By
mayenga
Swali kwako Dk Slaa,
Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?
Mayenga,
Jibu
Asante sana kwa maswali mazuri sana. Ningependa kujibu tu kwa ufupi kama ifuatavyo:
a) Kuwa nilipokuwa Padre na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) niliondolewa kwa Ufisadi na kutafuna michango ya Ziara ya Papa Yohane Paulo wa Pili. Ah, sijui nisemeje, anayetafuna michango na kufanya ufisadi hufikishwa kwanza mahakamani na akipatikana na hatia hufungwa gerezani kwa mujibu wa Sheria.
b) Kama hoja hii siyo ya Propaganda na kama mtoa hoja anaelewa Sheria za Kanisa Katoliki, au na wale wanaopigia debe hoja hii, basi ningelitegemea mambo kadhaa i) Wangeliweka hadharani "Hati"( Decree) ya kuondolewa kwa ufisadi. Kanisa Katoliki ina very elaborate procedure kwa mujibu wa Sheria zake, hivyo isingelimwondoa tu mtu aliyetafuna michango, na hata kumwondoa Upadre, ambao kama nilivyosema ni Sakramenti na haufutiki, isipokuwa kwa Taratibu elaborate za " Laiciztion", hati ambayo hutolewa na Papa peke yake kupitia Wizara ( Idara yake husika). Hati niliyonayo inayonirudishia hadhi ya Ulei (Laity) haitoe mahali popote process yoyote dhidi yangu, bali inajibu Maombi niliyowasilisha mwenyewe kwa mandishi yaliyosainiwa na mimi mwenyewe chini ya Kiapo, na kwa kuwa maombi yangu yalifikia viwango vinavyotakiwa nikapewa Decree husika.
c) Katika Kampeni ya 1995 ndiyo hoja kubwa iliyotumika na CCM na kwa bahati mbaya kila uchaguzi unapokuja hujaribu kufufua tena propaganda hiyo.
Hata hivyo, iwapo si propaganda, basi ningeliwategemea kwenye Jamvi hili wangeliweka angalau Indicators (viashiria) kuwa huyu bwana aliondolewa na Kanisa, aidha kwa document, au kwa kiashiria kuwa kuna chuki kati ya Dokta Slaa na Maaskofu au viongozi wa Kanisa Katoliki. Badala yake Dr. Slaa ameendelea ku enjoy uhusiano na Kanisa Katoliki katika ngazi zake zote, na hata siku wazee wa Karatu walipokuja kuniomba katika delegation kulikuwa na Mapadre wawili Fr. Reginald Barhe ( class mate wangu) na Fr. Dominick Rahhi aliyekuwa Parokia ya Karatu wakijua kuwa nikiwaona wenzangu, basi nitakubali kugombea. Nami kwa Historia yangu ndani ya CCM nikakubali na kuwaambia nitagombea kwa Tiket ya CCM kwa kuwa ndiyo chama nilichokijua hadi wakati huo. Hata ccm wenyewe katika hoja ya kuniengeua kuwa Mgombea kwa tiket ya CCM walieleza kuwa "nimesaidiwa na Kanisa Katoliki, japo hawakuweza kuonyesha uthibitisho wowote, wala sikuhojiwa kuhusu hoja hiyo) badala yake wakaamua kuniondoa kwa msingi wa "siyo mwenzetu".
Hivyo sina zaidi ya kusema hiyo ni propaganda isiyo na mshiko kwa kuwa Wananchi wa Karatu ndio walionifanyia Sherehe ya Upadre, ndio walioshiriki siku ya Upadre wangu, ndio walioniomba kugombea na kunifanya nishinde kura za maoni ndani ya CCM (kabla ya kuondolewa kwa mizengwe) na ndio walioendelea kunichagua katika chaguzi zote 3 toka 1995.
d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.
Nadhani kwa ujumla maelezo haya yametoa picha kamili ambayo imeendelea kurudiwa mara kwa mara na wana CCM katika jitihada zao mbalimbali, hasa wana CCM wanaotoka nje ya Karatu, kwa kuwa Karatu hadi leo majina yangu ni Willy, Dr. na Padre kwa maana ya ukaribu wa watu wa Karatu na Dr. Slaa.