Kanda maalum ya ushirikina

Kanda maalum ya ushirikina

View attachment 397114usafiri wa namna huu ni wa kiwango cha chini sana kuweza kuukuta kwenye kanda maalum..maendeleo kwenye ulimwengu wa kawaida huenda sambamba na maendeleo kwenye ulimwengu wa kiroho..hivi hapa Dar na maeneo ya jirani unaweza kweli kumkuta mtu anafuga fisi?
Me nataka kujua kwa nin wamchague fisi kama usafiri na sio swala
View attachment 397023kila kinachotokea kwenye ulimwengu wa macho ya kawaida ni replica ya ulimwengu wa roho! (Ushirikina ni mkusanyiko wa juju uchawi ulozi chumaulete kuwanga nk)
Tunapozungumzia kanda maalum ya kitu maana yake ni kwamba eneo hilo lina uhitaji wa ziada wa huduma fulani
..mfano Dar kwa sasa ni kanda maalum ya kipolisi kutokana na matukio ya ujambazi kushamiri! Kariakoo kwa sasa ni kanda maalum ya kodi za mamlaka ya mapato Tanzania kutokana na uhitaji wake!
Eneo lote la pwani ya Dar nenda mpaka bagamoyo msata wami pangani mbwewe mkata mpaka tanga mjini ni kanda maalum ya ushirikina
Hapa ndio kuna vilinge vingi vya ushirikina kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania, hapa ndio kuna wachawi waganga na walozi(kwa ujumla wao washirikina wa kila aina)
Hapa ndo kuna kila aina ya matibabu kuanzia miti shamba tunguli kisomo mpaka uganga/uchawi wa kitabu
Unaweza kwenda mikoani na sehemu tofauti kama gambosh nk lakini ukashindwa kwa hakika kukutana na ushirikina halisi....huu ukanda hukosi
View attachment 397030
Kwanini ukanda huu lakini?
Mazingira na jiografia yanaruhusu, malighafi za baharini na nchi kavu vinapatikana kwa wepesi urahisi na kwa wingi! Taka viungo vya binadamu hupati shida! Taka makombe na mazao bahari mengine ni rahisi mno! Taka variaties ya mizizi miti magome na hata matunda na majani huku sio tatizo kabisa
Lakini kwanini isiwe ndani ya Dar na ni nje ya Dar na maeneo ya karibu au mbali kidogo?
Ushirikina ni mambo ya kiroho zaidi yasiyo na ithibati za kisayansi! Yanahitaji ukimya utulivu upweke usiri uchache wa watu na kitu chochote kilichoendelezwa na binadamu kwenye ulimwengu wa teknolojia..teknolojia na usasa ni sumu kubwa kwenye ushirikina
Unaposhuhudia misafara isiyokoma kwa waheshimiwa sana Unaposhuhudia ajali za kila siku! Unaposhuhudia upotevu wa watu wazima na watoto! Unaposhuhudia mambo ya ajabu ajabu usishangae sana bali jua kwamba uko karibu kabisa na ukanda maalum wa kishirikina View attachment 397053
 
Wageni wa Gwaji man
35ff3fa55e270b1588b84e32e2e3bf9d.jpg
 
Maswali

Je kila mtu anaweza kologeka ?

Je ni mtu wa aina gani analogeka kwa urahisi ?

Je ni mtu wa aina gani halogeki kabisa ?

Lengo ni kujua, kutokana na elimu ya uchawi na ushirikina ni mtu wa aina gani hawezi kuathiriwa na aina zote za ulozi.
Usijibu kwa watu Wachamungu, hao inaeleweka, ukimwamini Yesu Kristo hakuna uchawi wala ulozi wa kukuathiri.
Nataka elimu nyingine inayo zuia ushirikina kufanya kazi kwa mtu.
 
Uchawi ni replica ya maisha haya ya kawaida
Kuna watu kinga ni ndogo hivyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa mbalimbali na kuna watu ni resistant kwa magonjwa
Kwenye uchawi ni hivyo hivyo ila mtazamo pia mtazamo unahusika ....ukiamini katika kulogwa utalogwa kweli
Ukishaanza kushiriki hayo mambo unafungua njia ya kuwa mhanga wa kufanyiwa ushirikina
 
1.Unadhan kwa nini mababu zetu walishindwa kuwaroga wazungu na waarabu waliokuwa wakiwatesa miaka hiyo?
2. Kwa nini katika vita vya majmaj risasi hazikugeuka maji pamoja na kinjekitile kuwa alikuwa mganga maarufu sana miaka hiyo?
3. Team zetu za afrika kwa nini zenyewe kwa zenyewe zinarogana ila zinapocheza na wazungu dawa zao team za afrika hazifanyi kazi?
 
Hao ngozi nyeupe na njano mbona walirogwa sana tu...ila habari hizi zilifichwa sana
Kinjekitile pia uchawi wake ulisaidia sana ila kinachitajwa na kutangazwa sana ni kule alikoshindwa
 
walirogwa wapi wakati biashara ya utumwa iliendelea na kufanikiwa sana. wazee wetu waliendelea kuteseka na mwishowe walichukuliwa utumwani.kwa nini hatukushinda vile vita? mi nahitaji ushahidi kuwa wazungu walirogwa sana na wakashindwa maeneo kadhaa. sababu kama mpaka mwishoni waliendelea kututawala na kututesa wao na waarabu then ni wazi kuwa mababu zetu walishindwa.

na kwenye mechi za kimataifa inakuaje?

Soma habari za Osale Otango na wengine utajua nazungumzia nini
 
Back
Top Bottom