Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Viongozi wa CCM wazidi kuaibika, baada ya Mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo Kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya Papa na kumtaka Wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

Kanisa Katoliki Lamshukia Wasira

LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA

Na Waandishi Wetu

KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.

Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: "Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari."

Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

"Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake," alisema Ruwaichi.

Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

"Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa," alisema.

Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... "Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele."

Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

"Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu," alisema Dk Slaa.

MY TAKE:
Ni aina gani ya viongozi wa CCM tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza Mkapa kudanganya sasa kafuata Wasira. Who is next??

Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.
 
duh kauli yako hii, let me reserve my comment
 
DSN na Wana JF,
Mkuu comments yako haiendani na Mada au hoja ya muhusika, ungesoma mada yote ndio u-comments, labda nimekuelewa vingine, kiujumla upo nje ya mada, labda ufafanue una maana gani.
Nawakilisha

Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.
 
Mnajua wasira anafikiria kwa ********* sasa kama aliiba fedha hizo inabidi kudhibitisha akishidwa kutoa udhibitisho nadhani azomewe kila apitapo kwasababu naona mavuvuzela wamezidi CCM
 
Point:
Wameshindwa kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii badala yake wanaeneza siasa za kishenzi!
Wamefilisika hoja!
 
Back
Top Bottom