Safi sana na imetulia.
Kelele za mpita njia,
Hazimtoi pangoni mwenyewe,
Wapi kanga moko huchezwa?
kama zi kwenye majumba ya starehe!
Huchezwa hadharani?
Au mbele ya watoto mashuleni,
Huchezwa stendi ya basi Ubungo?
Palipo wote na watoto pia?
Huko Kilabuni wacha ichezwe,
Acheni wanengue mpaka wakatike,
mikono mfukoni iwekwe,
mijengo isimame imara,
atazamaye kaipenda mwenyewe,
Kiingilio si bure ni ngawira,
Kanga moko wenyewe twaipenda,
Kama huipendi waifwatiani?
Mbunge alalama sauti juu apaza,
eti ipigwe mafuruku nchini kote,
mbona ujinga na ununda bungeni,
mwashindwa piga marufuku???
Matusi ruksa bungeni,
Mwatukana mpendwavyo,
Mangapi ya kuudhi bungeni twayasikia,
Lakini pingu mwaitia Kanga Moko?
Mwaendeleza ujinga wenu bungeni,
michango mwashindwa toa kwa kiswahili,
Ujumbe haufiki mpaka neno libane matusi,
mmekomaa mashavu ndimi za chuma,
Midomo yenu yanena ukengeufu,
Vichwa vyenu vimejaa mvi
Vichwani akili fupi kaa za makinda,
Bunge gani la misonyo na utusitusi JUU.
Msiiguse wala msiiseme vibaya kanga moko,
kanga moko siye yatuburudisha,
jadilini hoja maridhawa bungeni,
kanga moko ni upepo wapita,
Msiitaje kanga moko Bungeni,
Suala la Kanga Moko liko Mahakamani.
Msikomae na ulimbukeni komaeni na;
Uhaba wa maji safi,
Uovyo wa maji taka,
Wizi na ubadhirifu serikalini,
Ufisadi rushwa na ufuska,
foleni za magari ubungo,
Ndege mbovu TBS nyanya,
Mauti Kuzama kwa meli,
Mabilioni Iba ficha Uswiss,
CCM sheria chini wao JUU,
Watiwa mfukuko na mabilionea,
Rais kiguu na njia,
Muhimbili ife sie na APOLO,
Ritz! Milionea,
Kapata wapi kinda yule pochi????
Haya basi mgawie kidogo Willie!!!