Kanisani

Kanisani

Chukua na hii! Mwalimu wa dini(sister) alipokuwa akiwafundisha watoto wa darasa la 7,kuacha dhambi ili waende mbinguni,...mbinguni ni mahali pazuri, huko hamna kuoa au kuolewa, hamna kiu ya maji, hamna njaa! Huko ni raha tu! Mwisho sister/mwalimu akauliza ni wangapi wanapenda kwenda mbinguni? Wanafunzi wote walinyosha mikono juu kuashiria wapo tayari kwenda mbinguni,isipokuwa m1,Bernadeta Membe. Sister alipomuuliza kwanini hataki kwenda mbinguni, alijibu, mama ameniambia nikitoka hapa nirudi nyumbani!
 
Back
Top Bottom