Kanda ya Nyasa: Maandalizi ya Oparesheni 255 yakamilika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,343
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba Kamati ya Utendaji ya CHADEMA kwenye ile kanda kabambe ya Nyasa imemaliza vikao vyake kwa ajili ya Maandalizi ya Oparesheni 255.

Oparesheni hiyo Kabambe ina lengo la kuwaamsha Wananchi juu ya Umuhimu wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuwafundisha Uzalendo wa kulinda Rasilimali zao zikiwemo Bandari za Tanganyika.

Screenshot_2023-10-11-09-53-01-1.png
Screenshot_2023-10-11-09-53-05-1.png
Screenshot_2023-10-11-09-52-50-1.png
Screenshot_2023-10-11-09-52-57-1.png


Angalizo: Kama wewe ni Mzalendo na una uchungu na Mali za Nchi hii, na labda una roho nyepesi, basi tafadhali sana usihudhurie kabisa Mikutano ya Oparesheni hii, maana madudu yaliyofanyika Nchi hii yanayoenda kufumuliwa hadharani ni mazito mno, yanaweza kabisa kukuletea kiharusi ama pengine kukusababishia Umauti.

Usije kusema hatukukujulisha.
 
Lissu ataonekana Kanda ya Nyasa , ambapo anatarajiwa kutua na Ndege binafsi Songwe , Usiondoke JF
Hiyo itakuwa vyema sana.

Honestly, hizi operesheni za CHADEMA bila watu fulani hususani Tundu Lissu kuwepo, utamu, hamasa na msisimko hupungua.

Jamaa huyu ni jembe na mikutano yake huwa kama ile ya Yesu Kristo wakati wa maisha yake hapa duniani..

Yesu Kristo alikuwa anafuatwa na umati wa watu kila aendako bila hata kuwaita au kuwatangazia kuwa atakuwa na mkutano mahali fulani

Ndivyo alivyo Tundu Lissu. Huyu ndiye kiongozi wa taifa hili ajaye
 
Hiyo itakuwa vyema sana.

Honestly, hizi operesheni za CHADEMA bila watu fulani hususani Tundu Lissu kuwepo, utamu, hamasa na msisimko hupungua.

Jamaa huyu ni jembe na mikutano Huwa kama ile ya Yesu Kristo wakati wa maisha yake hapa Duniani..

Yesu Kristo alikuwa anafuatwa na watu Kila aendako bila hata kuwaita au kuwatangazia kuwa kutakuwa na mkutano.

Ndivyo alivyo Tundu Lissu
Umeweka mfano hai mno !
FB_IMG_1684753314240.jpg
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba Kamati ya Utendaji ya CHADEMA kwenye ile kanda kabambe ya Nyasa imemaliza vikao vyake kwa ajili ya Maandalizi ya Oparesheni 255 .

Oparesheni hiyo Kabambe ina lengo la kuwaamsha Wananchi juu ya Umuhimu wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuwafundisha Uzalendo wa kulinda Rasilimali zao zikiwemo Bandari za Tanganyika

View attachment 2778495View attachment 2778497View attachment 2778498View attachment 2778499

Angalizo : Kama wewe ni Mzalendo na una uchungu na Mali za Nchi hii ,na labda una roho nyepesi , basi Tafadhali sana Usihudhurie kabisa Mikutano ya Oparesheni hii , Maana Madudu yaliyofanyika Nchi hii yanayoenda kufumuliwa hadharani ni mazito mno , yanaweza kabisa kukuletea kiharusi ama pengine kukusababishia Umauti .

Usije kusema hatukukujulisha .
"...zikiwemo bandari za Tanganyika...".



Mmeshafeli....

Huo ni UHAINI.... Tanganyika dola haipo

Huo ni UBAGUZI NA UKANDA....hamkuidai Tanganyika kipindi cha awamu ya Rais Kikwete na Rais Magufuli......

#SiempreJMT
 
Sauti ya Watanzania nao waalikwe ili kwa pamoja tulishambulie Jukwaa.
 
Back
Top Bottom