Wakipekee
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 5,361
- 9,235
"Kuna Maisha baada ya uchaguzi"
Hii ilikua kauli ya Mzee jakaya kikwete akiwaasa watanzania wasichanganyikiwe na mambo ya uchaguzi wakasahau kua kuna Maisha mengine ambayo ndio halisi baada ya hicho kipindi kidogo chenye hulka na mambo mengi ya ajabu..
Jana ilitoka list ya wachezaji walioitwa timu ya Taifa kwenye mchezo wa kirafiki, list hiyo ilitoka na hoja kubwa ya kukosekana beki wa Kati anayekipiga kwenye club ya wananchi Dar Young Africans. Hii ilishangaza sana wadau wa mpira kutokana na kiwango chake cha juu Sana iweje asiitwe timu ya Taifa?
Kumbuka Job ni moja Kati ya wachezaji wachache Tanzania waliopita kwenye MFUMO mzuri maana kacheza ngazi zote za timu ya Taifa kuanzia under 17,19,20 hadi senior timu iweje leo atemwe?
Hii inshu ilianza zamani Kule AFCON alikua hapangwi makusudi tu wakasingizia "hayuko fiti/ana majeraha" lakini baada ya Jana kumuacha na maswali kua mengi "chawa" wamekuja na majibu mepesi kua "Hana uzalendo" eti alikataa kucheza beki 2.. hahahhaha wakati wao wenyewe ndio waliosema kipindi kile alikua na majeruhi... Anyway ili Mbwa apigwe lazima Kwanza apewe jina Baya... Utasikia anakula mayai..
Haya mambo hayajanza Leo tangu enzi za kina Kaseja walikua wanaachwa bila sababu za msingi ukiuliza utaambiwa anavuta bangi... Tuliona Kapombe na Mohamed Hussein zimbwe jr waliachwa bila sababu baada ya kelele kua nyingi Zimbwe akarudishwa Ila pia inshu ya Kapombe ilianzia mbali Sana kuna kipindi walimbagua kwenye zawadi Hadi pale Samata aliposema atagawana nae zawadi yake ndipo wanaona aibu wakampa haki yake...
Ni juzi Tu walimuaacha Kelvin John bila sababu baada ya maswali mengi wakasema Hana nidhamu
Anyway za ndaaaaaaaani kabisa kuna kikundi cha "kitapeli" ambacho hupenda mambo ya TEN PERCENT hawa ndo watakufanya watakacho pale utakapokataa kutoa KITU KIDOGO ili upangwe...
JOB piga kazi kumbuka wewe ndio umebeba tuzo ya Beki Bora NBC PREMIER League 2023 so watabana kusini utapita kaskazini.... Kama alivosema jakaya kuna Maisha nje ya timu ya Taifa, wewe utakua Legend kwenye klabu Bora ya Yanga pambana..
Fid Q aliwahi kusema "kizuri ni kizuri lakini chenye ubora ni Bora" ipo siku atakuja kocha mwenye akili timamu atakuita na utacheza soka...