Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

Wassira a.k.a Sokwe wa Mahale! Yaani hii njemba iombe sana isijekutana na Dr. Jane Goodall, haki ya nani atamrudisha Mount Mahale ama sivyo kitamuanzishia utafiti kujua ni jinsi gani ameweza kuishi na binadam mpaka wakamwamini na kumpeleka Bungeni.
 
Tujikumbushe msemo wa Eleanor Roosevelt:
"Great minds discuss ideas;
Average minds discuss events;
Small minds discuss people." -

Unamweka wapi Waziri wako Mheshimiwa Stephen Wasira?

Ungeweka category nyingine ya "Absent minded discuss rubbish" yaani majungu, uongo, matusi etc. nadhani ndiyo category anayofit huyu waziri.
 
Ni kweli siasa za kuchafuana hazina tija kwa jamii. Lakini napata wazo sasa kwamba kukashifiana kunakoshamiri leo hii ni muendelezo na ulipaji wa visasi kwa mwasisi wa SIASA ZA KASHFA hapa nchini WILBROUD SLAA pale alipoamua kuwakashfu watu tena kwa kuwataja majina kuwa ni mafisadi , wakati yeye akiguswa tu utasikia majibu "WENYE USHAHIDI na waende Mahakamni" , Majbu marahisi ambayo yanakuwa kama kejeli fulani huku Watanzania wakijua kabisa kwamba ni kodi zao ndizo anazichezea kama ambavyo amekuwa shujaa wa kuyakemea hayo Majukwaani.

@Mtotowamvuvi,
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuchafuana kwa propanda na kufichuwa maovu. Na ni dhahiri Wassira ama hafahamu tofauti yake au ameamua kuvuruga CCM huko Meru. Alichofanya Dr. Slaa pale Mwembeyanga ni kuueleza umma wa Tanzania wizi wa rasilimali za nchi huu unaofanywa na watu wachache. Na mbaya sana watu hao wamepewa DHAMANA na wananchi wa Tanzania kuzisimamia hizo rasilimali kwa manufaa ya wote. Lakini kwa roho ya ajabu na bila huruma wameamua ni wao na familia zao na marafiki ndio wanastahili kuzila!

Kwa upande mwingine Wassira na ccm wenzake wanafikiri mbinu ya kupambana na Dr Slaa ni kuamka asubuhi na kuzusha mambo. Dr Slaa alionesha documents za wizi, na hata bungeni kapeleka ushahidi.

Baada ya miaka 50 madarakaani, CCM wanatakiwa wawaeleze watanzania ni kwanini hatuna maji, kwanini barabara zetu ni mbovu, kwa nini zaidi ya theluthi moja ya watanzania (milioni 45) wanapata mlo mmoja tu kwa siku - tena kwa kubangaiza? Kwa nini wagonjwa wanalala chini?

Ni fedheha na madharau kwa watanzania walipa kodi kwa mtu kama Wassira na wakina Ole Sendeka kusimama mbele za watu na kutukana badala ya kutoa majibu kwa maswali ya msingi. Tanzania inapitwa kwa mambo mengi sana ya maana na nchi kama Rwanda, nchi ambayo imetoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwenye orodha ya maadui wakuu wa Tanzania CCM inatakiwa iwe number moja!.
 
Tujikumbushe msemo wa Eleanor Roosevelt:
"Great minds discuss ideas;
Average minds discuss events;
Small minds discuss people." -

Unamweka wapi Waziri wako Mheshimiwa Stephen Wasira?
Small minds... Ni zaidi ya kilaza..
 
Naunga mkono wazo hiil liwe fundisho; tena siyo Wassira tu na CCM yenyewe maana Wassira alikuwa anazungumza on behalf ya mgombea wa chama chake..
 
Kweli labda itasaidia kuwarudishia akili hawa viongozi wa CCM manake wamezidi kuropoka kila kukicha...

Mkapa hovyo, Wasira hovyo kabisa!
 
Naunga mkono wazo hiil liwe fundisho; tena siyo Wassira tu na CCM yenyewe maana Wassira alikuwa anazungumza on behalf ya mgombea wa chama chake..
Mkuu inaweza kuwa sawa na ikawa fundisho. Lakini kampeni za Arumeru zinaonyesha kwamba tunako enda si salama mno; watu wanakashifiana badala ya kuwapa wananchi sera zao na kuwaambia watawafanyia nini wananchi wa Arumeru pindi wakichaguliwa. Nadhani ni vyema hivi vyama vikakutanishwa na kuambiwa viache kushambulia personalities. Tukisema washitakiane basi tutashuhudia mashtaka yafuatayo:
  1. Vincent Kiboko Nyerere atamshitaki Benjamini William Mkapa kwa Ben kusema kwamba Vincent si mtoto wa Nyerere
  2. Benjamin William Mkapa/Serikali itamshitaki Vincent Nyerere kwa kumtuhumu Mkapa/Serikali kuwa walimuua Baba wa Taifa
  3. Vincent Kiboko Nyerere atamshtaki Olesendeka kwa kumtaka aondoke kwenye eneo moja la Jamhuri yaani Arumeru na kuwaachia Wameru na Wasai. Kikatiba unaruhusiwa kwenda kokote ndani ya Jamhuri bila kibali achilia mbali kugombea Ubunge kokote sembuse kupiga kampeni eneo ambalo hujazaliwa!
  4. Dr. Willbroard Slaa atamshitaki Wassira kwa kumkashfu kwamba aliiba pesa za kanisa ndio maana akafutwa upadre
  5. nk kwa kuwa huu siyo mwisho wa kashfa!
 
Hata mimi naunga mkono, taifa letu linaelekea kuwa taifa la waongo.Wasira apelekwe mahakani
 
Hata kama Dr asingetaka, hivi mtu mwingine harusiwi kumshtaki Wassira kwa kashfa alizotoa? Wanasheria tusaidieni katika hili.
 
Haya ndio madhara ya siasa uchwara,stephene wassira ndio waziri wa mahusiano lakini angalia anachokifanya?je anaboresha uhusiano?au anaharibu uhusiano?kichefuchefu huyu naye katumwa kuongeza nguvu arumeru kwa ccm,hivi hakuna watu huko ccm?na hili wenye akili zetu timamu tulishalitarajia litatokea watu wanapotaka kutumia siasa chafu kwa kutumia kanisa kufanikisha malengo yao ya kisiasa,eti wassira nae ni waziri wa uhusiano kweli siasa tanzania imebakwa kinyume na maumbile.
 
Wakatoliki wanaficha mapadti walawiti watoto wa kweli kweli ndio wawe wezi wa pesa.

Ni rahisi kunwamini manumba kuliko hawa maaskofu.

mwulizeni huyo askofu kanisa lake lina mapadre wangapi wanao lawiti na kunajisi watoto atasema hakuna waongo wakubwa.
 
Ok nimeona nikujibu japo kwa great thinker ingekuwa aibu mimi kumjibu kwa kuwa tayari maana yangu iko wazi.Haya mada yako wewe inaangalia muhusika alipoaanguka yani Kanisa kutupiwa madongo na wanasiasa ambayo si ya kweli.Lakini kanisa alikutazama limejikwaa wapi na wanasiasa mpaka likafikiwa kutungiwa uongo dhidi yake na muumini wake aliyepata kuwa Padri kama wito wake na wito huo ulipokwisha kwa sababu zake binafsi ambazo si wengine hatuna sababu ya kuzijua kwa kuwa wito ni mambo binafsi na ni kati ya kanisa na muumini wake binafsi.Sie raia wengine tena watu wazima kuingilia mambo binafsi ya kanisa na muuumini wake ambae kwa hadhi alifika kuwa padri ni sawa na kuingilia ndoa ya mtu na mkewe.Ndoa ikishafungwa wenye uwezo wa kuingilia migongano ya ndoa ni viongozi wa dini na hata wao pia si waamuzi wa mwisho muamuzi kwa ndoa za kikristo ni Mungu.

Hivyo kwa kanisa kutokuangalia aina ya viongozi wa kisiasa na serikali wanaofika kwenye shughuri zake na kuwajibika kama daraja na wananchi,imekuwa ni ugonjwa uliofikisha Kanisa kufika sehemu kutoheshimika kama nyumba muhimu ya kiimani na kuwa wanaotakiwa kukaribia kanisa lazima wawe ni wanasiasa wenye heshimika kwenye jamiii. Matokeo ya kubeba wanasiasa wasio na maadili ndio chanzo cha wao kuona kanisa kama nyumba ya kishikaji na sio nyumba ya Mungu.

Kanisa limekuwa likiwazoeza kuhalika viongozi kwenye shughuri zake kiasi kuwa imekuwa ni sehemu yao ya kuja kutolea madongo kwa wengine,yani membali za kanisa zimekuwa ndio sehemu ya kufikishia madongo kwa wanasiasa wenzao,hivyo basi nao wanasiasa wengine wameona kanisa kama ni washikaji na kumbe kanisa ni Nyumba ya imani muhimu sana ya maisha ya wanadamu.Tizama wamemualika EL Ifakara kafika uko kalusha kijembe kwa Serikali ya Kikwete,pata picha wasaidizi wa Serikali ya kikwete wako njiani kutoa tamko la Lowasa la Kanisa la Roaman Cathoric Ifakara Morogoro,sio tamko la Lowasa jimboni kwake Monduli sharehe za shule za kata Kata alizoshadadia zijengwe enzi yake.Hivi unapata picha gani inayokwenda kwenye baadhi ya viongozi wakuu na wasaidizi wao dhidi ya Lowasa na Kanisa Katoliki Tanzania

Viongozi wenyewe ndio kama hawa wenye matamko haya nimemnukuu Pakajimmy

Hivyo ukitizama unaona kuwa kwa picha hii,kanisa linapaswa kuita watu waadilifu,kama hawapo liaache kabisa kuita watu wa kada ya kisiasa na utawala.Hivi pata picha umualike mtu kama Joseph sinde ni heshima gani utakuwa umetoa kwa kanisa au Mtu kama Salim Mohamed Salim,kiasi kuwa wanasiasa wasio waadilifu watasikia tu membali za kanisa na hivyo kanisa kuonekana ni sehemu ya heshima na hata wageni wake ni watu waheshima kwenye jamii ambao hawana madoa ya kutiliwa shaka.Wakikosekana wale ambao ni waadilifu Serikalini na wastaafu basi wako hata wataalamu kama Pro Shivji au Pro Baregu.

"Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kupona" LK 5"32, Mt. 9:13, Mark 2:17.Hayo ni maneno ya Bwana Yesu. Hainingii akilini jinsi unavyoweza kuwabainisha kuwa hawa ndio wenye wema na uwape mwaliko halafu wengiene useme ni mafisadi ili uwanyime mwaliko. Na Kanisa la kweli la Yesu Kristu alie hai likifanya hivyo basi yumkini litakuwa limekosa hadhi ya kuitwa Kanisa. Mafisadi na wote wenye dhambi wanatakiwa kupewa nafasi sawa na watu wengine ili watubu. Kuwabagua na kushindwa kuwapa nafasi ni kupoteza nafasi ya kuokoa roho zao. Na kama mtu ambaye anatuhumiwa kuwa fisadi anakuja na kutumia nafasi hiyo kuwapiga wengine vijembe hayo ni matukio na fundamental purpose ya kuwaita inakuwa haina maana kuwa watumie nafasi hiyo vibaya. Na protocal hairuhusu wakati mtu anaongea ukakurupuka kumwambia badilisha kauli.Haiko hivyo maana unaweza kuanza kuleta malumbano yasikuwa na tija. Na mtu akiongea kitu ambacho ni hasi kwa mwingine basi kama hakina maana watu wataamua.

Halafu tufike mahala Watanzania tuwe na critical and critic analysis and assessment. Hivi madudu yote yanayolifanya Taifa liwe ombaomba katikati ya utajiri wa asili yamesababishwa na Lowasa? Hivi utajiri wa madini tuliokuwa nayo na mikataba mibovu imesainiwa na Lowasa? Barrick Gold Mines ndio wenye migodi mikubwa Tanzania.Je, ni Lowasa huyu? Mikataba hii ilisainiwa kati 1983, 1984 and 1985. Hivi ni Lowasa? Waziri wa Nishati na Madini alikuwa ni Lowasa au Kikitwe? Mikataba hiyo ni ya haki? Mrahaba wa 3% ulianza lini? Nani aliuza mbuga za wanyama kwa waharabu? Ni Lowasa? Nani alisaini mkataba wa IPTL na Rada 1985? Ni Lowasa au ni Mwinyi kama Rais na Kikwete kama Waziri wa Fedha? Kuna mkono wa Lowasa kiasi cha kuitwa fisadi? Je, Richmond inayafanya haya yote kuwa bure na Lowasa kuonekana ndiye mabay asiyestahili kusogelea malango ya makanisa?

Nafikiri tuache kujastify kitu kiovu na kibaya kwa kuleta visingizio. Wassira aambiwe plain point kuwa umelikosea adabu kanisa katholiki na kumkosea heshima Dr.Slaa kwanza kama mtu na kiongozi wa chama. Na ameikosea heshima serikali na chama chake kwa kauli mbovu. Approach aliyoitumia ndio hiyohiyo aitumie kuomba radhi kwa watu na taasisi alizozikosea. Kama hatafanya hivyo tumdharau na kumwombea ili sumu yake asiwaambukize wanae na watu wengine
 
Kesi ya nini,
si unajua kwenye msafara wa wasomi na vilaza kama wasira wapo kujaza nafasi.
 
Sikutegemea kama ccm ya Mwalimu inaweza kugeuka na kuwa li-chama la wajinga kiasi hiki! Kama tunatawaliwa na chama cha wajinga Kama Wasira, basi Mungu atuhurumie.

Wajinga wanapita kwa kishindo kwenye chaguzi nyingi kwa sababu wana mtaji wa wajinga wenzao. Hujiulizi leo mwanafunzi anafika darasa la saba lakini hajui kusoima na kuandika wewe unategemea hayo madarasa yote ya chini amepitaje kama hakuandaliwa kuwa mjinga ili aje awape kura wajinga wenzake?
 
"Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kupona" LK 5"32, Mt. 9:13, Mark 2:17.Hayo ni maneno ya Bwana Yesu. Hainingii akilini jinsi unavyoweza kuwabainisha kuwa hawa ndio wenye wema na uwape mwaliko halafu wengiene useme ni mafisadi ili uwanyime mwaliko. Na Kanisa la kweli la Yesu Kristu alie hai likifanya hivyo basi yumkini litakuwa limekosa hadhi ya kuitwa Kanisa. Mafisadi na wote wenye dhambi wanatakiwa kupewa nafasi sawa na watu wengine ili watubu. Kuwabagua na kushindwa kuwapa nafasi ni kupoteza nafasi ya kuokoa roho zao. Na kama mtu ambaye anatuhumiwa kuwa fisadi anakuja na kutumia nafasi hiyo kuwapiga wengine vijembe hayo ni matukio na fundamental purpose ya kuwaita inakuwa haina maana kuwa watumie nafasi hiyo vibaya. Na protocal hairuhusu wakati mtu anaongea ukakurupuka kumwambia badilisha kauli.Haiko hivyo maana unaweza kuanza kuleta malumbano yasikuwa na tija. Na mtu akiongea kitu ambacho ni hasi kwa mwingine basi kama hakina maana watu wataamua.

Halafu tufike mahala Watanzania tuwe na critical and critic analysis and assessment. Hivi madudu yote yanayolifanya Taifa liwe ombaomba katikati ya utajiri wa asili yamesababishwa na Lowasa? Hivi utajiri wa madini tuliokuwa nayo na mikataba mibovu imesainiwa na Lowasa? Barrick Gold Mines ndio wenye migodi mikubwa Tanzania.Je, ni Lowasa huyu? Mikataba hii ilisainiwa kati 1983, 1984 and 1985. Hivi ni Lowasa? Waziri wa Nishati na Madini alikuwa ni Lowasa au Kikitwe? Mikataba hiyo ni ya haki? Mrahaba wa 3% ulianza lini? Nani aliuza mbuga za wanyama kwa waharabu? Ni Lowasa? Nani alisaini mkataba wa IPTL na Rada 1985? Ni Lowasa au ni Mwinyi kama Rais na Kikwete kama Waziri wa Fedha? Kuna mkono wa Lowasa kiasi cha kuitwa fisadi? Je, Richmond inayafanya haya yote kuwa bure na Lowasa kuonekana ndiye mabay asiyestahili kusogelea malango ya makanisa?

Nafikiri tuache kujastify kitu kiovu na kibaya kwa kuleta visingizio. Wassira aambiwe plain point kuwa umelikosea adabu kanisa katholiki na kumkosea heshima Dr.Slaa kwanza kama mtu na kiongozi wa chama. Na ameikosea heshima serikali na chama chake kwa kauli mbovu. Approach aliyoitumia ndio hiyohiyo aitumie kuomba radhi kwa watu na taasisi alizozikosea. Kama hatafanya hivyo tumdharau na kumwombea ili sumu yake asiwaambukize wanae na watu wengine

YESU KRISTO alikuja kwa ajili ya wenye dhambi. Mathayo 11:28 - Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha. Yohana 4:10 - 12 - Mwivi haji ila achinje na kuharibu bali mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele.
My take: Lowasa anaendaga kanisani kutubu au anampango wa kulinunua kanisa? Katika mambo anayoyafanya kwa kanisa ni ili liendelee au ni ili ajipatie utukufu? Mipango yake mwenyewe alifofanya mathalan Richmond vinaendana na kutubu au na kuliharibu kanisa? Ni watu gani waliotaka kumuengua Askofu Malasusa asiwe askofu mkuu wa Lutherlan? Lowassa hakuhusika? Hivi mwenye dhambi ananyenyekea kwa kanisa au kanisa ndilo linamnyenyekea mwenye dhambi?
HAPANA LOWASSA ANANIA MBAYA NA KANISA! kama wenzake walifanya makosa haimpi na yeye nafasi ya kufanya makosa!

Kwa heshima na taadhima namwomba Dr wa Ukweli awaelekeze wanasheria wake wafungue kesi ya kashfa dhidi ya Wassira ambaye kila siku anazungumza maneno ya hovyo. Kanisa limeshakanusha hivyo taarifa na madai yake ni ya uongo hivyo atakiwe aombe radhi kupitia vyombo vya habari la sivyo apelekwe court au angalao baraza la habari ili lizee hili liumbuke. Mod plz naomba uiache thread yangu ili Dr aupate ushauri wangu
....umefika wakat watanzania tuwajibike na taarifa tunazowapa wananchi
 
Back
Top Bottom