Hayo mambo mengine ya kupiga goti ni kuiga uzungu ambao nina hakika kiitikadi zetu hauna mahusiano yeyote na uhalisia wa maisha yetu.
Kibongo bongo demu unaenda kuchagua nae pete ya uchumba, mnaita watu halafu unajifanya kupiga goti na yeye anajifanya kushangaa na kilio juu wakati amepanga kila kitu mwenyewe.
Za kwetu sisi ni kumleta demu kwako, kila siku anajifanya kusahau nguo moja moja, ukitahamaki chumba chote kimejaa nguo zake. Baada ya muda anakwambia sioni siku zangu, anazaa, unaenda kujitambulisha kwao. Baada ya miaka 10 na watoto 3 mnachangisha ndugu na marafiki kufanya sherehe ya ndoa na mtu mloishi kindoa kwa miaka 10. Hakuna mambo ya goti hapo.