Kamwe sitosahau wema huu aliyonifanyia Mungu

Kamwe sitosahau wema huu aliyonifanyia Mungu

Hamna Mungu hapo wala nini, coincidence ya matukio tu hyo..

Ni kawaida ya wanadamu tukizidiwa tunatafuta kisingizio cha kujificha.

Kete ziko kwa maadui, usiwaache tu afu useme Mungu atatenda. Pambana mwenyewe ushinde. Mungu huyo hawezi kukusaidia in reality, wewe ulisaidiwa na aliekupigia simu.
Khhaaa
 
Wakuu,

Kuna kipindi nilipita matatizo makubwa sana, kiufupi siendi kwa waganga ila nasali siyo ile deep sana, ila kila kitu changu namtizama Mungu, nikipata tatizo nasali.

Sasa bhana ikafikia kipindi matatizo yakanizidia, uji ukazidi unga. Ni Ile point huoni chochote, mbele ni giza mtindo mmoja. Adui zangu wakaanza kuzitingisha champagne wazifungue, aisee ndio nilikuwa naishia hivyo.

Weight imekata, sina hela, mapenzi nayo yakanichanganya, sina kazi, ni story ndefu sana ila sina kipaji cha Umughaka kuelezea Kwa kirefu. Eh, Huku na huku hali ikazidi kuwa mbaya, sali na kusali wapi, yaani adui wakawa wanafungua vinyaya vya champagne waifungue.

Jamani nilipita kwenye moto, nakumbuka kuna siku niliamka usiku nikalia sana mbele za Mungu juu ya matatizo yangu, vile ambavyo Mungu amewapa adui zangu ushindi, nililia lesso ikajaa kamasi na machozi siwezi elezea hali niliyokuwa nayo.

Nikamwambia Mzee Baba Mungu nahitaji mambo mawili tu; 1. Anichukue (yaani nife) au 2. Aniondolee matatizo, hii ni serious kabisa kwani nilikuwa nimezidiwa na matatizo.

Huwezi amini asubuhi nimeamka macho yamenivimba kwa kulia, sina mbele wala nyuma nikapigiwa simu moja tu n the rest is history.

Nilimwona Mungu aisee, jamani Mungu yuko! Adui wakabaki midomo wazi, wanaulizana imekuwaje? Nilivukaje? Kivipi? Kwanini? Mungu ni mwema, alinivusha. Bado nakula ugali, bado ananipa mitihani ila siyo ile iliyotaka kuniangusha.

Kwakweli mimi na nyumba yangu tutamtegemea yeye mpaka ukamilifu wa dahali, Mungu nakushukuru, siwezi kusahau ulivyonifuta Machozi yangu.

Asikiaye na afahamu siyo chai ni kwl tupu, kwa hivyo ukiona kuna la kujifunza chukua, kama ukidiss sawa tu.

Furahia Ukuu wa Mungu[emoji1635]
 
Roho mtakatifu akufungue akili mkuu ili upate kuyaelewa maandiko hususani Biblia.
Nawezaje kuelewa maandiko yenye contradiction nyingi kiasi hiko.

Contradiction ambazo hamna hata mmoja wenu humu anaweza kuzitatua.

Bisha.
 
Sasa km watu tulionao ni km wewe ndio mtachangia nini ktkt mkataba wa DP World? Mama piga kazi nchi yetu ni wajinga wengi sana bado.
Logical non sequitur

Bandari na mada hapo wapi na wapi.
 
Hapana! Hapana kabisa kiongozi!!!

Hiyo umeitoa wapi?

Mkuu, jichunguze! Kama unaamini hivyo, ujue umedanganywa, kabisaa!!!

Imani ni halisi! Imani ni KWELI kwa asilimia mia moja. Imani si kitu cha kubezwa hata kidogo. Imani ni maisha!!! Imanini kila kitu!!!
Mkuu, unaelewa maana ya neno imani.?
 
Hata kama ni kwa imani, unaelewaje kitu kimoja kikaandikwa kwa contradiction nyingi kiasi hiko?

Yani kuna makosa hata ukiyaangalia unaona kabsa huyo Mungu muweza wa yote Mungu mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.
Angekuwepo asingeruhusu kitabu chake kiwe na contradiction nyingi kiasi kile.
Utakapokuwa tayari kujifunza, utaelekezwa hivyo the so called contradiction zitatoweka pia, kwa sababu hazipo tangu hapo.
 
Imani ni kuwa na hakika ya mambo ystarajiwayo. Ni bayana ya mambo yasiyoomekana. Waebrania 11:1
Nko kwenye dhana ya uhalisia tu wa kiswahili siko kwenye imani, hivyo achana na hadithi za alfu lela ulela
 
Utakapokuwa tayari kujifunza, utaelekezwa hivyo the so called contradiction zitatoweka pia, kwa sababu hazipo tangu hapo.
Umejuaje zitatoweka na hazipo?

Hujaweza kutengua hizo nlizokupatia.
 
Back
Top Bottom