Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

cha
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni


Cha msingi ni afya,kama uko fresh potezea,katika maisha tunakutana na vitu Vingi sana,vingine hutakaa usimulie maisha yako yote mpaka unaingia kaburini.tafuta muda ukae nae uongee nae umueleze jinsi unavyofeel kwa kile alichokufanyia.kila mtu ana historia yake,mengine hutakaa uyaseme.lakini pia kama unafikiria kuendelea na kesi sawa tu but uwe tayari kupoteza vingine pia.am sure kwa asilimia kubwa mchumba wako atasepa,aibu pia kwa familia kwamba binti alipata mchumba then akasepa.yako mambo mengi pia but kama utapima na afya kuwa ok,kwa maoni yangu potezea.

haya ni maoni yangu,ndivyo navyofeel but wewe ndiyo muamuzi wa mwisho
 
Kwanza kabisa kapime Mimba na HIV, kwa miaka hii sikutegemea kama kuna wanaume bado wanatumia hizi mbinu za kizamani,Mwanamke kama hataki kwasababu za msingi mwache aende zake...wapo wengi. Pole dada.
 
Msamehe tu, ila mpe Onyo na ikiwezekana mdai pesa ndefu sana.
Baada ya hapo hizo document uangalie namna ya kuzihifadhi asije kua alikupiga picha na baadae akatake advantage au akataka kukufukuza kazi..
 
Huwez kumpenda aliyekubaka,fuata moyo wako,utakuja jilaumu,mpende aliyekupenda mwanzo,hatakama hana.kitu achana na.mbakaj utakuja juta huyo.hafai
 
Na kuongezea tu huyo mchumba wake alikua anajua kuwa mkewe mtarajiwa kuna lift kila siku huwa anaitegea...?

Una akili sana mdogo wangu!

Ingawa kwa sasa tuache kumuuliza maswali hayo na tuseme tu HILI LIWE FUNZO KWA WENGINE WENYE TABIA KAMA YAKE.
 
Pole kwa yalio kusibu aiseeee....
Pamoja na kwamba una majeraha ya mwili na roho.... nikuombe kwa heshima ya jf nivema ukuje utuletee mrejesho wa kitakacho jiri
 
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni

Dada yangu kwanza pole sana.
Pili, kitendo jamaa alichokifanya ni jinai kwa mujibu wa sheria ya jinai (SOSPA) na kama akikutwa na hatia anaweza 'kufichwa' gerezani miaka ningi;
Tatu, kumtunzia hiyo siri si suluhisho kwani huyo ni ' mbakaji mzoefu' ukimwacha basi kuna hatari ya binti mwingine kuwa 'victim' wa huyo bazazi;
Nne, jamaa ajali utu wa mwanamke na ni kiumbe atarishi katika jamii

Nini cha kufanya:

Mosi, kaa kimya; au
Pili; kaa kimya na uishi na dhamira ya kuwa 'mtunza siri' wa mbakaji (sexual predator);
au simamia utu wako kama mwanamke na kuendelea kupigania haki yako ya msingi kwa kuendelea na hiyo kesi ( fungua kesi pia kesi ya madai, bibie ikibidi).
 
Sasa hapahapa dar hakuna hata alieisha unveil identity ya hawa wahusika?

Maana kama kuna wafanyakazi wenzao humu ni rahs ku connect dots

Boss - Tegeta
Mtendwa - Bamaga
Juzi kati - Sherehe
- bi dada kuumwa na kulazwa
- na lazima kazini hawako kwenye good terms

Hapa kama upo karibu nao hasa kiofisi lazima uwe umesha wajua, la sivo hii story ni shigongo type.

hahahaha... kabisaa hujakosea inspector Dagliesh...
 
We hate rubbish!
Siku zote ukifanyiwa kitu unatakiwa kuwa na maamuzi kama umekubali na kuwa kimya na kaku please means brain yako ninaongozwa kama sisimizi!
What else should we tell u?
 
Ila wanawake tujifunze kama mtu huna hisia nae unamzoea ya nini?kweli aanze tu karne hii kila siku kukusubiri au kukupitia kituoni?we unamlipa kitu gani?mtu kama huna hisia nae achana na botu vyake,anyway inabidi nae apimwe afya na ujue hali yake kwa ujumla,kisha muandikishiane kwa mwanasheria ok?sikunyingine utaingiliwa kinyume na maumbile we jiachie tu
 
Baadh ya wanawake kwa kupenda ndoa!!!!
Pamoja na ulichofanyiwa bado unawaza kama anafaa kuwa mumeo!!!

Muachie mungu afanye kazi yake
 
Duh hii nomaaaaa.. Kapime ngoma usije ukampatia huyo mchumba wako. Baada ya hapo chukua maamuzi.
 
duuh...jamaa hana utu....anastahili kupelekwa mbele ya sheria( lakini uamuzi ni wako) .....ninajaribu kufikiria hapa wangapi washapitiwa kwa style hii....
 
Wanawake wanapenda sana fever burebure, na kuwaona wanao toa fever wajinga. Jifunze kuishi kwa kujitegemea mahusiano yenye viashiria vya mapenzi achana nayo, kama humhitaji huyo mtu. Lkn kama na wewe ulikuwa kwenye mipango sawa.
Lkn ana mke na umri wake wa kuishi bila mke, na sababu kama hana ninini alishawahi kuwa na mke sababu gani zilimfanya aachane na mkewe. Lkn kama hajaoa ni kwa nini hajaoa anaumri gani chunguza ukiona sababu za kuridhisha nenda mahakamani, ukiona mtu safi muoane

...eti hapa kuna walakini kuhusu hulka ya huyu mwanamme... Mtu ana kazi tena position ya juu nzuri kabisa, ana makazi yake mwenyewe fresh kabisa, he owns a car and so forth... sasa inakuaje hana hata kabinti kakubambikizia hapa mijini? dar es salaam hii hii kweli? hatua zote hizi kweli ambazo ameshapiga kimaisha? how old is he...
 
Ila wanawake tujifunze kama mtu huna hisia nae unamzoea ya nini?kweli aanze tu karne hii kila siku kukusubiri au kukupitia kituoni?we unamlipa kitu gani?mtu kama huna hisia nae achana na botu vyake,anyway inabidi nae apimwe afya na ujue hali yake kwa ujumla,kisha muandikishiane kwa mwanasheria ok?sikunyingine utaingiliwa kinyume na maumbile we jiachie tu
Ukute kashaingiliwa.. Nakusalimu lalamaliwato
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom