Kanisa lamuandalia tuzo Lowassa

Kanisa lamuandalia tuzo Lowassa

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
KANISA la Overcomers lililopo mkoani Iringa, limeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kumtunuku Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kutokana na mchango wake alioutoa katika jamii.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Boaz Sollo, alisema jamii ya wakazi wa Mkoa wa Iringa inatambua mchango wa Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli.

Dk. Sollo alisema kuwa tuzo hiyo itampa moyo wa kuendelea kushiriki zaidi katika shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuiendeleza injili kama ambavyo amekuwa akifanya.

"Hii tuzo itamuongezea ujasiri wa kujituma katika kuisaidia jamii, sambamba na kuchangia ujenzi wa makanisa katika mikoa mbalimbali bila kujali wanaomkatisha tamaa ili kumrudisha nyuma.

"Tumeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kiongozi huyu ambaye haipiti wiki moja anasikika akifanya kazi za kijamii, habagui, hachagui na wala hana upendeleo," alisema Dk. Sollo.

Aliongeza kuwa tangu alipojiuzulu uwaziri mkuu, hajawahi kuutembelea mkoa huo jambo linalowafanya wakazi wa mkoa huo kuwa na hamu ya kumuona kutokana na jitihada zake za kujihusisha katika masuala ya kijamii.

Alisema tuzo hiyo itatolewa mwezi ujao wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo na kituo cha redio ya dini ya Overcomers, ambayo ni maarufu kwa mikoa ya kusini.

Wakizungumza na MTANZANIA kuhusu tuzo hiyo, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamelipongeza kanisa hilo kwa kuandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kutambua mchango wa kiongozi huyo.

CHANZO: Mtanzania
 
Badala ya kutumia

KANISA LAMUANDALIA TUZO LOWASSA

ungetumia

DHEHEBU LA OVERCOMES LAMUANDLIA TUZO LOWASSA

ili kuondoa utata kwamba tuzo hiyo ni ya kanisa kwa maana ya wakristo wote.

kuna tofauti gani kati ya kanisa na dhehebu???
 
R.B hiyo michango yake inatoka kwenye kampuni zipi ili tujue kwa hakika kampuni zinazoongoza kwa kile kinachoitwa "Corporate Social Responsibilities" au ni kutoka kwenye mshahara wake wa Waziri mkuu mstaafu? Nauliza maana tukimsikia Mengi tunafahamu hizo pesa zinatoka kwenye makampuni ya IPP
 
Last edited by a moderator:
Hii imenikumbusha neno moja la enzi zetu,

EL awa "kipusa" wa shughuli

Hamuondoki mikono mitupu
 
Lawassa kageuka dili sasa,,, Membe kalagabaho, endelea kutumia umafia wa kutoa watu macho na kucha wenzio wana calculated move ya kuwa nominated na CCM
 
Anajitolea kwenye mambo yapi ya kijamiii? Kujenga makanisa? Wakristo mumekuwa niwatu wa kukwamisha harakati kila siku. Aiwezekani kwa jitu kama hili (fisadi) kupewa tuzo ya heshima.
 
Dhehebu ni moja, mfano RC.
Kanisa kinaweza kuwa lolote, RC, Nagliacn, Full Gospel na mengine.

Ukisema kanisa linamwandilia zawadi EL ina maana hayo yote.

Hilo dhehebu ndio nimelisikia leo...
 
Kuna kanisa moja tu Katoliki la mitume.Ukiniuliza kwanini tembelea kanuni ya imani ambayo madhehebu yote yakikristu hukiri.Kwa maana nyingine hao wanaprotest agaist the church(Catholic) though kwenye kanunu zao za imani wanasadiki kwa kanisa Katoliko(Catholic)kwa maneno.
 
R.B mpe EL haya maneno
"Nani atakaye nimtuume afundishe vijana ni tayari Bwana wangu Nitume mimi Bwana"
 
Saaafi sana ngoja sasa tuweke mfumo kristo wa ukweli ili wapinga kristo wapate uhalali sasa wakulalamika
 
Pengo andaa tuzo kwa Wilbroad Slaa na Chadema kwa ujumla,malasusa andaa tuzo kama hizo kwa hao makamanda na matuzo mengimengi wapewe wanasiasa wakikristo ili tupumue maana kila akikaa wa dini fulani hivi malalamiko kuanzia kwa rais mpaka kumbi za kelele haziishi...Ni democrasia tu ila kidini zaidi maana mmetutuma hatukutaka na hatukuwahi kuupenda lakini kwa yanayotokea kwa kukalia kiti dini fulani tumejua ni hatari kwa taifa na ni jambo la kujilaumu sana kuchagua hawa jamaa
 
Na kweli na azidi kuchochea chuki dhidi ya viongozi wa dini na serikali maana na serikali yenyewe imelala usingizi fofofo.

Kweli hii nchi imetumbukia katika shimo la hatari, na soon tutasahai ile Tanzania tuliyokua tukijitia kisiwa cha amani. Tutakimbilia Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya kutafuta hifadhi, maana wao wameshaonja joto ya uvunjifu wa amani kutokana na uroho wa madaraka wa watu kama Lowassa ambaye kwake URAISI ni kwa gharama yoyote ile na saa hizi watu wameshapofuka macho na kusahau kila kitu hata wale waliokua humu JF wakimshambulia kwa maneno makali, ambayo sasa wanaona hata aibu kuyatamka maana wanaona watakumbushia f_s_di mkuu na watapoteza ulaji.

Kwa sasa nyumba za ibada peleka tu minoti hakuna atayehoji ulipataje. Sasa hivi nyaraka za viongozi wa dini za 2010 zilizokua zinazungumzia ufisadi hazipo tena na badala yake zinaibuka kauli na matamko kusema mambo ya jumla jumla na yanayotokana na mikakati mipya inayotengenezwa kutusahaulisha ufisadi waliokua wanauimba. Mwenye macho haambiwi tizama.

Tujiulize, ili kutusahaulisha ufisadi ulioendelea na unaoendelea kila baada ya mda kuna tukio litatokea tofauti na ufisadi na likianza kupoa litatokea lingine, huku tukiendelea kutoa matamko ya kujionyesha tunajali na kuendelea kuchangia makanisa na misikiti kwa mamilioni ambayo yangetosha kumaliza mradi wa maji wa Monduli ambao Kikwete alipokwenda alimsifia Lowassa kwamba ni kiongozi bora atashirikiana naye kupata fedha za kumalizia mradi wa maji uliokwama, ambao gharama zake hazifikii zinazotolewa makanisani.

Tunazugwa na JK na kina Membe hapa kwamba ni maadui wa Lowassa kumbe wanajiandaa kuendeleza mtandao.
 
Back
Top Bottom