Waumini wa Kanisa la KKKT watakiwa kuvaa barakoa wanapoingia Kanisani

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1588000389008.png


Waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kusini,wametakiwa kuhakikisha wanavaa barakoa wanapofika ibadani.

Wito huo umetolewa na askofu wa kanisa hilo dayosisi ya kusini Dkt. George Fihavango mara baada ya ibada ya Jumapili katika kanisa la hilo usharika wa Mji Mwema mjini Makambako,ambapo amesema kuwa waumini wote wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa ibadani ili waweze kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Aidha ametoa wito kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa dayosisi ya kusini kuhakikisha waumini wote wanavaa barakoa wanapokuwa ibadani.

Amesema licha ya tahadhari ambazo zimeendelea kuchukuliwa na waumini wa madhehebu mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) kwa kukaa umbali wa mita moja na nusu hadi mbili na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabun,lakini ni wajibu kila muumini kufuata taratibu mbali mbali za kujikinga na virusi hivyo.
 
Back
Top Bottom