technically yes.
walikuwa wanasimamia mafundisho ya musa na manabii, lakini walitakiwa wayaache kwani hayakuwa na wokovu na yalijaa kujionyesha mno. hivyo walitakiwa wafuate mafundisho na sheria ya kristo.
jua ya kuwa hawakuhesabia haki bila sheria. kosa linakuwepo pale sheria ya kristo ilipokufikia.
warumi 7:5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na Sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.
warumi 7:7 Je, tuseme basi, kwamba Sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila Sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama Sheria isingalikuwa imesema: "Usitamani.
:12 Basi, Sheria yenyewe ni takatifu, na amri yenyewe ni takatifu, ni ya haki na nzuri.
:13 Je, hii inamaanisha kwamba kile kilicho kizuri kimesababisha kifo changu? Hata kidogo! Iliyo ni kwamba, dhambi, ili ionekane dhahiri kuwa ni dhambi, imekitumia kile kilicho kizuri na kusababisha kifo changu. Hivyo dhambi, kwa njia ya ile amri, ilijionyesha kikamilifu jinsi ilivyo mbaya mno.
7:14 Tunajua kwamba Sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia, mimi nimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi.
:23 Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini mwangu.
:24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka katika mwili huu unaonipeleka kifoni?
:25 Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya dhambi.
chamsingi zaidi ni kuwa, imani haikuwa universal, yaani ilihusu taifa teule la wayahudi pekee.lakini baada ya yesu, imani imekuwa universal(inawajumuisha mzabibu mwitu pia)