Kamusi: ESE Dictionary 1.3 UPDATE mchango wako ni muhimu

Nyasiro

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
1,201
Reaction score
551
Hili ni toleo jipya la hii kamusi ya Kingereza-Kiswahili-Kingereza. Unaweza kufatilia thread ya mwanzo hapa: https://www.jamiiforums.com/tech-ga...roducing-ese-dictionary-%96-%93kamusi%94.html

Katika toleo hili nimeongeza features zilizoombwa na wadau mbalimbali kwenye jukwa hili na sehemu mbalimbali.

Kama kuna bugs zozote tafadhali naomba utoe tarifa pia itapendeza kama ukiweka na screenshot. Download halafu share na mwenzio.

Tembelea: esedictionary.com

BAADHI FEATURES MPYA

  • All returned results can now appear on a single page
  • Copy returned results to clipboard
  • Send returned results to Microsoft Word
  • Register missing words
  • Zoom in or zoom out returned results
  • Ability to choose English or Swahili as Interface language
  • Send app to clipboard when closed or exit when close is selected

1 kamusi.PNG

1-300x211.png

4-300x211.png

DOWNLOAD NOW

Kama umeinstall v1.2 Beta hakikisha una uninstall kwanza kabla ya kuinstall hii version.

Shukrani kwa wote waliochangia mawazo yao hadi kufikia hapa.
Joe Nyandigira, C6 , Stefano Mtangoo, Magembe R. Malima, wickerman, Donn, FREDRICK IHEMBE njunwa wamavoko Deejay nasmile na wadau wote mliotoa mawazo yenu.

Naomba mfanye testing kama kuna shida yoyote ili ifanyiwe kazi pia naomba na screenshot zenu

ONGEZA MANENO
Kama kuna neno umelitafuta na hukulipata katika kamusi hii tunaomba usaidie wengine kwa kuliongeza kupitia: nyasiro.com/kamusi/add.php Itachukua chini ya dakika 5 tu.

NEWS
ESE Dictionary has been listed in the list of 17 best FREE Dictionary --- http://listoffreeware.com/list-of-best-free-dictionary-software/
 
Mkuu Nyasiro hii iko poa zaidi. Nimependa sana ulivyobadilisha user interface. Nashauri uweke language selection wakati wa kuinstall mf. unaweza kuweka English na Swahili ili mtumiaji aweze kuchagua lugha atakayopenda wakati wa installation.
 
Last edited by a moderator:

Ok mkuu asante kwa ushauri wako kwenye toleo lijalo tutaongeza installer languages.

Karibu sana.
 
great work Nyasiro .... nafurahi kushiriki katika production angalau kwa asilimia chache 🙂
 
Last edited by a moderator:
great work Nyasiro .... nafurahi kushiriki katika production angalau kwa asilimia chache 🙂

shukran asante sana mchango wako sio kidogo umesaidia sana hasa katika UI design.

Unaweza tuna screenshot nione inavyo behave kwenye PC yako?
 
Inspired...as always 🙂

:A S wink: Bahati mbaya sikuweka clipboard monitoring.....

BTW

Nlitaka ku-implement KiSwahili Text to Speech katika kamusi hii lakini nimekwama kutoka na kutokuwepo kwa TTS engine. Kuna SwahiliTTS inaonekana imefanywa kwa Java na Wakenya katika Chuo Kikuu cha Nairobi lakini pia sijafanikiwa kuona inavyofanya kazi zaidi ya kuishia kusoma documents tu: http://www.ajol.info/index.php/ajst/article/viewFile/55170/43645

Nilipata matumaini kidogo nilipoona Speech Synthesizer inayo support kiswahili na nimejaribu kuipitia na kuona inavyofanya kazi, kwa ukweli imejitahidi lakini ina matatizo ya stress kwenye kutamka ny na ng' Tatizo sauti zinazokuwa generated sio za kiswahili ingawa zinafuata utamkaji wa kiswahili iangalie hapa + source codes eSpeak: Speech Synthesizer
ningependa kuona SwahiliTTS engine inayofanya kazi ki-swahili na sio kizungu... ichek may be tunaweza kutengeneza engine yetu one day.
 
sad indeed!

Nyasiro,
Watanzania kwa situation ya sasa ni big failure, kuanzia viongozi mpaka waongozwa. Ni vibaya ila acha niseme tu kuwa Watanzania, hasa walio fani za ufundi kwa namna yeyote tumeiangusha sana nchi hii. Nimeshafanya initiative nyingi sana kujaribu kuleta unity ya hawa wataalam ili kufanya kitu ila mara zote nimekuta ni wabinafsi pasipo maelezo. Kila mtu anataka lake na hana mpango wa maslahi ya nchi.

Kwa hiyo nasikitika kusema kuwa hilo kwa sasa halitatokea na kama likitokea, basi itakuwa moja ya maajabu!
Mimi ninafikiria kuwekeza kwenye next generation zaidi kuliko hii ya sasa, so I don't think I will take on this initiative. Nataka kwenda vyuoni ambako vijana hawajawa tainted na ubinafsi uliopo kwa "weledi" wa mtaani.

Tanzania ina safari ndefu, na mpaka tutakapofika ... tuendelee tu na vya kizungu-kizungu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: hbi
shukran asante sana mchango wako sio kidogo umesaidia sana hasa katika UI design.

Unaweza tuna screenshot nione inavyo behave kwenye PC yako?

ese 1.png

Na ikiwa maximized inaonekana hivi
ese2.png

So far naona sasa hivi imesimama vema software
 
sad indeed!
Nyasiro,
Watanzania kwa situation ya sasa ni big failure, kuanzia viongozi mpaka waongozwa. Ni vibaya ila acha niseme tu kuwa Watanzania, hasa walio fani za ufundi kwa namna yeyote tumeiangusha sana nchi hii. Nimeshafanya initiative nyingi sana kujaribu kuleta unity ya hawa wataalam ili kufanya kitu ila mara zote nimekuta ni wabinafsi pasipo maelezo. Kila mtu anataka lake na hana mpango wa maslahi ya nchi.

Kwa hiyo nasikitika kusema kuwa hilo kwa sasa halitatokea na kama likitokea, basi itakuwa moja ya maajabu!
Mimi ninafikiria kuwekeza kwenye next generation zaidi kuliko hii ya sasa, so I don't think I will take on this initiative. Nataka kwenda vyuoni ambako vijana hawajawa tainted na ubinafsi uliopo kwa "weledi" wa mtaani.

Tanzania ina safari ndefu, na mpaka tutakapofika ... tuendelee tu na vya kizungu-kizungu

Naona kama umekata tamaa. Mimi naamini hakuna kinachoshindikana hasa ukizingatia mfumo wa fonolojia ya kiswahili ni rahisi sana. Kiswahili kina irabu tano (a,e,i,o,u) ambazo utamkaji wake hauna mbwembwe. Pia tuna konsonanti na nazali (nasal) sounds ambazo hazina shida kabisa. Hii kitu naona ni rahisi kama kuhesabu 1-2-3. Tukipata engine ya namna hii tutarahisihsa sana utendaji kazi katika sehemu mbalimbali, kwa mfano usomaji wa hotuba na vitabu virefu ambavyo binadamu anachoka kusoma unaweza kurahisishwa sana.

Wazo la kwenda vyuoni ni zuri lakini kwa mfumo wa elimu wa Tanzania ni vigumu kupata mchango unaohitajika kwani unakuta mtu anasoma DIT kwa mfano ana course 10 sasa ukishamwambia kufanya kazi nyingine ya namna hii itakuwa ngumu kwake.

Wakenya wanazidi kutupiga bao kila sekta tupo nyuma sana. Watanzaia tunaumwa huu ugonjwa Tanzanian Surfers Loves News, Entertainment and Pornography na unahitaji tiba.

Tuanze kupunguza uzungu uzungu taratibu tutafika tu.
 
Sijakata tamaa ila naona kuna vitu kuvifanya Tanzania kama team ni kama haiwezekani.
Watu hawako serious, na walio serious wengi wabinafsi. Badala ya kuhangaika nao tumeamu tutafanya kama solo.
Kwa hiyo project ambazo tuliplan ziwe community driven zitabaki internal. Pamoja na mfumo wa elimu kuwa maiti, tutaendelea kumwaga sumu mashuleni/mavyuoni ili kizazi kijacho ndio kifanye yale tuliyo envision yafanywe na kizazi cha kwetu.

Lets die with our selfishness and let the youngsters shine!
 
Mkuu hiyo imekaa poa zaidi.vp kuna uwezekano wa kuifanya app kwenye simu? au haujafikiria hilo. itasaidia sana kwa sisi ambao hatujui lugha alafu pia hatuna pc
 
Bado muda upo. Kinachohitajika ni kujituma na kuonesha juhudi zako bila kukata tamaa kwani haiwezekani juhudi zikaonekana hapo kwa papo. lazima kuwepo muda ambapo mengi yanatokea kama vile kudharauliwa, kutukanwa na kuchekwa. Tusife moyo.
 
Good work, kutakuwa na version nyingine? Nyasiro

Version nyingine itakuwepo kama nitaendelea kupata features request na bugs report. Pia kutakuwa na version mpya kama watu watajitolea kuongeza maneno ambayo hayapo kupitia: [url]http://nyasiro.com/kamusi/add.php[/URL]

Mkuu hiyo imekaa poa zaidi.vp kuna uwezekano wa kuifanya app kwenye simu? au haujafikiria hilo. itasaidia sana kwa sisi ambao hatujui lugha alafu pia hatuna pc

Bila shaka itakuwepo version ya Windows Phone na Android kulingana na mahitaji na michango ya watu kwa sababu muda unaotumika ni mwingi na pesa inatumika. Ntajitahidi kadri niwezavyo tupate version ya Android manake watu wengi wanatumia Android ila sidhani kama itakuwa hivi karibuni.
 
Kuna bug nimeigundua.

Unapo search neno la kiswahili ambalo lina alama " ' " kama kwenye neno ng'ombe kamusi haileti majibu. Bila shaka kutakuwa na shida kwenye SQL SELECT STATEMENT. Ntalifuatilia suala hili.

UPDATE
Nilikuwa nafanya testing:

Na matokeo yanaonesha code hii haitafanya kazi
Code:
select * from dict where swahilisortby = 'ng'ombe'

code hapo juu zina quote 1. katika sql single quote inatumika kuonesha mipaka ya string. kwa hiyo uki search neno kama ng'ombe SQL query ita search mpaka kwenye ng na hii italeta syntax error kwa sababu kunakuwa kuna string 2 ndani ya quote 1

lakini

Code:
select * from dict where swahilisortby = "ng'ombe"
code hii itafanya kazi vizuri kwa sababu kuna double quotes na string ni moja tu.

Sasa nimechanganyikiwa kidogo kuhusu matumizi ya double quotes na single quotes kwenye sql statements

CC Stefano Mtangoo zech snipa Sabrina and all devs
 
You can escape single quotes with two single quotes like 'ng''ombe' that should work, i have not tested it(as i am lazy sometimes'). Try it and let me know if it works.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom