Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,512
Habari wakuu,
Husika na kichwa hapo juu,
Kanga ni vazi lililotumiwa na wanawake wengi kipindi cha miaka ya nyuma. Vazi la kanga lilikuwa likitumiwa na wanawake wakiwa wanaenda mahali kama sokoni. Kukiwa na sherehe ya mbalimbali za wanawake, vazi la kanga lilitumika kama zawadi kwa mwenye sherehe.
Vazi hilo pia lilitumika zaidi kwenye misiba ambapo wanawake hukifunga kanga kiunoni na nyingine hujitanda au kujifunika. Kipindi hicho ukiangalia kabati la mwanamke utakuts kanga zimepangwa vizuri. vazi hilo la kanga lilitumika kuwatega wanaume kimapenzi.
Miaka ya hivi karibuni kanga imepoteza thamani kutokana na kuingia kwa kijora.Kijora/dera ni mavazi yanayopendwa sana na watu wa uswahilini. Hata wanawake wa kiislam wamekuwa wakipendelea mavazi hayo. Kijora/dera hupendwa kuvaliwa sana kwa sasa kwakuwa ni vazi la kujisitiri.
Pia ni vazi la heshima kwa wanawake na kwa sasa vazi hilo linavaliwa na wanawake wengi. Ukienda sherehe nyingi za uswahilini utakuta wamevaa sare zao za vijora/ dera. Hata katika misiba pia mavazi hayo huvaliwa kwa wingi na wanawake.
Kiufupi vazi la kanga linapotea na kijora/dera kimechukua nafasi
Picha kutoka maktaba