Kaniroga kwa kutumia penzi lake

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,213
56,849
Sio kwa kutumia mizimu, bali kaniroga kwa utamu utamuni. Sauti yake tamu hulindima mithiri ya bubujiko la chozi lenye kuleta furaha!.

Jina lake zuri nimeliandika katika kikiminika cha damu yangu! ngozi yake haina ajenda ya ulaghai bali hunigusa na kunikaribisha kwa kuniambia "karibu mume wangu nikupe tamu yangu". Macho yake mazuri huongea vile anavyonipenda!,hayajawahi kunidanganya maana hayafanani na uongo!.

Huwa nafurahi akiniambia anakiu!,kwani napenda nimpatiapo maji koo lake huyagugumia maji kiulaini huku akipumua kwa hisani ya jina langu kenzy. Naam hakika kaniroga. Nampenda mpaka najionea wivu! nimemuahidi kumuonyesha maana nzima ya Mapenzi, na si kumuonyesha ushenzi ambao mwisho wake huaribu utenzi.

Kirogo chako binti wewe kimenilevya,mbele zako nishakuwa Teja. Napenda unavyonitishia ati utakuja kunimeza. Nami nakuambia nitajilegeza tayari kwa kumezwa. Utani wako wakupendeza, hakika siwezi kuubeza.

Nitalitaja jina lako sio tu kama mke bali mwenye nafasi ya undani wangu,mwenye kuijua hali ya mwili wangu na hata pumzi ya uhai wangu.

Ni wewe tu malaika wangu usiechoka kuniambia "NAKUPENDA" na ni Mimi tu nisiechoka kukuambia "NAKUPENDA PIA MKE WANGU"😊

NAKUPENDA SANA KOMAMANGA WANGU.
 
Kuna mahojiano niliona Ebitoke akimzungumzia Mlela nilicheka sana. Ebitoke anasema Mlela hakuwa mwanaume wake wa kwanza lakini alimpa kitu ambacho hakuwahi kupewa tangu abikiriwe na hajapata kitu kitamu kama kile tangu alipomuacha na hatokaa akasahau utamu wa ile kitu alipewa na Mlela

Penzi limemroga mtu
 
Na unaweza ukashangaa mi nikamuonja mlela na nisikie chochote haya mambo ni ntu na ntu
 
Kuna mahojiano niliona Ebitoke akimzungumzia Mlela nilicheka sana. Ebitoke anasema Mlela hakuwa mwanaume wake wa kwanza lakini alimpa kitu ambacho hakuwahi kupewa tangu abikiriwe na hajapata kitu kitamu kama kile tangu alipomuacha na hatokaa akasahau utamu wa ile kitu alipewa na Mlela

Penzi limemroga mtu
Kila mtu na chake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom