Kampuni za Simu na Siri zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za Simu na Siri zetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Dec 11, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jamani

  Leo katika mambo mengine kuna mtu aliniuliza niko wapi nikamwambia akawa anabisha katika huo ubishi akaenda kwa jamaa zake wa kampuni za simu kuchunguza akaambiwa ukweli kuhusu eneo nililokwepo huko kwenye kampuni za simu

  Sasa bado nina wasi wasi na kampuni hizi za simu kuhusu utendaji wao na mamlaka waliyonayo mpaka kuamua kutoa siri za wateja wao popote walipo bila idhini ya mteja mwenyewe na bila mpango wowote ule

  Nimesikitika sana kwa kitendo hichi na nimehuzunika sana kwa suala hili

  YAANI PAMOJA NA KUTUMIA MAMBO YOTE HAYA WANATOA SIRI ZETU NA MAMBO YETU MENGINE KWA WATU WENGINE AMBAO HATA HAYAWAHUSU KIVIPI ? KWA MPANGO GANI ??
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Pole Shy. Hapo ndipo nami ninapata shida kuhusu employment ethics, confidentiality is of the highest priority katika hali zote. Unajua kwa sababu ya njaa za baadhi ya watumishi wakipewa vijisenti kidogo tu wanatoa siri. Basi Shy kwa Tz mtu akitaka kupata mawasiliano ya mume au mke pale ambapo mmojawapo anahisi kuna ufirauni kati yao basi ni kuwapa pesa tu wafanyakazi wa coy za simu, wata print mawasiliano yako yote na utaumbuka kikweli hasa.

  Kwa upande wa kujua sehemu uliko wanatumia tu freguency na wavelength zao na wanajua kabisa unakaaa wapi. Kule kwenye mitambo kuna geography yote ambapo mitambo yao inaweza kuruka(inaonekana katika satellite). Pia hata katika internet is not safe. Hata hapa ninapoandika ni kuwa wakitaka kuni tress watanipata thru satellite. Hata hivyo siogopi kwa kuwa nafahamu I speak out the truth na anayekerwa anitafute tu. No security katika mitandao at all!!!!
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Endelea kusikitika na kuhuzunika, suluhisho litajileta lenyewe.
   
 4. m

  mussy New Member

  #4
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana na nakubaliana na wewe kuwa sio poa kuwekw mambo ya mtu kwa hadhara kwani hayawahusu.
  Ila kutokana na hizi simu tunadanganyana kinoma so tuache uongo.
   
 5. m

  mussy New Member

  #5
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana na nakubaliana na wewe kuwa sio poa kuweka mambo ya mtu kwa hadhara kwani hayawahusu.
  Ila kutokana na hizi simu tunadanganyana kinoma so tuache uongo.
   
 6. w

  wajinga Senior Member

  #6
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Whats the name of the phone company????????????
   
 7. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  Anyway hiyo inawezekana kabisa. Lakini nina mashaka kidogo kuhusu status ya huyo mtu na umakini wa hiyo kampuni ya simu. Kwanza ni kampuni gani haswa inayofanya utumbo huo !?

  Maana kwa sheria ya haki za faragha( law of privacy) , hawakutakiwa kutoa siri zako kwa mtu yeyeto yule bila ya kufuata utaratibu maalum uliowekwa na sheria hii. Ndio tunajua hata hizi sms zote tunazotuma kwa kupitia mobile phone na hata e-mail huwa zinahifadhiwa kwanza kwenye mitambo kabla ya kuwa deleted. Mtu anaweza kzipata hata sms zako za mwezi mzima ulizo tuma au kutumiwa !

  Ndio nataka kujua hilo shirika la simu ambalo linaweza likatoa siri za mteja wao kwa mtu yeyote kana kwamba hawajui kama kuna sheria ya haki ya kutunziwa siri. Embu tupe haswa uhalisia wa tatizo lenyewe.
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimeshapeleka email kwa watu wanaohusika na mawasiliano katika tume yao naamini watanijibu kwa sasa natafuta kuweza kuonana na mwanasheria ili kuweze kumweleza jambo hili muhimu sana naamini katika vyombo vya sheria tutaweza kupata suluhisho la tabia hii chafu

  hili jambo limenishitua sana na kunisikitisha sana sijawahi kuwa na siku chungu kama leo hii katika maisha yangu
   
 9. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2008
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Anyway hiyo inawezekana kabisa. Lakini nina mashaka kidogo kuhusu status ya huyo mtu na umakini wa hiyo kampuni ya simu. Kwanza ni kampuni gani haswa inayofanya utumbo huo !?

  Maana kwa sheria ya haki za faragha( law of privacy) , hawakutakiwa kutoa siri zako kwa mtu yeyeto yule bila ya kufuata utaratibu maalum uliowekwa na sheria hii. Ndio tunajua hata hizi sms zote tunazotuma kwa kupitia mobile phone na hata e-mail huwa zinahifadhiwa kwanza kwenye mitambo kabla ya kuwa deleted. Mtu anaweza kzipata hata sms zako za mwezi mzima ulizo tuma au kutumiwa !

  Ndio nataka kujua hilo shirika la simu ambalo linaweza likatoa siri za mteja wao kwa mtu yeyote kana kwamba hawajui kama kuna sheria ya haki ya kutunziwa siri. Embu tupe haswa uhalisia wa tatizo lenyewe.
   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa online then mtu mmoja akanitumia im kuniuliza nipo wapi kwa muda huo sikumwambia nikamwambia niko mbali kidogo nikamtajia na eneo akaniambia subiri kidogo

  baada ya muda akauliza huko anapojua yeye akaniambia mbona simu yako inaonyesha uko sehemu fulani ?

  Sasa nikashangaa sana kwanini taarifa zangu amezipata mapema sana na mimi bila kujulishwa manake mimi ni mteja wa kampuni hiyo haiwezekani aulize tu apewe kiurahisi hivyo
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
 12. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280

  Kama ni kweli huyo mtu alipata locational info zako kutoka kampuni ya simu basi tuna matatizo makubwa sana.

  Hata hivyo nadhani ni reputational risk kubwa kudanganya kuhusu sehemu ulipo kama unayemdanganya hujui yupo wapi! Pengine alikuwa anakuona live and he/she wanted to test your level of integrity.
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nathani tunahitaji mdahalo mkubwa na wa kina kuhusu kitu hichi kwa kushirikiana na wadau wa kampuni hizi za simu
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Acha uongo kijana,tafuta shule usome hata diploma kwanza.....
   
 15. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,280
  Trophy Points: 280
  Wanajua kila kitu but hawatakiwi kutoa siri za wateja
   
 16. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Text messages zinaweza kuwa diverged bongo, at a price.

  Hubby akiwa na kimwa mama mwenye nyumba anaweza kuongea na wakuu wakawa wanamfowardia messages zote anazotuma hubby.
   
 17. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ndo maana siku ile......... yaani unataka kuniambia kuwa........ Lakini mbona.......... Mh..... hii tekinolojia mbona iko hivi lakini?
   
 18. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hao wamekiuka maadili ya kazi yao.Wamekiuka pia masharti ya leseni(waliyopata kutoka TCRA) ya kutoa huduma hiyo.
  Sasa basi,pale TCRA(pale mawasiliano house,along Ali hassan mwinyi road opp.Las Vegas Casino,kama hutaki hiyo basi Jolly club) kuna kitengo cha consumer and industry affairs(DCIA),pia kuna kamati(customer consultative committee,CCC).Hao wanashughulika na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini chini ya sheria ya mawasiliano ya mwaka 2003,sikumbuki kifungu!Peleka malalamiko yako huko na ushahidi (hapa ndio ipo shida).
  Kwa maelezo zaidi(na kufahamu haki zako kuhusiana na huduma za mawasiliano nchini) tembelea TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority
   
 19. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #19
  Dec 12, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine kama haujui jinsi technolojia zinavyofanya kazi bora uache tu kuandika, kuliko kuandika utalaam wa vijiweni.
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wewe sema jamaa alikuwa anakuona alitaka ajue kama ulikuwa unamdanganya kwa maana waTZ wengi wanatabia ya kudanganya sana kwenye cmu mtu anakwambia nipo Mbezi kumbe yupo Magomeni.
  Ndugu yangu Shy hata ulalamike haikusaidii kitu unapoteza muda wako bure we endelee na hamsini zako tu kama kawa.......
   
Loading...