Sakata la kuchoma makanisa limeendelea tena baada ya kanisa la Baptist Vingunguti kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane na robo.
Watu wasuojulikana walionekana kwenye eneo hili la kanisa na kuwasha moto,nyumba jirani kuna binti alitoka kujisadia kwenye choo kilichoko nje,na ndipo alipoona vijana wakitokomea na huku kanisa likiwaka moto,ndipo alipowaamusha wasichana kutoka kwenye familia ya mchungaji Hezron Mwaisemba na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.
Wasamalia wema waliamka na kuanza kuuzima moto kabla haujashika kasi. Kwa mujibu wa mchungaji Hezron amesema vijana hao walikuwa na chupa ya mafuta ya petrol ambayo waliyatumia kuchoma,waokoaji walikuta chupa ya mafuta, kiberiti na kisu kikubwa yaliyopatikana kwenye eneo la tukio, vitu vyote hivyo vimechukuliwa na polisi waluofika kanisani hapo usiku huo.
Kanisa hili liko mtaa wa Mtambani, kitongoji cha Faru kata ya Vingunguti.
Watanzania wapenda amani tutafakari kwa makini nini suluhisho la jambo hili. Nafanya juhudi za ku-upload picha, bado zinagoma.
Source: Mimi mwenyewe niko eneo la tukio.
===========
UPDATE - Oct 21, 2013

Kanisa la Baptist buguruni Dar es salaam limechomwa moto.. Akizungumza kanisanai hapo kwa uchungu mchungaji wa kanisa hilo Ezekiel Mkumbila amesema wamesikitishwa na sana kitendo kilichofanywa na watu wasioulikana.
Mchungaji Mkumbila amesema kanisa limechomwa ndani na kusababisha hasara kubwa sana..Amesema kanisa hilo lilchomwa jumamosi majira ya saa 8 usiku...Kamanda wa polis kanda maalum ya Ilala amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema ameagiza polisi kufanya upelelezi ili kubaini ni nani waliohusika na uchomwaji wa kanisa hilo...
(Wapo radio news)