Kaondoka na Moyo wangu

Kaondoka na Moyo wangu

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kwanza

UTANGULIZI

Ni mwanamke nilompenda toka ndani ya mvungu wa moyo wangu,

Nikayabeba matatizo yake na kuyafanya yangu,

Sikutegemea kama angekuja kuondoka na moyo Wangu,

Siku mbili kabla Mimi na yeye kufunga pingu,...

My Princess bado unaishi ndani ya upendo Wangu

01

Jina langu kamili naitwa Ramadhani Maulidi,(si jina halisi) nikiwa mtoto wa mwisho wa mzee Maulidi nimebahatika kuwa na kaka wa nne na dada watano nikiwa nimezaliwa mwaka 1994,kaka zangu wote wameshaoa dada zangu 3 wameolewa,wawili wapo nyumbani

Kaka yangu mkubwa ni mwalimu wa sekondari mkoani Singida,

Sisi ni wenyeji wa mkoani Kilimanjaro nikiwa mdogo darasa la tano kaka yangu aliamua kunichukua kwa dhumuni la kwenda kunisomesha, si unajua tena akili za kitoto nilifurahi kwenda Singida,ivyo mama angu akaangaikia uamisho mwezi wa nne likizo fupi ile kaka akaja kunichukua tayari kwenda kuanza maisha mapya mkoani Singida,

Nilipoanza masomo kadri siku zilivyokuwa zikienda furaha ya kuishi kule ikawa ikipungua,hasa kutokana na nyumbani kudekezwa,

Nilikuwa nikienda shuleni napewa hela si unajua tena mtoto wa mwisho kwa mama,

Huku Kwa kaka hela nikawa sipewi,nyumbani nilizoea kufatilia vipindi kwenye runinga,huku hata tv nikawa siruhusiwi kuangalia nyumban nilikuwa sifanyi kazi hata moja huku nikawa naambiwa nikachote maji mbali kisimani,achia mbali kazi za shamba nk,

Hakika maisha ya kule kijijin Yalikuwa ni magumu ukilinganisha na ya kwa wazazi nilipotoka...

Ulka ya usafi na utanashati nilikuwa nayo toka awali,wakati wanafunz wenzangu wakifua kila jumatano na jumamosi au jumapili mimi nilikuwa nikifua jumamosi tu kwani nilikuwa na nguo pear tatu ivyo nilikuwa sivai nguo chafu...

Utanashati nilokuwa nao ukawavuta watoto wa kike kujenga urafiki na mimi,wakati nilipofika darasa la sita shuleni kwetu aliamia mwanafunzi mmoja alotambulika kwa jina la Princess Yule Mwanafunzi nakumbuka mama yake alikuwa ni daktar wa hosptal Moja Iitwayo Makiungu hosptal,

Kiukwel princess alikuwa na sura nzuri hakika kila mwanafunzi alimmezea mate na kutamani awe tu Mchumba ake!,

Huku watoto wa kike wakijigonga kupata nafasi ya urafiki,

Ligi kali ya kumgombania Princess ikazuka pale shuleni,

Ila katika ligi ile mi nilibahatika kuwa mshindi hapo ndipo tulipoanza mahusiano na binti yule mrembo...

Nakumbuka siku hiyo kama bahati tulikutana mnadani,huko niliweza mshawishi Princess kwa mara ya kwanza akanipa penzi lake,yeye alikuwa ajafanya nami ndo nilikuwa naanza,nilimshukuru nikimpa pole alilia sana akidai nimemuumiza nikamuomba msamaha,

Kwanzia hapo penzi letu likamea na kuzidi maradufu,japo tulifanya siri...

Hatimaye nikamaliza darasa la saba,na kurejea nyumbani Moshi kusalimia nikiwa nimekaa mbali na wazaz kwa muda wa miaka mitatu kasoro...

Matokeo yalipotoka mi jina langu alikuonekana kwa kwel niliuzunika sana,ila kaka alinambia nisijali tusubiri matokeo ya pili ikiwa sitofaulu basi angenipeleka ufundi au 'privet' bahati nzur matokeo yalipotoka mwez wa pili jina langu likawa miongon mwa waliofahulu ila mimi nikapangwa shule mpya iitwayo Makiungu,

Nikaandaa zangu safari nikarejea zangu Singida,nilipo Uliza Juu Ya Mpz wangu princess niliambiwa yeye kafaulu Mungaa,nikaanza Mbembeleza Kaka Yangu anifanyie uamisho kweli hilo likafanikiwa...

Penzi Letu mimi na princess liliendelea kwa siri,mpaka tulipofika kidato cha tatu ndipo mpz wangu alipobadilika!

Akawa akinikwepa,nikiongea naye anajibu kama ataki,siku hiyo akanipa barua kwenye bahasha kwenda kuisoma alinambia kwa sasa ameona bora alivunje penzi letu kusudi apate muda wa kusoma hawezi changanya vitu viwili ivyo mimi nitafute mwanamke mwingine, niliumia sana baada ya kuisoma barua ile,

Si kwamba wanawake awakunipenda shuleni pale la hasha wa madarasa ya juu na hata wa mtahani wengi walinihitaji wengine walinambia na wengine walinionesha dalili ila moyo wangu ulikuwa kwa mwanamke mmoja tu!

princess

Nilimpenda Sana Mwanamke huyo na tokea nimekuwa naye sikuwah kuwa na mwanamke mwingine,

Nilijikuta machozi yakinichuruzika, nikachukua daftari nikachana karatasi tayari kwa kumjibu,ila kila barua nilokuwa nikiiandika niliona ina makosa na kuichana nika andika ingine swala likawa lile lile,si chini ya makaratasi manne nilichana,baada ya kuridhika na barua mojawapo nikaikunja vizur na kuiweka kwenye bahasha kesho yake nikampelekea,

kumpa akaipokea...

Wakati anaondoka nikamkamata mkono nikamuuliza princess nimekukosea nin mpaka uamue kuniacha?!,

Akanijibu wala hata ujanikosea kitu,

"sasa kama sijakukosea kwanin unipe adhabu hiyo"

"nimeamua tu"

Alinijibu kwa mkato akauchomoa mkono wake kwenye mkono wangu akaondoka zake...

Baada Ya Mapumziko tukarejea madarasani ambapo kiongozi 'Monitress' wa darasa akaingia na daftari
alizotoka nazo ofisini....

"Rama Mau unaitwa ofisini na sir Amede"

Baada ya kusikia wito ule kutoka kwa kiongoz yule wa darasa pasina kuwa na khofu yoyote nikanyanyuka tayari kuelekea ofisini!...

Mwalimu Amede alikuwa ni mwalimu kijana wa tahaluma sisi akutufundisha na wala sikuwa na mazoea naye...

Nikachepuka haraka kwenda,kufika ofisini nilishtuka kumkuta kashika ile barua nlo mtumia mpz wangu na mbaya zaidi hata kaka yangu alikuwa kule ofisini

"naam mwalimu"

Niliitikia baada ya kuifikia meza ya mwalimu Amede

"umekuja Shuleni Kusoma au umefata mapenzi"

Mwalimu yule wa tahaluma aliongea kwa ukali!

Mimi niliangalia chini kwa aibu ila sasa kichwani kwangu nikawa nikijiuliza hii barua princess nikakamatwa nayo au nini kilichotokea ,

Mbona yeye ofisin ayupo?!

"Rama si unaulizwa wewe?"

Ghafla nikashtushwa na sauti ya kaka yangu...

Ambaye alikuwa mkuu msaidizi katika shule ile

Je Unahisi Rama atajibu nini?,barua imemfikiaje Sar Amede tuendelee kufatilia mkasa huu wa kweli ulomtokea ndugu Ramadhan

Nawe Kama Una Mkasa Unaweza Wasiliana Na Mtunzi Kwa No 0767433106 ukamsimulia kwa dhumuni la kuifunza jamii

ITAENDELEA.....
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

AUDIO: PRINCESS LEY

Sehemu ya pili,

Sehemu ilopita tuliishia kijana Rama kaitwa ofisini,kufika akashtuka kumkutwa mwalimu Amede akiwa kashika barua ambayo alimtumia Princess Je nin kiliendelea?

twende pamoja katika sehemu hii ya pili ya mkasa huu wa kusisimua ambayo ni mkasa wa kweli...

"Rama!"

kaka yangu akaniita kwa ukali,huku akinyanyuka kutoka katika kiti chake na kunifata akiwa kashika fimbo

"naam," Nikaitika huku nikitetemeka,

"uoni aibu unaniaibisha mimi kaka yako haya lala chini,"

Haraka sana nikajitupa chini,kaka alinifata sitosahau alinitandika fimbo tano,alipo maliza akaja Amede,naye Akanichapa,mwalimu Mwingine alokuwa akiitwa Ikunguu,walimu Walinitandika Mpaka makalio yakawa yakiwaka moto,

"na tukija kugundua unaendelea na swala hili tutakusimamisha shule na utarudi zako moshi mtoto mpumbavu sana wewe"

Kaka aliongea akionekana kukasirika,

"aya nenda darasani"

Mwisho nikaruhusiwa kurudi darasani ila sasa nikawa nikijiuliza kichwani kwangu,mbona ile barua sikuandika jina langu zaidi ya kuandika jina la Princess nakumbuka barua yenyewe ilisomeka hivi...

kwako my princess,👸
bila shaka u mzima,
ila mimi mwenzako kifikra si mzima,

Nimepokea barua yako kwamba wahitaji tulivunje penzi letu💔,sawa sijakataa,ila tambua unauweka moyo wangu katika kiza kinene,we pekee ndo mwanamke nikupendaye,na nipo tayari kuyasimamisha mahusiano yetu kingono i mean mpaka tumalize masomo ila plz baki kuwa mpz wangu,

thaman ya furaha yangu, imebebwa na penzi lako,
ivyo unavyotaka kufanya nikujaribu kunipokonya furaha yangu,kama nimekuudhi nsamehe mpz wangu,naiman utanijibu...

sikiliza wimbo wa "mapenz kitu gan" wa mb dog uwe maalum kwa ajili yako...

Ni mimi kipenz cha moyo wako

Ndivyo nilivyoiandika barua ile,sasa iliwafikiaje walimu,na pili walintambuaje kwamba mwandishi ni mimi na tatu mbona Princess akushirikishwa katika kesi ile!

Hakika ndugu msomaji sikupata majibu ya maswali haya nikaingia zangu darasani nikijitahidi kuvunga kama akuna kilichotokea, mwalimu wa kiswahili alikuwa akiendelea na kipindi

"we Rama ulikuwa wapi muda wote wakati kipindi kinaanza ndo unaniingilia darasani,"

Mwalimu yule tulipishana njian wakati mimi nikielekea ofisin yeye alikuwa akija darasani

"nilikuwa ofisini mwalimu"

"huko ofisini ulikuwa ukifanyaje wakati wa kipindi changu"

Nikanyamaza,

Kunyamaza Kwangu Mwalimu akatafsiri kama na dharau na vile mlezi wangu alikuwa ni 'second master' pale shule nahisi ilichangia walimu kunibana na kila mwalimu alinijua

"haya toka nje mpaka nimalize kipindi ndo uingie"

Sikuwa na budi kutoka nje na kumuacha mwalimu aendelee kufundisha,baada ya dakika zake 45 kukamilika akatoka na kunikuta pale nje

"nifate"

Akaongea huku akinipa yale madaftar ambayo alikuwa kayashika mkononi tukaenda mpaka ofisini

"huyu mtoto alikuwa anafanya nini huku ofisini nusu saa nzima ndo ananijia darasani"

Mwalimu Amede sindo akampa ile barua ambayo ilikuwa imewekwa kwenye faili langu,

"kala fimbo hapa!..."

"ngoja na mimi nimwadhibu aya kamata chini"

Nikalala chini sikupenda kuwa mbishi mwalimu akanchapa na kwa kuwa alikuwa ni mwalimu wa zamu akanipa na adhabu juu nipalilie bustan ya hapo ofisin niongezee maua pamoja na kuinyeshea wiki nzima asb na jioni

Sikurejea tena darasani nikaendelea na kazi mpaka mida ya chakula...

Baada ya chakula kengele ya darasani ikagongwa tukaingia darasani,

Bado kichwan kwangu nilikuwa na mawazo na kila nilipo mtupia macho Princess alionesha kutojali hata ile kuniangalia kimapembe akuniangalia alikuwa bize na mambo yake,nikaona nisiumize kichwa mwenyewe bora swala hili nimshirikishe rafiki yangu Yassin pengine atanipa mawazo,

Sindo nikamuadithia kilichotokea ofisini,naye alionekana kushtuka akaniuliza mara mbilimbili ukuandika jina lako katika ile barua

"haki mi sikuandika"

"sasa walimu walijuaje ni yako hapo ndo inaponipa mkanganyiko,"

"au Princess aliamua kuepeleka kwa dhumuni la kunshtaki nini"

Nikajikuta wazo hilo likinijia,

"inawezekana kwa nini yeye asiitwe?"

"sindo hapo Yassin,yani dah kama ndo ivyo 'P' atakuwa kanikosea sana,"

"no,au itakuwa aliitupa mwalimu akaiokota wakasaminisha hati,brother ako akatambua ni yako ila wakashindwa kujua ulimtumia princess gan na princess wakachukua jina la kimahaba,kwanza Princess shulen hapa wapo wengi"

"pia ilo linawezekana man lakin kama ndo ivyo wangeniuliza ulimwandikia
nani?,unajua awakuniuliza Kabisa Juu ya alotumiwa barua hiyo!

"dah kwel hapo kuna utata,tusiishi kwa kudhani swala hili niachie mimi nitampeleleza atanambia kila kitu ntakufikishia kwa sahivi mpotezee usiongee naye chochote walimu watakuwa bado wanakufatilia mi ntachunguza ntajua kila kitu,

Basi nilikubaliana na rafiki yangu kumwachia swala lile yeye,mchana ule mwalimu yoyote wa somo akuingia tukaendelea kujisomea somea mpaka sa tisa kengele ya usafi ikagongwa...

Tukatoka madarasani, tukafanya usafi tukakaa mistarini,tukaruhusiwa kwenda nyumbani...

Kichwani Kwangu nikijua ya meisha...

"we Rama njoo"

Nilishtuka sauti ya kaka ikiniita tena kishari,nikaitika na kuelekea sebuleni,alikuwa kakasirika vibaya sana,mkewe alikuwa pembeni...

JE UNAHISI NIN KILIENDELEA USIACHE KUENDELEA KUFATILIA MKASA HUU WA KWELI UTAKAOKUFUNZA NA KUKUBURUDISHA PIA,
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

AUDIO: PRINCESS LEY

Sehemu ya tatu

Kijana Ramadhani anaanza mapenzi akiwa bado kijana mdogo sana,wakati akiwa kidato cha tatu mpz wake anayavunja mapenzi ghafla na kumwambia waachane swala hilo linamuumiza kichwa Rama Na Kuamua Kumuandikia barua ya kulalamika kwa bahati mbaya ile barua inafka kwa walimu na kuadhibiwa vibaya sana,soo aishii shuleni anapofika nyumbani kaka yake anamwita je anataka kumwambia nin twendelee na sehemu ya tatu ya mkasa huu wa kweli ulontokea mimi japo jina nililotumia huku si lakwel la kiusalama fb,

kaka akanipa ishara niketi kwenye kochi,

Kiukweli nilitokea kumuogopa sana kaka yangu naye alilitambua ilo,pengine ni kutokana na ukali wake,

Sikuwah kukaa na kupiga naye stori pia ilikuwa ni nadra kuliona tabasamu lake muda wote alikuwa kavimba,na hata maisha ya pale nyumban alikuwa akiyaendesha kijeshi hasa katika swala la kazi,

"Rama katika siku ulizo niudhi leo umeniudhi na jambo hili sitoweza kulifumbia macho,wewe ndo mfano wa kuigwa hapa shuleni lakin mapenz na wewe,wewe na mapenz na nakwambia wazi sikufichi kama ushayajua mapenzi hapo amna masomo tena na ukija kumtia mtoto wa watu mimba sitokuwa na msaada na wewe chukua ongea na baba yako...

Dah,hakika Nilichoka yani jambo dogo lile kaka kaamua kulifikisha mpaka nyumbani Moshi,akampigia baba ambaye tayar alisha ongea naye na kumweleza kila kitu,baba akaanza kunisema

"Rama Mwanangu achana na mapenzi soma ayo yapo utakutana nayo tu,soma upate kazi nzuri uwe una ela mbona watajileta wenyewe,ila usinisikilize umtie mtoto wa watu mimba utatafuta pa kukimbilia ila kwangu usikanyage..."

Nakumbuka baba alinisema,kaka akanisema tena nikajifanya nimesikia...

Kesho yake shule nilimweleza kila kitu rafiki yangu Yassin juu ya noma nililoletewa home,jamaa angu alinipa pole kisha akanambia
Rama jana nilionana na Princess Prepo nilijaribu kumdadisi hasa kwa nini amekuacha hakunipa sababu yoyote zaid ya kunijibu kaamua tu,nilipo mbana zaidi alinijibu saivi anahitaji kusoma kwa ajili ya mtihani wake mwakani,

"sasa unanshaurije best?"

Nikamuuliza rafiki yangu nikionesha wazi kukata tamaa

"achana naye Rama,mpotezee kama kaamua hivyo usimlazimishe kumbuka mapenzi ayalazimishwi kaka"

"ni kwel asee lakin mtoto yule nampenda eti"

Nikajibu nikionesha wazi kuelekea kukata tamaa

"lakini ndo ivyo yeye akupendi utamlazimisha?!,subiri utampata anayekupenda"

"Sawa" Nikakubali Kishingo Upande,ila Kiukweli Moyo Wangu Ulikuwa Ukiniuma Sana Kila Nikimuona Yule binti,japo atukuongea kila mtu akachukua amsini zake,na vile nilionywa sikutaka kuja kuletewa shida tena...

Siku zikaenda,taratibu nikaanza kumsahau Princess na kumuona wa kawaida tu,ila pale shuleni kuna mwalimu mmoja alikuwa anipendi,

Sar Amede,mwalimu Wa tahaluma...

Pia alikuwa akitufundisha mathematics alikuwa akiingia anafundisha anatoa mifano anaandika swali mtu wa kwanza kumwita akalifanye ubaoni ni mimi Rama nikishindwa anantembezea viboko,roho ikawa ikiniuma sana nikajua pengine ni bro ndo kamwambia ivyo,inaweza ikawa si zamu yake anakuja kuhesabu no nikiwepo kwa walowah walochelewa anawasamehe,nikiwa nimechelewa kwa bahati mbaya kutokana na kazi ajal ilo ntatembezewa bakora akidai ntachelewaje na nipo ndani ya uzio wa shule...

Ni Kwel Muda Mwingine alikuwa na haki ya kunichapa ila mara nyingi alikuwa akinionea pasina kujua sababu mpaka siku hiyo...

Kaka kuna vitabu alinipa nimpelekee Sir Amede unajua ndani ya uzio wa shule kulikuwa na nyumba tano za walimu zimefatana nyumba yetu ilikuwa karbu na getini,inafatia nyumba ya Sir Amede,alikuwa Akiishi Peke Yake,inafatia Nyumba Za Walimu Wengine ambao wapo walokuwa wakiishi na familia zao wengine walikuwa wakiishi peke yao,

Basi mi nikaenda kufika pale mlangoni kwake nikakuta kuna malapa ya kike,ilikuwa jumamosi hiyo,nikajua lazima Mwalimu atakuwa na kifaa leo,sasa nikawa nawaza nigonge au

Nikasema nikirudi ningeenda kumwambiaje kaka?,nikaona bora tu nigonge baada ya kugonga sana sir akatoka akiwa kifua waz na bukta tena ya manchestar!

Aliniangalia Kwa Chuki,

Sikujali nikamkabidhi vitabu vyake mi nikaondoka,

ila sasa bado nikawa nikijiuliza kwanin mwalimu antazame kwa chuki kiasi kile,

Kwa Nin anchukie mimi vile,nimemkosea nini mimi?!

Wakati nikiwa katika mawazo hayo huku nafua si ndo rafiki yangu akaja,

Yasin Yeye alikuwa ni mtoto kabisa wa mwalimu nyumba yao ikiwa ya tatu toka yetu yani inaanza yetu,inafatia ya sir amede alafu yao na nyenginezo

"Rama uwezi amin bwana princess kumbe anatembea na Sir Amede"

Nilishtuka,"anatembea Na Sir Amede Kivipi yani?"

Asb bwana si alintuma dukani sukari kurudi kuingia sebuleni nawakuta princess kavaa kanga tu kamlalia naye kavaa bukta na singland"

"haaa wacha bwana,kumbe ndo maana bro alinipa vitabu fulan mida ya saa sita sita nimpelekee nikakuta malapa flan ya kike pale nje nikagonga akatoka kankata jicho vibaya sana"

"ndo ivyo man,yule manzi snich kaku krash kisa teacher banah!"

"ndo ivyo man si unajua ticha pengine uwa anamwezesha majibu,visent nk,ivyo maamuz yake yapo poa"

"sawa sijakataa kosa lake ni kukuacha kwa kisingizio cha kuwa saiv anahtaji asome kule ndo kusoma?"

"yangoswe kaka tumuachie ngoswe ndo maamuz ya moyo wake" mi nikajibu

"ila sasa nshapata picha"

"picha?,ipi hiyo"

"itakuwa ile barua alimpelekea ticha mpz wake akamwambia unamsumbua kusudi ticha akufanyie alivyokufanya uache kumfata itakuwa alimpa tu isingewezekana ijulikane ni yako wakati ukuandika jina yule manzi snich sana"

"ndo ivyo kaka kikubwa si tushamjua kwa ni nini tumwache na maisha yake mi kashantoka moyoni"

"ok" tukaendelea na stori nyingine...

Siku hiyo ikapita,jumapili nako ikaisha

Jumatatu Kama Kawaida tukarejea shuleni...

Ni Kabla Mwalimu ajaingia asb ile nikiwa nimekaa zangu kwenye dawati mimi na jamaa angu Yassin ghafla Princess akaja...

"yassin mambo,"

Akamsalimia Lakin Yassin akuitika akaja kwangu

"Rama naomba daftar lako la maths sijafanya ile home work ya jtatu kabla sir ajaja plsss..."

Aliomba huku akideka akiwa katika tabasamu lake,akichezesha chezesha na vimikono vyake...

TUTAENDELEA
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya nne

Bado naendelea na mkasa wa maisha ya ndugu yetu Ramadhan na jana tuliishia pale ambapo Princess kaja katika dawati lake kumuomba daftar je unajua nin kiliendelea?!

Tusonge...

Basi baada ya binti yule kunambia vile mi binafsi nilihisi ananiinjoy,

Nikajikuta namjibu vibaya tena nikiwa mwenye hasira...

"si umuombe huyo mpz wako akupe majibu,"

"mpz wangu?,nan huyo mpz wangu"

Princess akaniuliza kwa nyodo,mdomo akiukunja

Yassin akadakia...

"unadhan ni siri hatujui kwamba unatoka na ticha wa tahaluma"

Taratibu Princess akarudi kwenye dawati lake akajiinamia chini,sisi tukaendelea na mambo yetu tukaachana naye...

Punde tu mwalimu akaingia alishtuka kumkuta Princess Wake kajiinamia akamwiita akamuuliza unaumwa?, Princess akujibu kitu akabaki kajiinamia...

Ikabidi mwalimu amwambie ainue kichwa uso mzima ulitapakaa machozi,akawa akimuuliza unatatizo gan Princess akawa ajibu yeye ni kulia tu basi akamwambia akamsubiri ofisini kwake,

Princess akatoka,sir akaendelea kufundisha ila siku hiyo sikumwelewa kabisa mwalimu kitu anachofundisha nilikuwa nikimuwaza Princess je alikuwa analia kutokana na jibu alilopewa na Yassin au?,na je angeeleza nin ofisini na nini kingeendelea?!...

Hakika nilikuwa na mawazo sana mpaka mwalimu akamaliza akatoka zake...

"dah mjomba noma nyingine inaibuka unahisi Princess atatutaja kweli nawasiwas sana,"

"anawashwa nin,unamuogopa atutaje aone hili soo litafika kwa mwalimu mkuu tutawachana wote sitokubali yule ticha anchape kifala"

Yassin aliongea kwa kujiamin,akanipa moyo kidogo,unajua noma la watu wawili si kama la mtu mmoja hivyo sikuogopa katu nilijua kama ni kusemwa tungesemwa wote wawili tena alomchana ni Yassin na wala si mimi"

"Ramaa" Ghafla nikashtushwa na sauti ya mwanafunz mmoja aliita kwa dirishani

"unaitwa ofisini kwa sir Amede"

"kumekucha Sasa"

Nikajisemea sambamba na kuamka huyo nikaelekea zangu ofisini ila sasa njiani nikawa nikiwaza kwa nini niitwe mimi na Yassin asiitwe au ndo ivyo jumba bovu laenda niangukia mimi tu,

Nikaelekea Mpaka Ofisini,ticha Wa taaluma,mkuu msaidizi na hata mwalimu mkuu pia walikuwa na ofisi zao japo mara nyingi kaka na sir Amede walikuwa wakitumia ofisi ya walimu kwa story pia walikuwa na meza zao,

Nikaingia mpaka ofisini nikamkuta Princess kakaa pembeni ya mwalimu safari hii alikuwa kanyamaza!

"umemwambia nini huyu?!"

Amede akaniuliza kwa ukali,baada tu ya kuingia ofisini kwake

"mh sir mbona sijamwambia kitu?"

"kwa hiyo huyu ni mjinga alie mwenyewe?"

Sir akazidi nibana akiukunja mdomo wake kwa dharau nikanyamaza,

Akasimama na kunisogelea
akantandika kibao cha usoni,

"sinakuuliza wewe umekuwa bubu au"

Muda huo huo akachukua fimbo ilokuwa mezani acha aanze kuntandika pasina kuangalia hata ananpiga wapi mara mgongoni, mabegani kichwani usoni,

Hasira si zikanipanda, akunipiga kistaharabu nikaizuia ile fimbo nikaishika oa kumpokonya nikaivunja...

kitendo iko si kikamkasirisha!

"unavunja fimbo siyo..."

Akaanza nipiga mangumi, mateke bila hata huruma, hasira zikazidi nipanda nikamuotea ngumi moja ya usoni nikaikamata tai yake sasa nikawa naivuta nikimwambia namuua,awezi nipiga kisa mwanamke sasa lazima nimuuwe,sikuwa na mzaa,unajua mimi ni mpole ila mtu asinchokoze huwa na hasira mbaya na za karibu...

Princess Kumwona Mwalimu Sijui Bwana Wake Yule Katoa Macho nimdhibiti vizuri akaanza piga kelele anaua,anaua anamuua mwalimu anauaaa

Si Ndo Walimu Kutoka Ofisi Ya Walimu Wakaja Wakanisika kunichangia...

SITAKAA NIISAHAU SIKU HIYO KATIKA MAISHA YANGU

Walimu wakiume walinipiga bila huruma tena si kwa fimbo,kaka yangu kuja naye akantandika kisawasawa!

Muda ule ule kengele ya mistarini ikagongwa,nikatandikwa tena na kila mwalimu

Nikaambiwa eti nimempiga mwanafunzi kisa kanikataa,baada ya kumpiga mwalimu akamkuta akiwa analia akamwambia atangulie ofisin,kutangulia baada ya kumuhoji ndipo Princess alipojieleza kwamba eti nimempiga kisa kanikataa mwalimu kuniuliza,nikawa kiburi alipo niadhibu nami kwa kuwa sina nidhamu ndipo nikampiga mwalimu,na kutaka kumuua...

Hili likiwa ni kosa la pili kosa la kwanza nilimwandikia barua ila binti alikukataa ukawa ukimsumbua ndipo alipoipeleka barua kwa mwalimu ukaitwa ukaonywa na pia ukapewa adhabu ofisini ila umerudia kosa...

Shule yangu aitavumilia huu upumbavu,pengine unafanya hivi kwa kuwa ni mtoto wa mwalimu ukijua uwezi fukuzwa wala kusimamishwa nikiwa kama mwalimu mkuu natangaza rasmi kwanzia sasa wewe si mwanafunzi wa shule hii,na siyo ivyo tu utakiwi kuonekana maeneo ya shule kwanzia sasa...
kaendeleeni na masomo...

Ndo Ikapita hiyo,sikupewa nafasi ya kujitetea,wanafunzi wakasambaratika,kaka alikuwa kanuna akusema kitu...

Nikaenda ofisini kwa mwalimu mkuu kujaribu hata kuongea naye nimweleze ukweli,hata akutaka kunisikiliza...

Sikuwa na budi kurejea darasani nikabeba begi langu NILIMKATA JICHO KALI PRINCESS ila naye alionekana kama kujuta alikuwa akintazama kwa huruma...

Rafiki yangu yasini akuongea kitu zaidi ya kuwa na uso wa majonzi,nikabeba begi nikatoka zangu kufika nyumbani nikamkuta kaka kumbe alirudi nyumbani!

"utakiwi kuonekana maeneo haya ya shule unafikiri utaenda wapi wewe si nilikukanya lakini,"

"hapana kaka tatizo ujui kilicho..

"Paaaaaaa"

Nilinyamazishwa Na Kibao Kikali kilichoita mpaka nikajihisi kutingishika kwa jino...

"masomo ndo basi na shule imekataa kukupa uamisho,nachokuomba toka kwangu utakiwi maeneo haya
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya tano

Kijana Ramadhan (si jina lake halisi) anaendelea kumsimulia mwandishi Maruma Mkasa Wa maisha yake...

Na sehemu ilopita tuliishia Rama anarudi kwao Moshi Ila ndani ya gari anakutana na mwanadada mrembo mfanyabiashara anayeahidi kumsaidia ikiwa atakubali,je Rama atajibu nini? twendelee

Kwa sekunde kadhaa nilimtazama yule dada machoni nikiwa na furaha ya ajabu,huzuni yote ikatoweka,nilikubali kwamba ni kweli Mungu huwa amtupi mja wake na pia huwa achagui wa kumpa!

"Sawa dada yangu ntafrah kama utansaidia kwanza mi naona hata aina haja ya mimi kwenda home watanletea noma bora twende wote tu!"

"Hapana Rama we nenda kwanza nyumbani ukawaeleze wakikubali utanijulisha mi ntakuja hapo nyumbani ntaongea na wazazi wako nikuchukue,siwezi kuondoka na wewe vuuu je ukipata matatizo huko,"

"Basi amna shida dada,"

Tukaendelea na stori ilikuwa ni kama tumetoka sehemu moja,yule alionekana kama dada yangu muda wa chakula tulishuka tukaenda kula yeye akanilipia tukarudi garini safari ikaendelea mpaka mjini Moshi,

Tukashuka stendi,

Kwa kuwa alipokuwa anafikia ni kwa babu yake aloitwa Sheghe Mohammed alokuwa akiuza madawa ya kiarabu au wengine uyaita madawa ya Kisunna Katika duka moja linalotazamana na msikiti wa riadha,akaniomba nimsaidie begi,

Nakumbuka Nilimsaidia begi mpaka hapo kwa babu yake akanandikia namba zake kwenye kikaratasi akanambia chochote nitamjulisha nakumbuka Moshi tuliingia mida ya saa kumi na moja,na alinambia kesho yake asbuh ndo angeondoka kurejea zake Dar,

Nikamwambia basi ntamjulisha,nakumbuka alifungua pochi yake akanipa elfu thalathin,sikukataa nilishkuru nikapanda ace za kcmc kuelekea nyumbani,binafsi nilikuwa nikiishi maeneo ya kcmc madukani

Ndani ya daladala nilikuwa nikiwaza tu,ni vipi ntapokelewa nyumbani,sikujua kaka aliwaambiaje nyumbani!,uzuni ikanirejea tena...

Taratibu Nikashuka kwenye daladala sasa nikawa nakata mitaa kuelekea makaz yangu...

Kadri Nilivyokuwa Nikipiga hatua kupafikia nyumbani ndivyo mapigo yangu ya moyo ya livyo ongeza kasi ya upigaji!

Nilitaman hata ningefika nyumbani usiku nikute mzee amelala ila ningeenda wapi sasa kupoteza muda?,ikanilazimu nikomae hivyo hivyo nikaufikia mtaa wangu...

"Mjombaaa" Watoto wa dada zangu walinikimbilia na kunipokea begi,sikutegemea wala kufikiri kama wangenikumbuka,walikuwa wakubwa sana

"Shamsia babu yako yuko?!"

Nilimuuliza mtoto mmoja wa dada yangu alokuwa ndo mkubwa kuliko hata yule mwenzake

"ndiyo,alikuwa anachukua udhu aende msikitini," dah kusikia vile ndo nkazidi kutetemeka,kwa bahati mbaya zaidi kitendo tu cha kufungua geti mzee huyo

"a..a..asalam..aleykum baba"

Nilitamka Kwa Uoga mwili wote ukitetemeka

"Waleykum Slam Rama Pole sana kwa safari..."

Baba aliitikia akiachia tabasamu,kitu ambacho sikukitegemea hapo kabla,tabasamu lake likaondosha hofu ambayo nilikuwa nayo,

"nimeshapoa!"

"ok we kapumzike wacha niende magharibi nikirudi tutazungumza"

Nikamwitikia mzee, nakuelekea ndani,mama na dada zangu walifurahi kuniona,nikapewa chakula nikala,

Yani kwa jinsi nilivyopokelewa sikufikiria,nikaenda kuoga mida ya saa mbili mbili nilikuwa chumbani kwangu nikijipumzisha...

Nikajikuta nikisahau swala la yule dada,nikapitiwa na usingizi kesho yake asbuh nakumbuka niliamka,mida ya saa mbili nikapiga mswaki na kunywa chai,ndipo baba alipo niita,

Sebuleni aliketi mama na baba,hapo ndipo baba alipoanza kunisema,alisema kaka alimpigia simu na kumwambia nimebadilika nimekuwa mlevi,baada ya kutoka shule uwa naenda mtahani narudi nyumbani usiku sisome,na mpaka ulipo mpiga mwalimu ukafukuzwa shule,sasa kama sisi wazazi wako tumeshindwa kukulea,kaka yako,shemeji yako wote wameshindwa kukulea dunia itakulea...

Kwa Kweli nilishangaa kusikia maneno yale eti mimi nakunywa pombe?,toka lini mimi nikanywa pombe,narudi nyumbani usiku toka lini mimi nikatoka nje ya uzio wa shule...

Sikutaka kuzikubali shutuma zile nikazipinga vikali sana,

"kwa hiyo kaka yako anakusingizia?,"

Baba akaniuliza kwa ukali,

"Ndiyo anansingizia,"

"na ilo la kumpiga mwalimu je?"

"huyo mwanamke mi sikumtukana ni rafiki yangu ila akaenda kusema mi ndo nimemtukana..."

"Kwa nin akutaje wewe na si mwanafunzi mwingine yeyote"

Nikanyamaza,

Wazazi waliongea siku hiyo,nilisemwa mwisho kaka akapigiwa simu Mama akamuomba kaka afanye juu chini nipate uamisho,

Kaka akasema kwa uamisho aitawezekana tena labda tu nisubiri mwakani ni ka apply chuo VETA,kaka akakubali kunilipia ada,nilifrah sana...

Sasa Ile namba ya Shuhaifa alipo nipa niliiweka ndani ya begi kwa bahati mbaya iliingia ndani ya daftari,sikujua...

Niliitafuta Sana bila mafanikio mwisho nikakubali imepotea...

Nikaachana nayo,

Nakumbuka Ilikuwa ni mwezi wa tisa,nikawa nikifanya kazi katika kiwanda kimoja cha maji kilichokuwa kikimilikiwa na mheshimiwa mbunge Ndesamburo Kwa Kipindi Icho,

Nilifanya kazi mwezi wa tisa mpaka wa kumi na mbili nikafanikiwa kununua vitu vyangu vya ndani ikiwemo kitanda,

godoro,na tv yangu...

Mwezi Wa Kwanza kaka akanilipia ada chuo fulani cha kulala ambapo nilichukua kozi fulani hivi ilikuwa ni kozi ya miaka mitatu,kaka akanlipia miezi sita muhula wa kwanza,

Hapo katikati kabla ya muhula wa pili kaka alipata matatizo kidogo yalomla ela
Ivyo hata ada ya kunsomesha mimi ikawa tabu ivyo sikuendelea na masomo....

Nikarudi Palepale Kiwandani,nikafanya Kazi hatimaye nilipanga chumba changu...

Nikayaanza Maisha yangu...

Siku hiyo nakumbuka nilikuwa nikitoka mjini,

Ambapo tulikuwa tukizungusha maji katika maduka,sasa baada ya kumaliza kuzunguka tuliagana na wenzangu nikawa naelekea kituoni kupanda daladala nielekee gheto...

"Ramadhan"

Ghafla nikahisi nikiitwa,sauti ni kama niliijua nikageuka sikuamin nilichokiona,

SIKUAMINI HAKIKA

Alikuwa ni Princess...

Princess nilo mwacha SINGIDA!

huku MOSHI kafata nini?!

Alikuwa Kavaa gauni chafu ambalo lilionekana ni la muda mrefu sana mwilini...

Alikuwa kakaa kwa mama ntilie mmoja akiosha mavyombo...

TARATIBU NIKAGEUKA NA KUMSOGELEA...
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya saba

Kijana Ramadhan (si Jina lake halisi) anaendelea na mkasa wake wa kusisimua na sehemu ilopita tuliishia pale kakutana na Princess Mjini Je Nin Kiliendelea?,twende Pamoja tujifunze zaidi

Nilisogea mpaka pale alipokuwa Princess Katika Kale Kakibanda,

"princess Ni Wewe?"
Nikauliza Kwa hamaki pasina kuamini kile nikionacho...

"ni mimi Rama habari za kwako,"

"salama vipi shule?!"

"dah nistory ndefu ila yote maisha"

"ah,ndo unafanya kazi hapa"

"ndiyo,mimi ni mama ntilie hapa karibu hata uwe unaniungisha"

Basi tulipiga stori mbili tatu hatukukumbushana ya nyuma,kila mmoja wetu alisahau,

kwa saivi unaishi wapi?"

"naishi kwa huyu mama maeneo ya kwa mtei,"

Basi,mimi nikamuaga akanipa namba zake nikampa zangu,

Tukaachana,

Nilielekea Mpaka Ghetoni nilipo oga,nikajipikia nikatulia sofani nikila huku macho yakiwa kwenye tv,ghafla mlio wa sms ukaingia kwenye simu yangu

'mambo'

Nikajibu 'poa P Za Kwako'

'salama Tu Rama Leo nimekuona nimefurah sana!'

'hata mimi pia'

'nimekumbuka mbal sana kwel penz letu ni la milele'

'mh!' nikaguna,nikaweka simu chini sikutaka kujibu ile sms,

'huyu binti kapagawa nini?!,yani alisababasha nikakosa shule akanifanyia vitimbi nikafukuzwa hata na kaka yangu,sasa leo hii bado anajihesabia ni mpz,nikajikuta nikicheka mwenyewe,

'mbona kimya Rama'

Akantumia meseji nyingine

'tafadhali naomba usizungumzie maswala ya mapenzi'

'kwani una mpz?'

'ilo halikuhusu'

Nikajibu Kimkato,akatulia hakutuma tena sms kwa muda huo niliendelea kuangalia tv mpaka saa nne nikaelekea chumbani kulala,ilipotimia mida kama ya saa tano kasoro akantumia msg nyingine

"najua nilikukosea sana Rama nipo tayari kupokea adhabu yeyote kutoka kwako ili mradi tu unisamehe,

Baada ya wewe tu kufukuzwa shule moyo wangu uliniuma sana,nami sikuweza kuendelea na masomo nikatoroka na kuja huku Moshi kusudi tu nikuombe msamaha,moyo wangu umekuwa ukiniuma,siku zote nimekuwa nikikutafuna pasina mafanikio,nimekuwa nikifanya kazi katika nyumba za watu,nimekuwa nikifanya kazi katika vibanda vya watu nikiwa na matumaini ipo siku ntakuona Rama,

Kweli Leo Mungu kasikia kilio changu nisamehe mpz wangu,

kwetu sikukosa kitu,pesa,malazi ila vyote nimeona havina thaman nimekufata wewe moshi

Naomba unisamehe Rama!

Kama vile alijua nimemaliza kusoma ile meseji palepale akanipigia nikapokea...

Princess alikuwa akilia...

Kama Nimasomo Rama niliona bora wote tukose,nimejuta mpz wangu nateseka uwez amin nalala kwenye kile kibanda cha mama ntilie,sina nguo nzur za kuvaa fikiria nimetoka singida kuja huku kwa ajili yako nisamehe Rama,binadamu atujakamilika,naomba nisamehe nirudi nyumbani nikaishi kwa aman...

Hata kama ni wewe ndugu msomaji usingeweza kutomsamehe,hasa sauti yake tamu tena ya kubembeleza ilo nakshiwa na kilio,nikajikuta moyo wa huruma ukinivaa usiku ule ule mida ile ile ya saa tano nikamgongea jamaa,mpangaji mwenzangu wa boda boda nikamwelezea kwa kifupi tukaelekea mpaka stendi katika kile kibanda alicho kwepo kweli tulimkuta ndani ya kibanda akiwa kalalia benchi,

Moyo Uliniuma Sana, akanikimbilia Na Kunipigia Magoti nikamnyanyua na kumwambia mi nimeshamsamehe kwa nin ile jioni aliniongopea kwamba anaishi kwa mtei kwa rafiki yake kumbe hana pa kuishi

Ukumbuke hiyo ilikuwa ni mwaka 2010 mwez wa 12 kipindi ambacho iltakiwa mwez wa kumi na moja ndo awe amemaliza form 4,lakin akanambia 2009 ile baada ya mimi kufukuzwa naye aliacha shule na kuja moshi kuntafuta,mi nikajikuta namwamini,nikamchukua mpaka geto,alienda akaoga,kesho yake nakumbuka nilimwachia elfu thalathin na tano akaenda kununua vijinguo maimoria...

Tukajikuta Penzi likizaliwa upya

Penzi Letu Likiwa na siku tatu siku hiyo akanambia...

"Rama kuna kitu nataka kukwambia sijui utakichukuliaje"

Nikamuuliza Kitu gani?,si ndiyo akanambia wakati akiwa analala kwenye kile kibanda mwezi mmoja ulopita aliwah kubakwa na wavulana watatu ambao akuweza hata ivyo kuzitambua sura zao,baada ya kumbaka wakakimbia akumueleza mtu yeyote siri ile ila kaja kujigundua ni mjamzito!

Nilishtuka,

Akaniomba sana nimsamehe, akupenda kubeba ule ujauzito,baba wa mtoto amjui kama kwel nampenda na nimeamua kuishi naye nibebe na lile jukumu...

Lilikuwa Ni swala gumu sana kwangu niliwaza sana,pasina kupata ufumbuzi mwisho nikamuomba ushahuri anti liz,yule mshahuri wa magazeti,ambapo alinambia kama kweli Nampenda,niishi Naye Na Kwa kuwa baba wa mtoto amjuh ni kubali kubeba yale majukumu,

Kwa Kuwa Ni Kwel nilikuwa nampenda,nilimsamehe nikamsamehe pia na hilo,

Siku hiyo nakumbuka nikamuuliza,

"princess hivi kweli unanipenda?"

"kwa nini unaniuliza ivyo Rama"

"nataka tu kusikia ukweli kutoka ndani ya kinywa chako"

"nakupenda,nakupenda,nakupenda sana Rama,kwa Nin Nisikupende Wakati Wewe Ndo Umenkaribisha Katika Ulimwengu huu wa mapenyi?,kwa nin nisikupende hali ya kuwa umensamehe hata kwa yale makosa makubwa niliyokukosea?,kwa nin nisikupende Rama,NAKUPENDA,NAKUPENDA NAKUPENDA SANA MY LOVE"

Kitu kingine alichojaliwa binti huyu ndugo msomaji...

kwanza alikuwa anamachozi ya karibu,alikuwa ana maneno matamu na sauti tamu ya kusihi,na pia binti huyu aliyajua mapenzi,

Ninaposema aliyajua mapenzi sima anishi ngono lah,japo pia hakuwa mvivu kitandani, alijua ku mu andle mwanaume,alikuwa kama ni kukufulia,anakupigia pasi na mwisho lile shati analipiga pafyumu,anakuvisha,nywele anakuchana...
mpaka aridhike na unadhifu autakao ndo utatoka nyumbani...

kalikuwa ni katahalamu sana tena sana kale kabinti!,

"nataka nikuoe princess kama kwel wanipenda naiman utokataa"

kakatoa macho,mdomo kameufungua kwa tabasamu la mshangao,kakanikumbatia machozi yakaanza kuchuruzika yenyewe...

"kweli RAMA unanioa mimi,siamin RAMA asante unanioa rama kweli?"

Kakauliza Kwa Furaha ya ajabu nikatabasamu,nikamwambia sitaki azae nje ya ndoa,nitamuoa na kweli NILIDHAMIRIA KUMUOA...
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya nane

Kijana Ramadhani (si Jina lake halisi) anatuendelezea mkasa wake wa kusisimua toleo lililopita tuliishia pale amemuomba Princess wafunge ndoa je nin kiliendelea?!

Tusonge...

Hakika princess alifurahi, kwa furaha ile akazidi kunidhibitishia na kumwamini kwamba ananipenda sana,pasina kutaka kupoteza muda siku ilofatia baada ya kutoka kazini nikaenda mpaka nyumbani, nikamweleza mama yangu nimepata mchumba na nataka kumuoa baada ya kugundua ana kiumbe changu tumboni hakika mama alifurahi,akanambia nimwambie na baba yangu,naye pia alifrah wakanambia nimlete nyumbani nikamtambulishe,

Kweli jumamosi nikampeleka wakasalimiana,nikamweleza mzee kuhusu mipango ya kumuoa kwani tayari alikuwa na mimba changa hili akijifungua awe ndoani

"Rama katika dini yetu ni haramu kumuoa mwanamke mwenye mimba,itakupasa harudi kwao akakae mpaka ajifungue ndo tupeleke posa mipango ndo ipo ivyo"

Baba yangu aliongea ila mimi sikukubali,nilijua kamwe Princess asingeweza kurejea kwao Singida

Nikamchukua Mwanamke Wangu tukarudi nyumbani tulipopanga,miezi ikazidi kwenda hatimaye mimba ikafikisha miezi nane kwa kuwa hakuwa na mtu wa kumwangalia nami kazi zangu zilikuwa za kusafiri katika kusambaza maji,nikamwomba mama ajifungulie nyumbani,kisha akishajifungua ndo tungeondoka kurudi tulipokuwa tunaishi,

Asingeweza kusafiri kurudi kwao na tumbo lake lile kubwa,wazazi wakanikubalia nikamleta nyumbani,akawa akilala na dada yangu...

Sikuacha Kumtumia hela ya matumizi wakati nikiwa safarini,niliporudi nilimletea zawadi,siku ya siku akajifungua,

Nakumbuka Siku hiyo ilikuwa ni saa sita usiku dada yangu aliponipigia simu hali yake ilibadilika ghafla tu nikamshtua rafik yangu wa bodaboda mpaka nyumbani bahati nzur jamaa yule wa boda boda alikuwa akijuana na dereva tax akampigia simu akaja tukambeba Princess tukamwingiza kwenye tax mpaka zahanati ilokuwa karibu,walijaribu kumzalisha ikashindikana wakatupa rufaa tukaelekea kcmc usiku uleule mpaka mida ya saa nane Princess alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike,

Alfurah sana,nilifurah pia,familia yangu yote ilijua yule ni mtoto wangu nilipewa pongezi,tukarejea nyumbani safar hii tulilala chumba kimoja tukitengwa na mtoto katikati,

Alikubali nikamuadhinia mtoto na kumpa jina zuri la Swalha,jina la mama yangu akakubali kusilimu nikamsilimisha na kumwita Zulfa,mtoto alipomaliza arobaini tukamtoa kwa maulidi,nikakubali kuingia gharama kwa ajili yake hakika nilimpenda yule mtoto kama mtoto wangu...

Baada ya arobaini si ndo mipango ya harusi ikaanza, ndugu walipotulazimisha tutoe namba za ndugu zao mwanzo Princess alipinga vikali,ila akaja kukumbuka ana mama mdogo wake Arusha akampanga alivyojua yeye siku ya siku mama mdogo wake akaja kumsalimia mtoto,kwa moyo mweupe akakubali kushiriki katika ile ndoa na akahaidi kumjulisha dada yake,walijua wenyewe walivyo ongea wote wakatupa baraka wakanipa mahari yao laki tano,nililipa zile mahari wakatoa ruksa tuendelee na ndoa,

Naumia sana kila nikikumbuka kilichoendelea, vikao vya harusi vikaanza, nikaanza kusambaza kadi ya michango,princess siku zote alionesha kufurah akuonesha tofauti yeyote katika uso wake...

Siku hiyo nakumbuka nilikuwa chumbani sasa kuna vocha nikawa nimetumiwa na rafiki yangu si ndo ikabidi nitafute karatasi niziandike zile namba ndo niziandikie kwenye simu,utaalamu wa kuzieditia kwenye simu sikuwa nao kwa wakati huo,nikafungua begi langu la zaman la shule na kutoa daftari haaa kufungua si ndo nikakuta namba,
Namba Za shuhaifa yule nilokutana naye kwenye gari kipindi kile zaidi ya mwaka sasa na miezi kadhaaa

Nikachukua zile namba na kuziingiza ndani ya simu yangu nikipanga nitafute siku nimsalimie...

Siku zikazidi songa hatimaye ikafika siku ambayo ilikuwa ndo mwanzo wa machungu kwangu....

Zikiwa zimebakia siku tatu kabla ya siku ya harusi yangu,ina maana siku hyo ilikuwa ni jumanne tuna jumatano tu,alhamisi siku ya kumpa mwanamke zawadi sijui ndo send off ile,ijumaa saa saba baada ya swalat jumaa ndo ndoa...

Naandika Nikiwa Na Uchungu Sana,wanawake si wakuwa amini,sijui nilimkosea nini mimi na kunipa adhabu kama ile,hakika sitokaa nimsahau yule mwanamke,kanipa jeraha la milele,

Siku hiyo ya juma nne alikuwa kaenda kuoga mi nikiwa chumbani ghafla simu yake ikaita,sikuipokea kwa kuwa si kawaida yangu kupokea simu yake...

Si Kwamba sikumuamini, lah,nilimwamini sana na pia nilimpenda sana Princess,ila Nasikitika Kusema Kwamba Yeye Akunipenda,muda Wote Kumbe alikuwa akicheza na hisia zangu....

AKAAMUA KUONDOKA NA MOYO WANGU

Simu ile ikakata,punde ikaita tena,ikakata ukaingia mlio wa sms kisha ikaita tena,kitu kikanambia si upokee nikaichukua kucheki mpigaji moyo ulinipasuka!

Nilikuwa Nimesimama, nikahisi Mapigo Ya Moyo yakiongeza kasi ya upigaji kiza kikawa kikitanda kizunguzungu kikali, nikakimbilia kukaa

ndipo kiza kikapita,simu ikakata,nikakimbilia kufungua text kulikuwa na meseji tatu,kutoka kwa ile ile namba ilo niumiza,na meseji mbili za mpesa,moja ni cha muamala wa sh laki tatu na elfu tano kutoka kwa jina la amede mghonja,meseji ya pili ni sh elfu sitini kutoka kwa jina lile lile...

Nikaachana na meseji zile nikaenda katika meseji nyingine,katika inbox
zote ziliseviwa my love meseji ya juu ilisomeka beby nimekutumia laki tatu na sitini na tano hakikisha kesho unakuja usije ukafunga ndoa love nijibu kama umeziona,

Nikashuka Meseji Ya Chini 'beby Nakutumia Nauli Na Pesa Nyingine Ya Akiba Sawa Mamy?"

Nikaenda Ya Chini ambazo sasa ndo zilishasomwa kuja juu ( yani Meseji za mwanzo au za nyuma tuseme)

"beby umefika?"

"pole sana mpz!"

Sasa Nikawa Sielewi Ili Nielewe Vizuri Nikaenda Sent Nasoma Alotuma Princess Narudi Inbox Alojibu Mtumiwaji bahati nzuri zaidi hakuwa mfutaji msg huyu mtu huu ndo ulikuwa udhaifu wake mkubwa,na alijiamini pia kwa kuwa sikuwa na kawaida ya kushika simu yake Meseji za namba nyingine sikuangaika nazo mi nili deal na za "my love"

umefika salama beby? (inbox)

ndiyo love nimefika salama ila sijui sasa ntaenda wapi love (sent)

tafuta chumba upange na kazi pia mi ntakuwa nakutumia pesa ya matumizi sawa? (in box)

sawa love (sent)

beby nimepata kazi kwa mama ntilie! (inbox)
hii ilikuwa ni ya siku za mbele kidogo kama baada ya siku mbili hivi baada ya yeye kuja

"beby nimemuona Rama ili kukupunguzia majukumu na hili nipate mtu wa karibu kuangalia mimba yangu niruhusu mpz niwe nae(sent)

princess unataka kunisaliti?!(inbox)

hapana love ila pale ninapoishi hakuna uangaliz mzuri,je nikifikisha miezi nane au tisa itakuwaje love?!"(sent)

"beby unataka kuolewa?!" (inbox) hapa kuna siku pia zilipita meseji alifuta

"hapana beby sipo tayari,lazima nitoroke naomba ntumie nauli"

Wakati Nikimalizia Kusoma Zile Meseji si ndo ghafla simu ikaanza kuita tena,ila nikawa nimeshapata picha ya kila kilichotokea...

Nikapokea Ile Simu huku nikitetemeka

"beby kesho asb ndo utasafiri au?!"

Aikuwa Sauti geni kwangu, japo ni muda mrefu sikuisikia ila niliitambua ni sir amede,mdomo ukabaki ukitetemeka kwa hasira ningeyaweka wapi macho yangu mimi,mchele kilo kadhaa,ng'ombe vitunguu nyanya ningewaangaliaje watu machoni,ama kweli mwanamke akitaka kucheza na akili zako...

Anazishezea kisawasawa

Shikamooni kinadada 😀😀😀

mama aliposema kuwa uyaone nilidhani ni maghorofa na vitambi ila kumbe akumaanisha ivyo ni matatizo kama haya...

Wakati Nikiwa katika butwaa lile si ndo princess akaingia,mwili wote ulikuwa ukintetemeka,nikampa simu,akaangalia yule mpigaji pasina hata chembe ya uoga akapokea palepale nilipo,

"nilikuwa bafuni naoga my...
umeshatuma?,sawa asante kesho na gari la asubuh"

mh,ndugu msomaji,sikuamin nilichokuwa nimekisikia,laki tano yangu?,mama yake na hata mama mdogo wake baraka zile walizonipatia je,wote ni wasanii au?,mbona sielewi,katika ndoto mbaya nilihisi ile ni mbaya zaidi

"ke..ke..kesho unaondoka?"

Nikamuuliza Kwa Kigugumizi,unajua Sikuamin eti! yah sikuamin lile lililotokea
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya Tisa

Ramadhan bado anaendelea na mkasa wa maisha yake yalo mtokea na katika sehemu ilopita tuliishia pale kagundua usaliti alofanyiwa na Princess Je nin kiliendelea...

TWENDE PAMOJA TUENDELEE KUELIMIKA NA KUBURUDIKA PIA...

Unajua zamani nilikuwa sijui kwanin sisi wanaume wengi ukwepa kuishi na wanawake walokwisha zaa au kubeba mizigo ya watu pindi mwanamke akiwa katika tabu ya kukataliwa na wenye mizigo hiyo!,

Japo si wote wenye tabia za kugeuka nyuma na kumrudia baba watoto,kuna swali Moja ningependa kuwauliza wasomaji,hivi mwanamke ikiwa umeshaolewa na huyo mwanaume alokuoa anamjal vizur tu mtoto wako,je una haki ya kutafuta mawasiliano ya x wako na kuhitaji msahada pesa ya matumizi kwa mtoto wako!,je ni sawa kuwa na namba zake na kuwasiliana naye?!...

au kumfata na kuhitaji ukaribu naye kisa kukusaidia katika malezi ya mtoto!

Twendelee na mkasa wetu....

Baada ya kumuuliza swali lile,Princess aliachia tabasamu,alitabasamu pasina kujal napata maumivu kiasi gani katika moyo wangu...

"Rama naomba unisamehe kwa yote yalotokea sikuwa na jinsi,najua nimekuumiza kwa mara nyingine nisamehe Rama ntakweleza ukwel,mimba hii sikubakwa ila ni sir Amede alinipa wakati nikiwa form 4 niliogopa kumtia aibu,nikajua atafungwa je ni nani angemlea mtoto wangu na kwa kuwa amede alikuwa anajenga Singida mjini,akanambia nitoroke mbali Arusha au Moshi,kwa Kuwa na ma mdogo wangu Arusha sikutaka kufikia Arusha nikaja huku Moshi,amede alinipa ela nyingi tu ambazo ningeweza kujikimu ila niliwaza juu ya mimba yangu ntampata wapi mwangaliz wewe ndo ukatokea,nisamehe Rama"

"kwa Nin ukubal sasa kuolewa kama unayajua haya yote?"

"ningekataaje kwa mfano,hata kama ni wewe,ningekataa ungejua sikupendi ila sikupanga kuolewa na wewe na mpenda sana Amede,mahari yako sir atakurudishia niache niende,hata kama ukinlazimisha utokuwa na furaha kwa kuwa sikupendi Rama,"

Ndugu msomaji unajua maana ya kuchoka, nilichoka,wapi ningeweka macho yangu,ilibaki siku moja,yani jumatano,siku ambayo alipanga aondoke,alhamis sherehe zianze 'send of' ijumaa ndoa wapi ningeweka macho yangu mimi,tungeieleza nin kamati ya harusi,michele tulonunua,dah jasho lilitapakaa mwili mzima,nikajikuta napiga magoti mbele yake...

Nilichanganyikiwa eti!,

"nisamehe Princess,kama kuna lolote nililowah kukukosea kuliko hii aibu unayotaka kunipa nakuomba usiondoke nakupenda Princess"

"hapana Rama kwa kweli,utampata yule umpendaye yupo ila si mimi,mimi ni wa Amede"

Binti yule aliongea pasina hata chembe ya huruma nilimuomba na kumuomba ila alikazania msimamo wake lazima kesho yake asbuh aondoke zake,ghafla wazo fulani likanijia,tena ghafla tu,unajua unaweza ukamuona mtu mjinga ukisikia kanywa sumu kisa kakataliwa ukamshangaa ila si yeye kuna roho inayo mtembelea na kujikuta akitamani au kukifanya kitendo kile,

Ilikuwa Mida ya saa mbili tukiwa kitandani nikawa mwenyewe sasa nawaza kikao cha mwisho cha kamati milion tatu na laki kadhaa zilikusanywa,watu wakijitutumua nikawa nikiwaza sasa nimesimama mbele ya watu,wamama wa kiswahili ntawaeleza nin wapi alipo bibi harusi,nitajibu nin,kila nkipita nje ntakavyokuwa nanyooshewa vidole kakimbiwa, kakimbiwa, hapana asee sitoweza kukubali gharika hiyo ya aibu inifikie bora kufa,kuliko kupatwa na aibu hiyo,hapo hapo nikanyanyuka na kwenda kununua vidonde panadol nikaja navyo nyumbani

"princess,si una amua kuondoka,sasa utaondoka mimi nikiwa mfu,sitokuwa tayari kuipata adhabu hii"

Palepale nikameza vile vidonge vilikuwa si chini ya vidonge kumi,si kukawia tumbo likaanza kuuma,

"haraka princess akaenda chukua maziwa fresh kwenye chupa alokuwa akiyanywa akawa sasa akininywesha tumbo linakata ila nkawa nafumba mdomo,machozi yanatoka,naye pia sasa akawa analia...

"siondoki tena tafadhali kunywa haya maziwa, nimeamin unanipenda mpaka wataka kujiua kisa mimi nisamehe Rama sito ondoka kweli tena nakuomba kunywa,"

Nguvu sasa ziliniisha nikajikuta nafungua mwenyewe mdomo si kwa kupenda,akanimiminia yale maziwa,akamimina mengine kwenye kikombe na kuninywesha,

Tumbo Lilikuwa likikata,mwili wote ukiweweseka,

Princess mara aende huku mara kule,

"unajisikiaje nikamwite mama..."

palepale nlipandisha kutapika,nilitapika,chakula chote nlichokula,nikatapika yale maziwa tumbo likawa likinguruma,wallah nikasema ndo nakufa sasa,mwenzangu akazidi nipa maziwa dah kwel sitakaa nisahau hiyo siku...

Princess akadeki yale matapishi bila kinyaa,akapiga magoti,huku machozi yakimbubujika,

"sito ondoka tena,nimeamin Unanipenda,nisamehe kwa haya yote yalotokea sitokuumiza tena Rama nakuapia,wewe ndo mume wangu usifanye hivi tena"

Princess aliongea kwa hisia,hata kama ni wewe ndugu msomaji ungemuamin,nami nikamuamin ila nikamwambia...

"princess,najua Unaniongopea Wala Unipendi Wewe...

"wallah Nakupenda Rama Nimeamin Unanipenda eti,nipo tayar kesho kutwa kuwa mkeo...

"unipendi princess,ila ombi langu kwako ni moja tu kubali tufunge ndoa hii aibu ya kifamilia ipite baada ya ndoa tukirudi kwetu mi ntakupa talaka uondoke utakuwa umeokoa maisha yangu na aibu pia nikubalie kwa hili"

"hapana Rama mimi sitokubali unipe talaka hata ukiniacha sitapata atakayenipenda atakayekubali kujitoa maisha yake kisa mimi nakupenda baba Swalha"

Akanikiss Shavuni,moyoni nikacheka baada ya kuniita lile jina baba Swalha yani Swalha yule mtoto wake nilihisi akini injoy kabisa ila sikujali

Nikatoka nje kusukutua nikajipiga maji kurudi chumbani binti akanikimbilia na kunikumbatia akiwa tu na kamtandio kilichoendelea nikile cha wanandoa na ilikuwa ni mara ya kwanza toka ajifungue,penzi la siku hiyo lilikuwa la tofauti toka nimemjua yule mwanamke,tulichoshana ila yeye alinchosha zaidi hatimaye nikapitiwa na usingizi....

Nilikuja kushtuka saa kumi na moja,japo nilikuwa na haya kufanya zinaa kabla ya ndoa,nikaenda kukoga kutoa janaba nikaelekea zangu msikitini,kuswali swalat subuh,jumatano hiyo,kesho yake ndo send off,ijumaa saa saba ndoa!...

Baada ya kuswali si ndo nikarudi nyumbani, chumbani,Princess na mwanae na hata nguo zao hazikwepo kitanda kilitandikwa vizuri net ilikunjwa juu kuangalia vizuri pale kitandani si ndo nikakuta barua,nikaisogelea nikaichukua na kwanza kuisoma....

Iliandikwa hivi....

Kwako Rama,

Najua utaumia sana baada ya kuusoma ujumbe huu ila nisamehe sina uamuzi mwingine zaidi ya huu,

Kuondoka,

Jana ulinshangaza wewe ni mwanaume wa ajabu sana wajiua kisa kukataliwa mh ulinshangaza kwa kweli ungekufa sijui ningewaeleza nin wazaz wako, usije ukarudia tena kitendo hiki chaguo lako lipo litakuja!

Rama mi si wako kuhusu aibu ningekubal kuolewa na wewe kwa jinsi unavyonipenda najua usingenipa talaka ndo maana nikatoroka zangu ukijiua tena sitahusika na kifo chako ahsante kwa msaada wako MUNGU atakulipa tutaonana

Rama usiangaike kunifatilia

baybay

Wako princess....

Nilishtuka kwa barua ile palepale nikampigia simu namba azikupatikana nikajua tu lazima huyu binti hatakuwa kantoroka,na hatakuwa ajafika mbali nikatoka mbio, kuelekea stendi, nikijua fika hakuna gari linaloenda singida mida hiyo mpaka saa kumi na mbili na nusu ivyo lazima ningemkuta tu,chap nikadandia bodaboda mpaka stendi...

kweli niliwah!...
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi

Kijana Ramadhan Iddy (si jina lake kamili) anaendelea na mkasa wake wa kusisimua toleo lililopita tuliishia baada ya kutorokwa na Princess anaamua kumkimbilia stendi akijua pengine anaweza akamkuta je nin kitaendelea?!

Twende Pamoja!

Kufika stendi kwa bahati nzuri niliwahi,sikukuta gari hata moja ilo ondoka nikakagua gari ziendazo singida zote lakini ndani sikumkuta Princess,nikakagua Mpaka Za Arusha,bado sikumuona mpaka gari zote zikaondoka!

Sasa nikawa najiuliza kichwani kwangu!

'kama princess ayupo kwenye haya magari atakuwa kaenda wapi?"

Nakumbuka nilikaa pale stendi mpaka saa tano, nikimpigia simu hapatikani, mpaka nikapata mawazo au usikute yupo nyumbani hapana wazo la kwamba yupo nyumbani nikalipinga baada ya kuikumbuka barua ile!

Ili Kuhakikisha nikampigia dada yangu mmoja na Kumuuliza Princess yupo chumbani?!,akanambia nisubiri atanijibu badae ripoti ni kwamba ayupo!

Sikutaka tena kurudi nyumbani,kawaida yangu nilikuwa nikiifadhi ela kwenye simu nikaenda nikazitoa zote,nikanunua line mpya,nika amishia zile ela kule nikachukua namba ya mtu mmoja tu

Shuhaifah!

Palepale nikampigia alishtuka sana nikamwambia mi ndo nipo kwenye gari nakuja alifrah akanambia nisijali nafasi yangu bado ipo hakika nilijiona mtu mwenye bahati,kuipasua ile 'line' nilikuwa na maana ni ili nikitafutwa nyumbani nisipatikane,wenyewe watajua jinsi ya kuzima soo...

Nakumbuka tulikuwa tukiwasiliana na alisema nikifika ubungo tu nimshtue,hatakuwa stendi kunipokea,sasa kwa bahati mbaya Dar ubungo pale niliingia usiku,nikamwambia kabisa nimefika si nikashuka!...

Sikujua hata ni sa ngapi simu ilichukuliwa huko mfukoni ila ninachokumbuka palepale stendi baada ya kuangaza macho na kutokumwona kuna mahali mama mmoja alikuwa akiuza visoda soda vijuisi nikawa nimekaa pale sasa si ndo nikasema nitoe simu kuwasiliana naye tena!

Kucheki Mfukoni amna kitu, nilishtuka,na siyo simu tu hata elfu 40 ilokuwa kwenye huo huo mfuko niliotia simu pia azikwepo na fedha nyingine zilikuwa kwenye ile line yangu mpya,ambavyo mbaya zaidi aikuwa na namba zaidi ya namba za Shuhaifah,dah kwa kweli nilichoka,ukicheki ni usiku,njaa ikawa inauma,sina simu ya kuwasiliana na mwenyeji wangu,namba zake kwa kichwa ndo sizijui,laini ile ndo mpya namba zake zenyewe sikuzishika, nilimpigia mtu mmoja tu naye namba zake sikuzikaririsha!

Kwa mara ya kwanza nikajigundua kuwa ndiyo nimekaribishwa mjini, nikajiona mpumbavu kwa kuivunja ile laini eti nikipigiwa nisipatikane, nikajilaumu bora tu ningekuwa nayo kwenye mfuko sasa si ningechukua namba huko za Shuhaifah,ntakuwa mgeni wa nani ndani ya jiji hilo...

Niliendelea kuzunguka maeneo yale ya ubungo nikishangaa shangaa kule walipokuwa wanauza uza vitu,nje sasa ya kule stendi...

Ilipofika Mida ya saa saba nilitafuta mahali nikalala, asubuhi kulipopambazuka niliendelea kuzurura maeneo yale ya stendi na nje nikitegemea kumuona Shuhaifah Bila Mafanikio mwisho nika amua kuondoka nikiwa sasa nishakata tamaa

Mida ya saa saba saba katika kuzunguka zunguka maeneo yale ya ubungo ni kafika katika carwash moja,nikaenda nikaongea nao nikawaambia bwana mi nimetoka Moshi nimekuja huku kutafuta maisha toka asbuh sijala sijabahatika kuonana na mwenyeji wangu simu nimepoteza,

Wale washkaji walinicheka kwa kweli!

"mangi hapa ndo dar,mtoto wa kiume kama umekuja pambana mbona utatoboa tu,alafu nawakubaligi wachaga kinoma leo tupo wote hapa kesho na kesho kutwa unaduka kubwa kariakoo,wachaga wametoboa huku town kama msela kakukwepa usife moyo mi kwetu moro ila nipo geto tutakaa wote utapiga kazi utayaanza maisha mapya"

Kwa kweli niliuzunika,kuanza maisha mapya,home kule nilikuwa na kazi nzuri naliwa vizuri,nilisha jinunulia vitu vyangu vyote nisahau nianze upya?!

Yote ni kwa sababu ya Princess,nikajikuta Nikimchukia zaidi ya kitu chochote,

"Nimeamini kweli unanipenda,mpaka unataka kujiua kwa ajili yangu sitokuacha Rama'

Nikakumbuka Ahadi yake ile siku nilivyomeza mavidonge alafu asb yake tu anantoroka!

Niliumia kwa kweli,masela wakanipokea nikafanya kazi pale kwa muda mrefu nikikaa na jamaa,huyu chalii Aliitwa Pius,ndiyo nilikuwa nikikaa geto lake...

carwash pale nilifanya kazi wiki mbili kwa siku tukilipwa 3000 aijalishi umeosha magari,pikipiki ngapi mimi kwa kwel sikuridhika na ile kazi,nikaanza kujitanua katika kutafuta marafiki zaidi,nikampata Jamaa angu mmoja alikuwa akiitwa John huyu alikuwa akifanya kazi kiwanda cha Bakhera kile pale tazara akaniita pale wanalipa 7000 kuingia saa mbili mpaka mbili usiku wewe ni kubeba tu gunia za unga tena unakimbia nazo muda wa kupumzika ni saa saba wakati wa kula (vijana wa Dar) Wanaofanya Kazi Viwandani nadhani wanajua hii ishu...

Mi pale kwa baresa nikaamia nikawa nikipiga shift yani naunganisha hata siku mbili nkaondoka na 28 nikapumzika siku moja,siku ilofatia nikaunganisha tena,ela nilotoka nayo nikapanga chumba na pale nikakimbia...

Maana niliona hapa asee naweza kufa!...

Nikaamia Kiwanda Kimoja Cha Sabuni Za Poa,kiwanda Cha Mo,muda Ni Ule Ule saa mbili mpaka mbili usiku,ila hapa kazi aikuwa nzito,japo walilipa 3000 ela unachukua kwa wiki,kiwanda iko kipo tbt,kituoni pale,wakati huo nakaa matumbi...

Siku zikasonga,hatimaye nikanunua kitanda,kochi langu moja ka tv ka deki na ka compyuta,chumba kikawa kinamuonekano,siku ya siku nikajikuta naanzisha mahusiano na mwanamke mmoja aloitwa Salma,huyu alikuwa ni mzaramo tulikuwa tukipiga nae kazi kulekule ndani japo naye alikuwa kapanga,mahusiano yetu yalikuwa kwa kasi mpaka tukapanga plan ya kuoana,kuishi pamoja tatizo likawa kumtambulisha kwa wazazi alihtaji iko kitu au tu nimlete nyumbani,

Nilimpinga Vikali si nilijua nyumbani nilishaharibu,kwao walikuwa wakintambua na nilikuwa nikiishi naye,ila ndugu zao na hata yeye wakawa wakinilazimisha nimuoe,mimi nikakubali ila sikuwa tayari kuwaambia nyumbani kwanza hata namba zao sikuwa nazo,
wenzangu wakachachamaa..
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi na moja

Kijana Ramadhan Maulidi anaendelea na mkasa wa maisha yake alokumbana nayo,sehemu ilopita tuliishia, baada ya kutua jijini Dar es sallam na kuyaanza maisha anajikuta akitokea kumpenda Salma Walokutana Kazini,je nini kiliendelea twende pamoja uendelee kujifunza...



"Hivi Rama unanipenda kweli na una malengo ya kuishi na mimi au lengo lako ni kunichezea tu mimi!"

Salma aliniuliza kwa sauti ya upole,sauti tamu!

"nakupenda sana tena sana Salma nawe nadhani unalijua hilo!"

"unan'danganya Rama,kama Wanipenda Kwa nini utaki kunitambulisha kwenu?,kwanin hutaki tuuoane kwa nin lakini?"

Dah niliishiwa pozi nikabaki kimya,unajua toka Salma aamie pale nyumbani ninapoishi ilikuwa ni siku ya tatu,alinambia yupo kwenye 'period' ivyo hakukubali ni mguse,wiki ile ikakatika,wiki ilofatia ilikuwa ikifika jioni anakosa raha ule uchangamfu wote anaupoteza na hata pale ninapo mgusa anakuwa mkali mara najisikia vibaya mara naumwa na tumbo,mpaka sasa nikawa siuoni umuhimu wake kuishi naye pale,japo kupika alinipikia,kufua alinifulia ila tatizo likawa kwenye tendo la ndoa!

"hivi unajua Salma mimi nimechoka?!,hivi mimi na wewe ni ni mtu na dada yake au?"

"kwa nini?!"

"sijaridhia aya maisha tunayoishi bora tu uondoke zako kama uwezi kunikidhia aja zangu"

"Kama ni Ivyo Rama mi ntaondoka ila siwezi kuikurubia zinaa hakuna mtu anayetuona ila Malaika na hata Mungu Pia wanatuona tulivyofanya huko nyuma vinatosha mpaka unioe ndo utaujua mwili wangu"

Nilicheka Kwa dharau,

"niujue mara ngapi huo mwili wako kipi hasa nisichokijua hapo"

"kama unaujua kwanin sasa unauhitaji!"

"kwa kuwa ni haki yangu!"

Nikajikuta naropoka,

"haki yako wapi? umenioa mpaka uniite mimi haki yako? kama una la kuongea bora tu unyamaze ulale zako!"

"ahaaa unajifanya ustadhat siyo,swala tano etie basi usingekuja kuishi na mwanaume kesho usepe zako una maana kabisa wewe"

"sawa mi ntaondoka kama ndo unahitaji ivyo,kama umenileta kwako kukidhi haja zako unitumie uniache mi ntaondoka ila sipo tayari kufanya unachotaka abadani asilani"

Kila mtu akalala kivyake tukiwa tumenuniana,Salma ghafla alibadilika akawa mtu wa ibada nilimchukia kwa kweli

Asubuh jumamosi hiyo niliamka zangu atukusemeshana, baada ya kunywa chai mi nikaelekea kwa jamaa angu mwenye banda la movie palepale matumbi nikawa nikitazama,kupoteza poteza muda

Ilipotimia mida ya saa sita ghafla simu yangu ikaita kumcheki ni Salma,kwa kuwa nilimnunia sikutaka kuipokea ikaanza kuita tena,

Nikaikata...

Sikukaa Sana nikapigiwa kwa namba ya ba mkwe,hii ni namba ya baba yake Salma huyu alikuwa muhabi yani wale waislamu wenye itikadi Kali na ndo maana hata walikuwa wakinilazimisha nimuoe mtoto wao

'mmh kuna nini tena!'

nikawaza nikatoka nje ya banda lile kuipokea hiyo simu katu sikujuwa nilichopangiwa au ninachoenda kuambiwa...

"Asalam aleykum mzee"

Nilimwamkia kwa adabu

"walekumssalam kijana nakuomba hapa nyumbani mara moja kuna kitu nahitaji tuzungumze"

Nilishtuka!,nikajua Lazima Salma hatakuwa kashaenda kusema umbeya kule kwao,

"sawa mzee wangu nakuja mida hii"

Wala sikurejea ndani tena ya banda nikaelekea mpaka nyumbani kwa kina Salma alipozaliwa nilijua nitamkuta!

Nilipofika Nilikaribishwa Sebuleni,

Nilishtuka kuikuta familia nzima pale sebuleni niliwakuta Watu siyo chini ya kumi,baba yake baba wadogo zake,wajomba dada zake wengine sikuwajua pia alikwepo sijui ndo Sheghe yule au ustadh mi sijui bhana!!

Hata Salma Mwenyewe Pia alikwepo nikaoneshwa sehemu ya kuketi nikaketi

Sasa moyoni nikawa nawaza

'Hii kesi gani inasikilizwa na familia nzima!'

Baba mkwe akaniambia...

"Rama mwanangu tumekuita kwa swala moja kwa kipindi
cha wiki kadhaa sasa unaishi na mtoto wetu kama mume na yeye mke tunahitaji kujua je ni kweli Unampenda Salma?,na Upo tayari awe mkeo maana katika vitu binadamu tunavyopaswa kufanyiwa haraka cha kwanza ni kumzika mtu anapokufa na cha pili ni kuozesha watoto walokwisha pendana ustadh yupo hapa cheti cha ndoa hiki hapa binti huyo hapo atakutajia mahari yake tuwafungishe ndoa maswala sijui ya sherehe ni hapo mtakapojipanga nyinyi na familia zetu ila kwa sasa tufanye hili swala chap ukaishi na mwenzako kihalali

JE UPO TAYARI TUWAFUNGISHE NDOA CHAP MUISHI KAMA MUME NA MKE KIHALALI?!"

Watu Wote sasa wakawa wakintazama mimi nikajikuta naona aibu nikajibu

NDIO NIPO TAYARI KUMUOA SALMA"

Watu pale wakafurah,Salma akaambiwa ataje mahari yake

Cha ajabu sasa kilichonshangaza na kunifanya mpaka Leo hii ni mkumbuke yule mwanamke na kumuona ni wa ajabu katika maisha yangu na ni wa ajabu pia katika mabilioni ya wanawake wote duniani

Ni hiyo mahari alonitajia!...

"mahari yangu nahitaji anisome sura til yasin,na ayatl kurusii kama zawadi yangu na sadaka yangu pia"

Cha ajabu hata familia pia aikushangaa baba akaagiza ukaletwa msahafu

Nikakabidhiwa nilikuwa natetemeka nilihisi kila kilichokuwa kikiendelea ni ndoto

Nikafungua ule msahafu nikasoma zile sura nilizotajiwa baada ya kumaliza ndipo tulivyofungishwa ndoa cheti kikaandikwa tukala cha mchana palepale saa kumi kila kitu kikawa kimekamilika tukaruhusiwa kuondoka zetu!

"sasa nipo maridhia kwa kila kitu juu yako mume wangu!"

Salma alintamkia huku akiwa na tabasamu jepesi,

"hivi imekuaje mpaka wazaz wako wakatufungisha ndoa ya mkeka?"

"Rama katika uislam hapana ndoa ya mkeka ila ndoa ni maridhiano ya watu wawili kuishi pamoja na kujenga familia,hiyo ndiyo ndoa mambo ya sherehe dufu ni mbwembwe tu"

"kwa hiyo amna kigodoro?"

"mmmh Rama acha hizo bwana,sasa lini utanipeleka Moshi nikawaone wakwe zangu,kule ndo kwetu saivi"

"usijali mwisho wa mwezi huu tutaenda,tutakaa mwez wote wa kumi na mbili,mwez wa kwanza tutarudi,"

"ntafurah mpz!"

Basi mi nikaendelea na kazi kama kawaida,nikawa nikitoka saa 12 narudi saa 2 usiku jumamosi na jumapili ndo nilikuwa free hata ivyo sikupenda kukaa sana nyumbani...

Siku zikasonga hatimaye baada ya kupoteza mawasiliano na kukaa mbali na nyumbani kwa muda wa mwaka mmoja na nusu hatimaye mwez ule wa 12 tukafunga safari kurudi Moshi,safari hii nikiwa na mke wangu niliyo mpenda zaidi ya kitu chochote

SALMA!
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi na mbili

Kijana Ramadhan (si Jina lake halisi) hatimaye anafunga ndoa na binti Salma,na Sasa wanaelekea nyumbani je nini kitakachoendelea huko!

tusonge.

"Rama mbona unaonekana una mawazo hivyo mume wangu!"

Salma alinihoji baada ya kuona tofauti niliokuwa nao,nilikosa uchangamfu sikuwa na hamu kabisa ya kwenda nyumbani,

Unajua toka kipindi chote nimeishi naye sikuweza kumuelezea mkasa wa maisha yangu kwamba nilikimbiwa na mwanamke nami kukimbia kuja dar, ikapaswa nimuadisie kila kitu kusudi hata tukifika asiwe mgeni na stori atatazokutana nazo

Salma alinipa pole na kuniurumia pia,

"na ndo maana ulivyokuwa ukinambia habari za nyumbani nilikuwa nakataa binafsi ukadhani kwamba mimi sikupendi ukwel Nakupenda Sana Salma"

"hata mimi Nakupenda sana Rama"

Basi safari iliendelea tukipiga stori kwa bahati nzuri kwangu gari iliharibika njiani,tukapoteza muda,hatimaye ilivyokamilika tukaendelea na safari,kichwa kilikuwa kinauma kwa ajili ya upepo nahisi pengine na mawazo tele yalokizonga kichwa changu!

Hatimaye tuliingia Moshi mjini usiku nakumbuka ilikuwa mida ya saa tatu tukapanda daladala za kcmc

"shusha kcmc madukani"

Tukashuka sasa tukawa tukielekea nyumbani,

Watu mtahani walikuwa wakitushangaa sana kwa kuwa tulikuwa tukiishi maeneo ya uswahilini ila sikujali,niliowajua niliwasalimia,walonisalimia niliwaitikia,tukafika mpaka nyumbani nikagonga,dada yangu akaja kufungua...

"Ramaaaa"

Aliniita Kwa Sauti Kubwa huku akinipokea begi,mama kusikia jina langu limetajwa huyo akaja akanikumbatia akawa akitaka kuninyanyua hakika kwa jinsi walivyo nipokea sikutegemea!

Tukapewa viti tukakaa,

"ndo ukafanyaje tena Rama mkatutoroka na kututia aibu kiasi kile haya huyo mwenzako yuko wapi na huyo mgeni ni nani?"

Mama akaanza kunipasulia hapohapo,

"ni stori ndefu sana mama yangu,ila namshukuru Mungu yamepita huyu ni mke wangu anaitwa Salma,nimemleta aijue familia yake!"

"karibu mwanangu mimi ndo mama mkwe wangu,baba kalala kesho utamsalimia Rama nakuomba mara moja"

Mama akaniita tukaelekea sebuleni,nikimwacha Salma na mawifi zake...

Nilipofika sebuleni nikaketi mama akaanza kunilaumu kwa kitendo nilichokifanya, mama aliongea kwa uchungu akisema heti mimi na Princess tulitoroka na hatukutaka kufunga ndoa,kwanin kama atakutaka kufunga ndoa kwanin tulikubali siku ya mwisho kutoroka,

Nikatanguliza Kuomba radhi nikamueleza mama mi sikwamba nilitoroka ila Princess alintoroka?

"kama alikutoroka kwa nini na wewe ukaondoka na wote mkazima simu mkawa ampatikani?!,sijui kesho utamweleza nini baba yako na ndugu zako kwa aibu mlotupatia mtahani ukaona aitoshi leo tena unatujia na kimwanamke eti mke wako kama ni ndoa baba ulishaichezea sijui utaongea nini ueleweke wewe?!"

"huyu ni mke wangu mama na mpaka ndoa tushafunga"

"unasema?!"

Hapo nikawa nimempandisha mama wa kichaga kichaa,mama aliongea,nilimtaka radhi alinilaumu hasa kwa kuoa bila kuwapa taharifa na pili akupenda kabisa mimi kuoa mzaramo,mama alinipinga vikali,

"kama ni mwanamke sema utafutiwe lakin si kutuletea wanawake wasotambulika hata ubini wao!"

Mama aliongea,nikajitetea na kuielezea familia yao ni watu wa dini,jinsi ndoa ilivyokuwa msimamo wa binti na hata mahari,

hapo ndipo mama kidogo aliponielewa, baada ya kuridhika jinsi nilivyomuelezea familia ilivyo,napia nikampigia mama mkwe mama akaongea naye hapo ndipo aliposafisha roho akampokea Salma Kwa Mikono Miwili,tukapewa Chumba baada ya kila mmoja kuoga tukala tukaenda kupumzika,

Kesho niliamka nikamkuta Salma Kashaamka yupo anaosha vyombo akadeki uwa,alikuwa ni mpiga kazi mzuri kuliko hata Princess,

Salma alikuwa mchangamfu, alipomaliza shughuli zote

Tukaitwa na baba,nikajieleza na kumtambulisha,kwa upande wa baba hakuwa na maneno mengi sana akatupa baraka pia aliongea na baba mkwe wangu wakafrah!

Amani moyon mwangu ikarudi tukatoka sebuleni na kurejea kule nje

Tulimkuta Mama akiwa anachana nywele zake

"mh mama una nywele nzuri embu ngoja nikusuke"

"mh Ntafrah mwanangu maana...!"

Salma akaelekea kumsuka mama nywele,mimi nikaingia zangu chumbani,chumba chetu kilikuwa cha kule nje...

Wakati nikiwa kule ndani ghafla nikasikia kishindo cha mtu kama kadondoka,si ndo nitoke nje,

Sikuamini nilichokiona Salma alikuwa chini akiangaika kujipiga piga ghafla akatulia!...

Mama na dada zangu walikuwa wakimwangalia kwa mshangao!

Nikamkimbilia Salma pale chini nikaanza kumwita Salma!,Salma!,Salma!...

"Rama mdogo wangu umeoa mwanamke mwenye kifafa?!"

Ghafla nikashtushwa na sauti ya dada yangu!
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi na tatu

Kijana Ramadhani bado anaendelea na mkasa wake wa kusisimua alokumbana nao na katika sehemu ilopita tuliishia wakati yeye akiwa chumbani nje anasikia kishindo kutoka anamkuta mkewe kadondoka na kupoteza fahamu,

Je nin kiliendelea?!

twendelee...

"sasa nyie badala mumsaidie mnasimama mnamwangalia ndo nini lakin hii!...

Kwa Kweli sikupendezeshwa na kitendo kile nikamkimbilia mke wangu nikawa nikimwamsha!

"Salma! salma! salma..."

"mwache ni kifafa icho hata amka mwenyewe"

Mama yangu aliongea maneno yale kwa kweli sikuyapenda unajua mimi na hasira za karibu nikajikuta nageuka na kutaka kusema kitu ila namshukuru Mungu sikukisema ila mama aliniona jinsi nilivyochukia,

"nawe Zamzam msaidie mdogo wako kumnyanyua huyo wifi yenu mumpeleke chumbani"

Ndo dada yangu akaja kunisaidia tukamnyanyua na kumwingiza chumbani, tukamlaza...

Yale Mawazo kwamba ule kweli ni ugonjwa wa kifafa ayakuni ingilia akilini kwa sababu nilishaishi naye kwa muda mrefu japo mara nyingi nilikuwa bize na kazi nikirudi usiku kwa usiku...

Ivyo bado nilikuwa na wasiwasi nilimshika kichwa na kumsomea baadhi ya sura ili kama kuna pepo baya lilimkumba litoke ila hapakuwa na mabadiliko yoyote...

"Ramaaa" Ghafla nikasikia mama yangu akiniita haraka sana nikaelekea nje kumsikiliza!

"hivi imekuwaje ukakubali kumuoa mwanamke mwenye kifafa je ujui familia yako yote itakuwa na huo ugonjwa?!"

"mama lakin unauhakika gani kama ule ni ugonjwa wa kifafa?!..."

Kuongea Vile mama akacheka

"usitake kuniambia kwa muda wote ulokaa naye mpaka wazazi wake kuamua kukuozesha ulikua ujui kama ana huo ugonjwa ina maana ujawah kumuona akianguka?!"

"hapana mimi sijawah ndo mara ya kwanza leo,"

"basi ndo ivyo ndo maana hata familia yao ikakuozesha kwa nguvu tena bila mahari ha ha ha ha nikashangaa familia gani wanakubali kumwozesha mtoto wao kwa yasin, ikhlas pamoja na ayatl kurusi maajabu hayo"

Kwa maneno yale nikaona kama mama ananidhihaki,mi nikanyanyuka tayari kuondoka!, wakati nikiondoka mama akawa akizidi nikera kwa maneno

"ndo umwandikie talaka tofauti na ivyo nitawapigia hao wa kwao niwapakiee yani wamekuona wewe ndo wakukubebeshea mwanamke mgonjwa..."

"mama umuogope Mungu,"

"nimuogope Mungu Nini!"

"kwani Umempima Ukamkuta na huo ugonjwa au unaongea tu mama!"

"ina maana wewe mtu mwenye kifafa umjui,alivyokuwa amekakamaa pale chini ukumuona?,akishtuka umwite niongee naye kwa kina!"

Sikujibu kitu nikatoka zangu nje,na kuelekea chumbani kwangu,nilimkuta Salma bado ajashtuka nilikaa naye pale mpaka akaja kushtuka, kwanza aliniangalia kwa khofu akawa kama anajiuliza nini kilichotokea ndipo nilipomweleza kuwa alianguka ghafla nje nikambeba nikamwingiza ndani,

Salma wa watu alionekana kuogopa,

"ndugu zako wamesemaje wameogopa?!"

Aliniuliza huku akiwa na khofu usoni,khofu ambayo hata mimi binafsi ilianza kunitia shaka!

"hapana wala ila Salma embu nambie ukwel unaugua kifafa?!"

Kumuuliza Vile Salma wangu akaanza kulia,nikazidi kumshangaa!

"sasa kulia ndo una maana gani au ndo jibu la swali nililokuuliza?!"

"nisamehe Rama,nisamehe sana mume wangu kwa kukuficha katika kipindi chote tulichoishi wote ila nakuomba Rama nipo chini ya miguu yako usiniache,usiniache Rama,nikwel Na huo ugonjwa na niliogopa kukwambia kwa kuwa usingekubali kunioa,usingekubali kuishi na mimi,wanaume wawili waliniposa ila walipoambiwa ugonjwa wangu walisitisha kunioa,na ndipo wazaz wangu walipoamua kufanya siri pia niliolewa na wanaume wawil ambao nao pia waliniacha punde tu walipogundua na huu ugonjwa naomba nawe usiniache Rama nilindie aibu yangu ntakuwa mgeni wa nani mimi kuachika mara tat...

Salma Kwa Kweli alilia , aliumiza moyo wangu nikamnyanyua pale chini na kumkalisha kitandani!

"Salma mke wangu unakufuru sana kwa kusema kwamba
eti huna bahati ya ndoa unakufuru sana,mimi si kama hao waliopita nimeshakuoa nitaishi na wewe kwa hali yoyote ambayo ningekukuta nayo,uwe umeathirika,uwe sijui na kifafa au sijui kifoto,tayar tushafunga pingu kuachana ni mauti,ila ulicho nikosea ni kutoniweka wazi tu hapo ndo nitakapogombana na wewe!"

"niliogopa mume wangu ila nisamehe babaa"

"basi sawa twende unaitwa na mama! alafu umeumia hapa kwenye paji la uso..."

Niliongea huku nikipapasa usoni alipoumia taratibu ule uvimbe...

"mama ananiita?! pana usalama kweli"

"we twende mke wangu utaenda kujulia hukn hukn"

Basi Salma akashuka zake kitandani tukatoka nje,ambapo mama ndo alikuwa akimaliziwa maliziwa kusukwa na dada yangu Zamzam

"mh Wifi karibu chukua kiti..."

Yule dada yangu akawa akimkaribisha kwa kumpa stuli alokuwa kaikalia

"wala hata usijali wifi we kaa umsuke mama stuli si ile kule"

Salma akaenda kuchukua stuli akaja akanipa kisha yeye akarudia kigoda kilichokwepo jikoni akaketi!

"pole sana mwanangu kwa kuanguka!"

"asante mama nimeshapoa!"

"ni ugonjwa gani huo mwanangu unaokusumbua"

"mama lakini nini?!,nimeshazungumza naye tumeelewana sipendi bwana umuulize hayo maswali!?"
Nikaingilia nikianza kuchukia...

"naomba uondoke hapa uniache nizungumze na mkwe wangu!"

mama akaongea kwa ukali akinikata jicho!...
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi na nne

Samahani Kwa kuchelewa kuuleta mkasa huu ni kutokana na siku mbili hizi kujisikia homa homa,ok twendelee...

Toleo lililopita tuliishia mama anahitaji kuongea na mkwe wake hivyo Rama Ikabidi awapishe je unahisi nini kiliendelea twendelee...

Basi nakumbuka nilitoka na kwenda kwa rafiki yangu jirani tu tukawa tukipiga piga stori mpaka mida ya saa mbili nilipoelekea msikitini, nilipotoka nikarudi zangu nyumbani,

Sikumkuta mtu nje wote walikuwa vyumbani mwao,nikaingia zangu chumbani,nilimkuta Salma kalala kageukia upande wa pili!

"my love!"

Nilimwita Kwa Sauti ya taratibu nikimfata pale kitandani,

Tofauti na mategemeo yangu akuitika,nikazidi kupiga hatua na ghafla nikasikia kwikwi,ishara kwamba alikuwa akilia,

"Salma unalia nin mpz,kipi kimekukuta mke wangu"

Nikamuuliza huku nikimgeuza aniangalie,

Macho yalikuwa mekundu kuonesha kwamba alilia muda mrefu!

"una nini lakini wewe?!"

Ghafla akanikumbatia kwa nguvu huku akizidi kulia,

"ni bora tukarudi zetu tu Dar,hapa mi sitoweza kuendelea kuishi!"

"kwa nin unasema ivyo?!"

"hapana mi naomba tu tuondoke!"

"ok,itabidi kesho ufue kesho kutwa tuondoke"

"hapana Rama kesho asb tuondoke,na usipofanya ivyo mi ntakutoroka na kurudi dar"

kwa kweli nilishtuka kwa kauli ile, atatoroka?, nikamkumbuka Princess,naye alinitoroka,sikuwa tayari swala hilo lijitokeze tena,

Ila nilijua lazima mama yangu hatakuwa kamwambia maneno yalo muumiza mwanamke yule na kumchoma,basi muda ule ule nikamwambia amke na kupanga vitu vyake,tukala tukalala,ila hakuna alopata hata tone la usingizi kati yetu,

Mpaka panapambazuka, Salma akaamka na kubandika chai,tukanywa

"mama mi nimeona turudi zetu Dar"

"lakin Mbona ghafla hivyo yani mmekaa siku nne tu na ulisema mnakaa huu mwez wote"

"sipendi kukaa mahala ambapo apampi amani mke wangu,"

Mama akakunja sura,

"lakini nilikwambia huyu mwanamke mgonjwa...

"kwa hiyo kama ni mgonjwa ndo hastahili kuolewa,embu fikiria kama ndo ungekuwa wewe ndo huyu bibi kwa upand wa baba akufanyie unayemfanyia huyu ungejisikiaje...

Palepale Mama Akanipiga Kibao...

"mtoto Mpumbavu Wewe Nikuzae Mwenyewe Nikulee Leo Unijibu unavyotaka ondoka na usirudi hapa kwangu!"

"ndiyo sitarudi,na wala sitatia mguu tena hapa katika nyumba yenu labda niwe maiti naondoka ndiyo..."

Nikaongea hasira zikiwa zishanipanda nikamshika mkono mwenzangu tukaondoka,

Wakati nikiwa kwenye gari simu ikawa ikiita ,kuangalia ni mama nikaikata mwisho nikaizima kabisa...

Baadaye mama baada ya kuona sipatikani akampigia mwenzangu,mama ananipigia...

"hapana kupokea"

Nikamwambia tena kwa kumgombeza,baada ya kuona anataka kuipokea nikamnyang'anya na yenyewe nikaizima na kuziingiza mfukoni,sikuziwasha mpaka tunaingia Dar

Ndipo nilipo mrudishia mke wangu simu yake nami kuwasha yangu meseji zikaanza kuingia kwenye simu yangu!

"pokea simu mwanangu tuzungumze"

"mh ndo umeamua kuizima kabisa"

"mwanangu naomba unsamehe na pia uniombee msamaha kwa mwenzako kwa yote yalotokea najuta kwa niliyoyaongea sikujua kama unampenda sana mke wako maneno ulonambia yanantesa mzaz wako,nisamehe mwanangu"

Wakati namaliza kusoma ile meseji mama akapiga!
nikapokea...

"mmefika salama wanangu?!"
Mama akiwa na furaha,

"ndiyo nimefika salama,"

"poleni kwa safari!,upo na mwenzako hapo?!"

"ndio,una muulizia wa nini?"

"mpe simu niongee naye"

"umtukane tena au?!"

"Rama mwanangu usiwe ivyo ngoja..."

Ghafla akakata punde simu ya Mke wangu ikaita nikamwangalia kwa jicho kali!

"ni mama huyo?!"

Nikamuuliza,akatingisha Kichwa huku akijibu...

"ndiyo mume wangu ni yeye"

"hapana kupokea"

"lakini Rama!"

"hakuna cha lakini au wewe umefurahia jinsi alivyokutukana,au unapenda aendelee kukutukana?"

"ni mama yako lakini..."

"hata kama angekuwa bibi yangu"

Salma akabeba simu yake na kutoka nayo nje,

"ndo unaenda wapi sasa?!"

"naenda chooni"

"Chooni ndo uende na simu embu lete hapa"

Salma akanipa ile simu ambayo bado iliendelea kuita cha ajabu akarudi kukaa kitandani!

"sasa si umesema unaenda chooni?"

"mume wangu! naomba jamani nimpokelee mama"

Baada ya Salma kuomba sana mwisho nikampa simu yake,ilikuwa ishakata akampigia mama...

Sikusikia Kitu Mama alichokuwa akimwambia,ila yeye alikuwa akijibu "usijali mama...nimekuelewa mama...sawa mamaa,...mama usijali nishakusamehe...kweli mamaa niamini,...sawa mamaa...nitamwambia..sawa mamaa,.kuwa na amani mama..nakupenda pia mamaa,na wewe pia mama usiku mwema...inshaallah"

Salma akakata simu nuru ya furaha ikionekana katika uso wake,mi nilijidai eti kununa

"mume wangu nikwambie kitu!"

"kisihusu maswala ya mama"

Akanifata Pale Nilipo Kuwa Nimekaa Kochini akachuchumaa kwa chini mikono yake akaiweka kwenye mapaja yangu...

mdomo akawa kaung'ata kimtego...

Mwanamke Yule alikuwa ni mtundu wa kushawishi,alinshawishi mpaka nikajikuta moyo unakuwa mweupe nikampigia simu mama,tukaongea vizuri tu dukuduku baina yetu tukalimaliza!

SURA YA TATU

CHANZO CHA USALITI CHANIFUKUZISHA DAR

Maisha yaliendelea kama kawaida,hatimaye Mke Wangu alikuja shika ujauzito...

Hakika nilifurah sana,nakumbuka siku hiyo ikiwa ramadhani ya mwisho yani kesho yake ilikuwa iddy nikiwa nimeenda kariakoo kuchukua bidhaa za dukani,katika duka nililokuwa nikiuza,
Wakati Nikiwa njiani katika duka moja nikavutiwa na hijabu moja,nikataman kumnunulia mke wangu kwa kumsapraiz kusudi aisherekee vizur sikukuu yake,lilikuwa ni zuri hakika,na nilijua pengine ni elfu thalathin mpaka hamsini,

Nikajongea Maneneo Yale nikakuta kuna binti mmoja alikuwa akiuza nikamuuliza bei!

"samahani dada ili hijabu hapa ni shilingi ngapi?"

"laki na themanin na tano"

"hee bei ya mwisho?!"

"laki na themanin"

"kiru nacha ela yote hiyo!"

"kwani wewe una shilingi ngapi kaka?!"

"elfu arobaini,au kisa kesho sikukuu nini ndo waniuzia mara tano kasoro yake ?"

Yule dada na wote waliyekwepo pale wakaangua kicheko!

"bei hiyo aifah kaka mwisho ndo hiyo laki na themanin nilokwambia"

"dah poa basi ngoja nijikatae"

Wakati nageuka kuondoka ghafla nikasikia nikiitwa nyuma yangu...

"Ramaaa"

Sindo Nikageuka,sikuamini Macho Yangu,

Shuhaiyah

Sikujua hata alitoka wapi, alikuwa pembeni ya yule dada! nikarudi...

"Shuhaifa ni wewe?!"
 
MKASA WA KWELI

KAONDOKA NA MOYO WANGU

MWANDISHI; ZUBERI MARUMA

WHATSUPP 0759427653

Sehemu ya kumi na tano

Kijana Ramadhani ana fanikiwa kuonana na Shuhaifa Kariakoo Wakati alipoenda kuchagua hijabu kwa ajili ya mke wake je unadhan nin kiliendelea tumalizie mkasa wangu huu wa kusisimua

Basi nilirudi Shuhaifah alifurah sana alitoka kabisa na kuja kunikumbatia!,

Tulisalimiana cha ajabu akanipa namba zake

"vipi ilo hijabu la elfu 40 ulitaka umnunulie wifi nin?!"

Nikaona aibu hata kumjibu akatungua lile baibui akalifunga vizuri na kulinipa kama zawadi nikampe mke wangu,kiukwel nilifurah akanambia atatafuta siku aje anisalimie,tukapeana namba za simu,tuka agana!

Kiukwel sikuwa na mawazo ya kimahusiano na mwanamke yule,ila nilishangaa siku hiyo, akintumia meseji za kimtego,akuishia hapo akaniaomba sikukuu tuonane tutoke,kweli sikukuu nilionana naye tukaenda kwenye hotel nzuri na mwisho tukajikuta tukichukua chumba,kwa mara ya kwanza nikamsaliti mke wangu,

Shuhaifa aliniahidi mambo mengi sana ikiwa kuniajiri kwenye super maket yake moja na kuniahidi kunilipa laki tatu,

Kwel nilianza kazi kwenye ile super maket,penzi letu likiendelea kwa siri alinipa kila nilichotaka na sikuwah kumwona na mwanaume...

Napia kitu kingine sikupajua sehemu alipokuwa akiishi zaidi ya ofisini kwake hapo hapo Kariakoo,

Siku zikasonga hatimaye mimba ya mke wangu ikafikisha miez saba,

Siku hiyo nikiwa kazini alikuja bwana mmoja mwarabu tena alikuja na maaskari!, akawaoneshea wale maaskari mimi palepale nikabebwa mpaka katika cruzar ya polisi,sasa sikumjua yule mtu ni nani,

Nilipelekwa kituo kidogo cha polisi nikashangaa natuhumiwa eti nimeiba milioni kumi,nililala siku mbili pale kituoni sikuruhusiwa kumjulisha mtu yoyote nilikuwa nikipigwa nikiambiwa nitoe zile hela,

Siku ya siku nikatolewa pale kituoni mpaka segerea,

Kwa bahati nzur segerea nililala siku moja kesho yake nikaitwa baada ya kuambiwa kuna watu wamekuja kuniona kwenda nilimkuta yule mwarabu na Shuhaifah, ambapo Yule mwarabu alinambia yule ni mke wake wa ndoa na mahusiano yetu aliyajua siku nyingi tu ila alichokuwa amepanga ni kunifunga maisha ila kutokana na mke wangu kwenda kumlilia na tumbo lake kaamua kuniachia kwa sharti moja tu

NIONDOKE DAR

na laiti akigundua bado naendelea kuishi Dar kitakachofuata ni kunitwanga risasi,

Shuhaifah naye akanieleza kwamba yule ni mume wake,kwel alimkosea ila hatorudia tena,nami akanisihi vilevile niondoke jijin Dar!

Nashkur walinipa ela kidogo, siku ilofatia tulirudi Moshi, nilimuomba Msamaha mke wangu kwa yote nilo mtendea kweli alinisamehe ila alinisisitiza kuwa makini, nilipofika Moshi tulirudi kwa wazazi,

Ilikuwa ni ngumu kwangu kupata kazi ila nilipambana, nilikuwa tayari kubeba mizigo stendi na hata masokoni nilipopata hela nilileta nyumbani ingine nikiweka akiba kwa ajili ya kujifungulia mke wangu!

cha ajabu toka mimba ikiwa na miezi mitatu Dar kule akuwah kuanguka,wala sikumwona na dalili yoyote ya kifafa mpaka tukahisi amepona,ila mimba ikiwa na miezi saba ghafla alianguka na mbaya zaidi aliangukia tumbo,

Mimi Nilikuwa Kazini Nikapigiwa Simu Ila Nilipofika Hosptalin Nilikutana Na habari nyingine...

Mke Wangu Pamoja Na Mwanangu Alokuwa tumboni wote awapo tena duniani!
Salma wangu akawa amenitoka,

*KAONDOKA NA MOYO WANGU*

Hii ilikuwa ni mwaka 2007 mwanzoni,nilimpenda sana tena sana Salma,ila mola alimpenda zaidi!

Namuombea huko aliko Mola Ampe makazi mema

kwa sasa sijaoa wala sifikirii tena kuoa ,bado nipo Moshi na ndo yalipo maisha yangu kwa sasa!

kwa taharifa nilizowahi kuzipata kwa kaka yangu ni kwamba Princess aliolewa na sir Amede,na Kwa Saivi Wamebahatika Kupata Mtoto Wa Pili...

Nnachoamin Lile alikuwa chaguo langu,ila chaguo langu ndo ilo lililoondoka na moyo wangu!



Hapa ndo mwisho wa mkasa wetu kesho tutaanza mkasa wa dada Shamim ambapo safari hii tutaenda nao mpaka mwisho!

MWISHO
 
Back
Top Bottom