuwa kashaenda kusema umbeya kule kwao,
"sawa mzee wangu nakuja mida hii"
Wala sikurejea ndani tena ya banda nikaelekea mpaka nyumbani kwa kina Salma alipozaliwa nilijua nitamkuta!
Nilipofika Nilikaribishwa Sebuleni,
Nilishtuka kuikuta familia nzima pale sebuleni niliwakuta Watu siyo chini ya kumi,baba yake baba wadogo zake,wajomba dada zake wengine sikuwajua pia alikwepo sijui ndo Sheghe yule au ustadh mi sijui bhana!!
Hata Salma Mwenyewe Pia alikwepo nikaoneshwa sehemu ya kuketi nikaketi
Sasa moyoni nikawa nawaza
'Hii kesi gani inasikilizwa na familia nzima!'
Baba mkwe akaniambia...
"Rama mwanangu tumekuita kwa swala moja kwa kipindi
cha wiki kadhaa sasa unaishi na mtoto wetu kama mume na yeye mke tunahitaji kujua je ni kweli Unampenda Salma?,na Upo tayari awe mkeo maana katika vitu binadamu tunavyopaswa kufanyiwa haraka cha kwanza ni kumzika mtu anapokufa na cha pili ni kuozesha watoto walokwisha pendana ustadh yupo hapa cheti cha ndoa hiki hapa binti huyo hapo atakutajia mahari yake tuwafungishe ndoa maswala sijui ya sherehe ni hapo mtakapojipanga nyinyi na familia zetu ila kwa sasa tufanye hili swala chap ukaishi na mwenzako kihalali
JE UPO TAYARI TUWAFUNGISHE NDOA CHAP MUISHI KAMA MUME NA MKE KIHALALI?!"
Watu Wote sasa wakawa wakintazama mimi nikajikuta naona aibu nikajibu
NDIO NIPO TAYARI KUMUOA SALMA"
Watu pale wakafurah,Salma akaambiwa ataje mahari yake
Cha ajabu sasa kilichonshangaza na kunifanya mpaka Leo hii ni mkumbuke yule mwanamke na kumuona ni wa ajabu katika maisha yangu na ni wa ajabu pia katika mabilioni ya wanawake wote duniani
Ni hiyo mahari alonitajia!...
"mahari yangu nahitaji anisome sura til yasin,na ayatl kurusii kama zawadi yangu na sadaka yangu pia"
Cha ajabu hata familia pia aikushangaa baba akaagiza ukaletwa msahafu
Nikakabidhiwa nilikuwa natetemeka nilihisi kila kilichokuwa kikiendelea ni ndoto
Nikafungua ule msahafu nikasoma zile sura nilizotajiwa baada ya kumaliza ndipo tulivyofungishwa ndoa cheti kikaandikwa tukala cha mchana palepale saa kumi kila kitu kikawa kimekamilika tukaruhusiwa kuondoka zetu!
"sasa nipo maridhia kwa kila kitu juu yako mume wangu!"
Salma alintamkia huku akiwa na tabasamu jepesi,
"hivi imekuaje mpaka wazaz wako wakatufungisha ndoa ya mkeka?"
"Rama katika uislam hapana ndoa ya mkeka ila ndoa ni maridhiano ya watu wawili kuishi pamoja na kujenga familia,hiyo ndiyo ndoa mambo ya sherehe dufu ni mbwembwe tu"
"kwa hiyo amna kigodoro?"
"mmmh Rama acha hizo bwana,sasa lini utanipeleka Moshi nikawaone wakwe zangu,kule ndo kwetu saivi"
"usijali mwisho wa mwezi huu tutaenda,tutakaa mwez wote wa kumi na mbili,mwez wa kwanza tutarudi,"
"ntafurah mpz!"
Basi mi nikaendelea na kazi kama kawaida,nikawa nikitoka saa 12 narudi saa 2 usiku jumamosi na jumapili ndo nilikuwa free hata ivyo sikupenda kukaa sana nyumbani...
Siku zikasonga hatimaye baada ya kupoteza mawasiliano na kukaa mbali na nyumbani kwa muda wa mwaka mmoja na nusu hatimaye mwez ule wa 12 tukafunga safari kurudi Moshi,safari hii nikiwa na mke wangu niliyo mpenda zaidi ya kitu chochote
SALMA!
Sent using Jamii Forums mobile app