Cardinal06
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 963
- 326
IN SUMMARY
Mchungaji wa kanisa hilo, Thomas Kipemba amesema licha ya kuporomoka kuta zake ambazo ziliwekewa nondo laini, litajengwa jingine kwa michango ya waumini zaidi ya 900 wanaoishi mji wa Muleba.
Ngara. Kanisa Kuu la Pentekoste katika Mamlaka ya Mji Muleba mkoani Kagera, ambalo lilikuwa limefikia hatua ya kuezekwa limeporomoka kutokana na madai ya kujengwa chini ya kiwango.

Amesema hadi linaporomoka zilikuwa zimetumika Sh200 milioni na hasara iliyopatika inakadiriwa kufikia Sh55 milioni.
Hata hivyo, mmoja wa waumini wa kanisa hilo, Adonis Mushaija amesema katika ujenzi huo waamini walichangia fedha taslimu, mazao na vitu mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi