Dr Willibrod Slaa
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
- Thread starter
- #161
NANU,Nadhani, haya yote yamekuwa yakitokea. the difference is only that..this time CHADEMA as opposition has a stake in it and akina Dr. Slaa were reading it carefully between the lines and were able to interpret each and every line on the adverse effect it will during the coming elections.
For sure if you go through all other muswadas there must be some changes which they may call it minor but have been changed after the parliament meeting. We don't have legislators eager to do proof reading of what has been enacted as the law compared to the parliament hansard, etc.
The problem for JK is that he is becoming also too transparent compared to his predicessors and he want the public to be informed of everything for reasons ofcourse well known to him!
Thanks. Labda niseme tu hii si mara ya kwanza kwa kitu cha namna hii kutokea.Huko nyuma sikumbuki ni mwaka gani, lakini wakati wa AG Andrew Chenge, iliisha kutokea tukio la namna hii. Wabunge tuliigundua katika hatua ya Kamati Bunge lililofuata. CPD (wakati huo marehemu Lushagara alibanwa, na AG ni timu yake walikiri kufanya makosa) CPD alionywa kama sehemu ya adhabu na ikaishia pale. Tatizo ni kuwa sasa wanatafuta majibu rahisi badala ya kukiri na kuomba radhi, ikiwa ni pamoja na kueleza nia ya kwanini waliichomeka jambo ambalo hata wazo lake tu halikuwasilishwa Bungeni. Angalau kwa lile la wakati wa Chenge wazo lilikuwepo. Hili hata wazo na wala mjadala haukuwepo wa aina yeyote kuhusu " Approving Authority".
Ni vema pia ikajulikana kuwa kwenye hili imekuwa rahisi kwa kuwa Sheria yenyewe imepatikana mapema. Kwa kawaida nakala ya Sheria inachelewa sana kupatikana kiasi kuwa hata mtu mdadisi inakuwa vigumu kuipata na kuichambua. Nadhani haya ni mazingira ya nchi yetu ambayo yanatufikisha hapa tulipo.