Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,433
Jana nilienda kusali kwenye kanisa moja mitaa ya kati.
Huko mhubiri alikuwa bize kuuponda mchezo wa soka kuwa ni wa kishetani uliotawaliwa na uongo na hila.
Akasema mchezaji anapompiga chenga mwenzake anakuwa amedanganya, maana anakuwa anamdanganya kuwa anaenda kulia wakati anaenda kushoto.
Akaendelea kusema wanapoangushana na kuchezeana faulo wanakuwa wanavunja amani na wanafanya uadui.
Pia akasema wachezaji wanapojiangusha kutafuta penalt wanasema uongo.
Akatoa kali zaidi kwa kusema fifa na kombe vya dunia viliundwa na shetani mwenyewe na akavileta duniani ili kuwapofusha watu.
Watu wawe busy na mpira na kumsahau mungu.
Akawashauri waumini wake waache kabisa kufuatilia michuano ya kombe la dunia inayoendelea afrika ya kusini.