Wakuu,
Kuna kipindi nilipita matatizo makubwa sana, kiufupi siendi kwa waganga ila nasali siyo ile deep sana, ila kila kitu changu namtizama Mungu, nikipata tatizo nasali.
Sasa bhana ikafikia kipindi matatizo yakanizidia, uji ukazidi unga. Ni Ile point huoni chochote, mbele ni giza mtindo mmoja. Adui zangu wakaanza kuzitingisha champagne wazifungue, aisee ndio nilikuwa naishia hivyo.
Weight imekata, sina hela, mapenzi nayo yakanichanganya, sina kazi, ni story ndefu sana ila sina kipaji cha Umughaka kuelezea Kwa kirefu. Eh, Huku na huku hali ikazidi kuwa mbaya, sali na kusali wapi, yaani adui wakawa wanafungua vinyaya vya champagne waifungue.
Jamani nilipita kwenye moto, nakumbuka kuna siku niliamka usiku nikalia sana mbele za Mungu juu ya matatizo yangu, vile ambavyo Mungu amewapa adui zangu ushindi, nililia lesso ikajaa kamasi na machozi siwezi elezea hali niliyokuwa nayo.
Nikamwambia Mzee Baba Mungu nahitaji mambo mawili tu; 1. Anichukue (yaani nife) au 2. Aniondolee matatizo, hii ni serious kabisa kwani nilikuwa nimezidiwa na matatizo.
Huwezi amini asubuhi nimeamka macho yamenivimba kwa kulia, sina mbele wala nyuma nikapigiwa simu moja tu n the rest is history.
Nilimwona Mungu aisee, jamani Mungu yuko! Adui wakabaki midomo wazi, wanaulizana imekuwaje? Nilivukaje? Kivipi? Kwanini? Mungu ni mwema, alinivusha. Bado nakula ugali, bado ananipa mitihani ila siyo ile iliyotaka kuniangusha.
Kwakweli mimi na nyumba yangu tutamtegemea yeye mpaka ukamilifu wa dahali, Mungu nakushukuru, siwezi kusahau ulivyonifuta Machozi yangu.
Asikiaye na afahamu siyo chai ni kwl tupu, kwa hivyo ukiona kuna la kujifunza chukua, kama ukidiss sawa tu.