Kanipa Deadline either nikajitambulishe kwao au tuachane.

Kanipa Deadline either nikajitambulishe kwao au tuachane.

Top Thinker

Senior Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
183
Reaction score
125
Nimekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wa roho yangu kwa takriban miaka mitatu.
Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukiishi mikoa tofauti. Yeye anafanya kazi Babati na mimi nafanya kazi Dodoma.
Licha ya umbali uliopo tumeishi kwa upendo na kuaminiana na hata ndugu na wazazi wanajua kuhusu uhusiano wetu tukitarajia kuja kufunga ndoa baadae.
Siku za karibuni amekuwa akisisitiza sana nikatoe mahali kwao nami nikawa namuambia sawa tutafanya hivyo na nimemueleza sababu ya kuchelewa ni matatizo ya kifamilia yanayonikabili.
Ghafla wiki iliyopita alikata mawasiliano na hataki pokea simu yangu wala kujibu sms.
jana nimekaa nawaza akanitumia sms kuwa nadhani nishaamua kama namhitaji niende kwao Marangu kabla ya tar 25 mwezi huu vinginevyo simuhitaji.
Kweli nimeishiwa nguvu kwa kuwa sidhani kama kwenda kwao kwa kuforce kwa deadline ni vyema. Anajua kuwa nampenda sana lakini sasa hakuna my love wala sweet.. Ni mwendo wa hey na hello yan full ubabe. Nishaurini wakuu maana natarajia kwenda lakini kwa sasa sijajipanga kusema kweli.
 
ukiona hivyo pengine na yeye anaulizwa,muda wowote huo hakuna mabadiliko?au kuna mtu anamfukuzia kwa kasi na ahadi teletele,yeye hajajua aamue vipi.fanya kweli bwana na yeye ajijue yupo position gani,ukiangalia mapenzi ya mbali.matatizo kila siku yapo.sio umgegede tu miaka nenda miaka rudi
 
Huyo kapata mtu mwingine thats why anakuzengua maana naamini mlishaongea na kukubaliana taratibu zote za kuishi pamoja sasa iweje akuamlishe kama mjeshi?
Kama vipi mpige chini kwani si umeshagegeda vya kutosha? Hasara kwake, hasara kwake? Piga chini huyo tena mwambie huendi hata kwa ndumba za babu wa loliondo.
 
Yupo aliyeonesha nia ya kwenda kujitaambulisha kwao mapema iwezekanavyo.

Na upepo ulivyo mwezi hauishi utamkosa kabisa kama usipochukua hatua za kunusuru uchumba huo!

Naushauri ujaribu umwelewesha sababu yenye mantiki wa nn hutaki kwenda ujitambulisha sasa, maana inawezekana na wewe bado una mambo ya kivulana yanakufanya ushindwe uchukua maamuzi thabiti!
 
ukiona hivyo pengine na yeye anaulizwa,muda wowote huo hakuna mabadiliko?au kuna mtu anamfukuzia kwa kasi na ahadi teletele,yeye hajajua aamue vipi.fanya kweli bwana na yeye ajijue yupo position gani,ukiangalia mapenzi ya mbali.matatizo kila siku yapo.sio umgegede tu miaka nenda miaka rudi
hadi yesu arudi labda wanasubiri parapanda
 
khaa miaka mitatu? wanachunguzana nini? hata kama ni ghorofa inaisha
mbona hunipi tena yule mnyamwezi jamani?

Yaani pamoja technolojia ya sasa, miaka mitatu unamchunguza mtu ambaye ukiingia FB unaweza jua hata akiwazalo.
Wee nawe hata hueleweki, mara ushapata mara bado watafuta. Sasa take ur pick from a dozen nyamwezis. kuna The Boss, Sikonge Fighter, mzabzab KIKUNGU, Boflo, ITEGAMATWI, monaco, @hkigwangala, Shardcole na waburushi fulani hivi wana indício na The Boss.
 
Last edited by a moderator:
Wew nenda kajitambulishe tu..Watakuelew tu hal yko..Three years ni ming sana ukizingatia dunia yenyew haielewek..B careful watakuibia wenzio..

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hiyo miaka yote kwa nini hukumvalisha mimba kwanza? Hapo nadhani kuna jamaa aliekuwa Fasta anataka kudaka hiko kidosho ndio maana umepewa deadline.
 
Muda si mrefu utampoteza huyo bi mdogo...
Sharti lililopo mbele yako limewekwa kwa kuwa kuna mwanaume aliye tayari kwa ajili ya kuoa...
Kama bado unamuhitaji, nenda kwao na ukaji commit kwa wazazi wake na huyo bi mkubwa akiwepo...
Pengine walau utautuliza huo moto wa kifuu na kupunguza cheche zake...
 
Wazazi nao wana changia kumstress inawezekana ndio mana anataka ukamalizane nao,chukua atua mapema la sivyo itakua kwako,chunguza vizuri kuna kipindi kinaendelea labda kuna mtu tayari kampta na yupo ready kutoa mahali...
 
True siku hizi ndoa imekuwa biashara,mm demu wng wazazi wake wali muozesha kwa jamaa asije mjua kisa sikuwa tayari kuoa,ila mungu mkubwa na ndoa yenyewe baada ya wiki ikavunjika
 
naunga mkono hoja!eti unampenda na still hauko tayari,inaingia akilini kweli? maisha hayana fomula,hayo matatizo ya kifamilia hata ukichelewa kuoa yapo 2 huwa hayaishi! she s ryt, km hutaki mwache mwenzio sio kumpotezea muda.
 
Muda si mrefu utampoteza huyo bi mdogo...
Sharti lililopo mbele yako limewekwa kwa kuwa kuna mwanaume aliye tayari kwa ajili ya kuoa...
Kama bado unamuhitaji, nenda kwao na ukaji commit kwa wazazi wake na huyo bi mkubwa akiwepo...
Pengine walau utautuliza huo moto wa kifuu na kupunguza cheche zake...

Yes,watu 8, u a very ryt!n this is it
 
Back
Top Bottom