Tetesi: Kampuni ya Yapi Merkezi kuchunguzwa kwa rushwa na kuingilia mambo ya ndani Tanzania

Wakati wa JPM, kazi ilipigwa kwelikweli na hii hii kampuni.

Kwa ufupi Hawa wakandarasi ni wakandarasi wa kimataifa, sio wakuokota , wanefanya ujenzi nchi mbalimbali.

Kwa Sasa wameamua kua hivo ili kuendana na Serikali ya Sasa ya Samia ilojaa upigaji na kutowajibika .

Lini Samia amewah fanya angalau ziara yenye lengo la kufatilia utendaji kazi ??.( Ukinielewa hapo, Utajijua wee ni Mpumbavu namba Moja).
Hakuna upigaji acha kukariri
Alafu pia hao wanaweza pia kukosea Kama wanavyokosea wengine, sio malaika hao.
 
Haihitaji degree kuliona hilo huyu mwamba wanataka kumnyang'anya tender ili waweke mtu wao ambaye watakula 1O% yao kila mgao ukitoka ku fund ujenzi.

Hilo zengwe ni kubadili timu ya fisi tu 😁😁😁 kama walivyobadili kwenye ishu ya vichwa vya treni kwa kisingizio kuwa alieagizwa alishindwa kuvileta kwa wakati.

R.I.p Magufuli yani sahizi wataelewa kuwa waliokuwa wanamkwamisha ni wapiga madili.
Natamani kuufahamu JPM aliwaroga kwa uchawi upi nyie watu!! Kwahiyo unajifanya umesahau kwamba huyo Mturuki aliletwa na utawala wa JPM? Yaani unajisahaulisha hicho kipande cha daraja kinachotajwa kilijengwa wakati wa huyo huyo JPM na hitilafu yake iligundulika wakati wa huyo huyo JPM!! Unataka kujisahaulisha hata kipande cha Dar Moro kimechukua miaka kadhaa wakati wa huyo huyo JPM! Wakati wewe na wenzako mnajisahaulisha, pitia huu uzi hapa chini kisha tujuze ikiwa wakati huo JPM alikuwa keshafariki

Nimeona daraja la waya (cable stayed bridge) la SGR Kamata likivunjwa, shida nini?

 
Narudia kukuambia, hawa waturuki ni wakandarasi wa kimataifa !!. Zingatia hili


Kama suala la upigaji hulioni ... Pole sana.
Sawa wa kimataifa. Kwahiyo wakifanya mambo ya ovyo yaachwe eti kisa waliletwa na JPM?! Hilo daraja hitilafu zilionekana tangu wakati JPM yupo hai kwahiyo unashangaza unapodai eti JPM ndio alikuwa dawa ya watu kama hawa wakati matatizo ya hao jamaa yalianza tangu wakati JPM yupo hai
 
Ndio anaundiwa zengwe achomolewe....
Anaundiwa zengwe na nani?! Kwani kwa mfano lile daraja ambalo tangu zamani lilishasemwa lipo chini ya kiwango lilijengwa na nani?! Hivi ulishajiuliza kingetokea nini kama lile daraja lingekuwa maporini huko na watu kufungasha virago mara baada ya "kukamilika" kwake?!
 
Habari nzito hii kama taifa. Miradi mikubwa kama hii inatakiwa nchi ijitayarishe ktk kila nyanja.

Kuanzisha mradi kwa kustukiza kufuatia tamko, badala ya tamko hilo kujadiliwa kwa kina kuona vipi litatekelezwa, athari zake kiuchumi, athari yake kwa bajeti ya nchi, kimazingira, uwezo wa nchi kufanya usimamizi wa karibu wa utekelezeji n.k


Miradi mikubwa inatakiwa iangaliwe kwa upana na masuala mtambuka kutiliwa maanani ili uweze kumsimamia mkandarasi vizuri uwezo wake na aina ya modeli ya ujenzi anayojinadi nayo au kuitumia katika utekelezaji za mradi husika

Build-Operate-Transfer systems

View attachment 2313992


TOKA MAKTABA:
Tarehe 12 November 2017

Zitto: Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli na vifaa vyote vikatoka Uturuki?


Hoja na maswali ya Zitto Kabwe, yanafaa kuwa hadidu rejea ya mjadala mpana juu ya miradi mikubwa kwenye jukwaa hili wakilishi la wananchi wote yaani JF : soma zaidi hapa chini :

 
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vyadaiwa vimeanza uchunguzi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Yapı Merkezi Bwana Erdem Arioglu.Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Arioglu anatuhumiwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa SGR huku akiwatendea visivyo makandarasi wa Kitanzania kwa kuwacheleweshea malipo yao.

Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni.Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.

Mbali na tuhuma hizo kampuni hiyo pia inatajwa kuendelea kuipa Tanzania hasara ya mabilioni kutokana na ujenzi wa chini ya viwango katika baadhi ya maeneo.Eneo mojawapo ni kipande cha daraja la Nkurumah eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliamuriwa kuvunja na kuanza ujenzi upya baada ya kuonekana liko chini ya kiwango ikiwemo muonekana wa wazi wa nyufa kama inavyoonekana pichani!.

Katika baadhi ya maeneo ya mradi huo usanifu umekiuka angalizo kwenye njia za maji na kuzifunga jambo ambalo linahatarisha usalama wa matumizi ya mradi huo pale utakapokamilika.Athari za jambo hili zinaelezwa kuwa zitailetea nchi maafa makubwa zaidi kama ajali na hasara za ukarabati wa mabilioni pale ambapo mradi huo utakamilika.

Katika tuhumu hizo imeelezwa kwamba serikali imeunda timu ya uchunguzi huku timu nyingine ya siri ikihakiki shughuli na rushwa katika mradi huo kabla ya kutoa ripoti rasmi.

View attachment 2313893
Hawa waliletwa na nani kwa utaratibu upi ?
 
Inaonekana walishakamuliwa na awamu ya 5 na sasa wanapigwa mkwara ili wakamuliwe na awamu ya 6. Waturuki wanachunwa kama mbuzi.
 
Sioni dalili sgr kuish miak ya HV ksribuni humuoni kina about na bm wanazidi kuingiza vyuma vipya kila siku Tena kwa root za dar moro
 
..kipande nilichohoji ucheleweshaji wake ni Dar to Morogoro.

..maelezo ya serikali yalikuwa kipande hicho kinajengwa kwa kutumia fedha za ndani, sio mkopo, donors / wafadhili.

..sijahoji kuhusu Moro Dom Makutupora. Lakini pia ninavyokumbuka fedha za kipande hicho ni mkopo toka kwa mabenki ya ulaya / mabeberu.

..mimi nilikuwa mmoja wa wanaJF waliotetea Yapi Merkez waliposhinda tender. Niliangalia rekodi yao ya ujenzi Dubai, Qatar, etc nikaamini wako vizuri. Sijui ni kwanini wamechelewesha mradi huu kwa kiwango hiki.

..hata Wachina wakichelewesha kazi tutahoji kulikoni. Tunatakiwa tu-demand kazi zenye kiwango zinazokamilika kwa wakati.
Huko uarabuni hakuna mito, milima na misitu.
 
Mkuu tatizo kila rais anayekuja anajitahidi kuanzisha miradi mikubwa lengo ni kutakatisha fedha na upigaji miradi inakuwa over budgeted makusudi plus ten percentages, upigaji huu hauna kelele, ndo mana mwendazake alianzisha miradi ya ujenzi kila kona, ujenzi wa vuvuko vya mabilioni lakini nyuma ya pazia makampuni ni yao au wanamiliki hisa ktk hayo makampuni, Africa viongozi na wananchi wazalendo udongo ulishafukia tuliobaki wote ni wezi tu na wachumia tumbo, Uhuru waliopigania mababu zetu hauna maana kabisa.
Usalama wa Taifa kweli wanaangalia huu uozo ukiendelea na hakuna kinachotokea!
 
..kipande cha Dar to Moro serikali ilisema tunatumia fedha za ndani, na tulihakikishiwa kwamba fedha hizo zipo.

..binafsi nilitegemea miaka hii ujenzi utakamilika kwa haraka kuzidi wakati wa Tazara kwasababu ya maendeleo ya kiteknolojia na uwepo wa vifaa na mitambo ya ujenzi bora zaidi.

..nimelinganisha Dar to Moro vs Dar to Kapirimposhi. Sioni mantiki ya mkandarasi wa Sgr kuchelewa kukamilisha kipande kidogo hicho kwa wakati.

Hiyo ya kuhakikishiwa uwepo wa fedha hakuna anayeujua ukweli maana tumeona mengi baada ya huyo aliyetuhakikishia kuondoka.

Ile reli ya Mchina fedha ilikuwa inatoka kwake (sina hakika kama ilikuwa mkopo au la) na wafanyakazi asilimia kubwa ilikuwa wanatoka kwake sasa hapo hakukuwa na kitu cha kuchelewesha.
 
Sawa wa kimataifa. Kwahiyo wakifanya mambo ya ovyo yaachwe eti kisa waliletwa na JPM?! Hilo daraja hitilafu zilionekana tangu wakati JPM yupo hai kwahiyo unashangaza unapodai eti JPM ndio alikuwa dawa ya watu kama hawa wakati matatizo ya hao jamaa yalianza tangu wakati JPM yupo hai
Mazezeta ya mwendazake ni janga la taifa
 
chanzo cha habari:thetanzaniapost.com

Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimeanza uchunguzi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Yapı Merkezi Bwana Erdem Arioglu. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Arioglu anatuhumiwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa SGR huku akiwatendea visivyo makandarasi wa Kitanzania kwa kuwacheleweshea malipo yao. Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni. Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.

Mbali na tuhuma hizo kampuni hiyo pia inatajwa kuendelea kuipa Tanzania hasara ya mabilioni kutokana na ujenzi wa chini ya viwango katika baadhi ya maeneo. Eneo mojawapo ni kipande cha daraja la Nkurumah eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliamuriwa kuvunja na kuanza ujenzi upya baada ya kuonekana liko chini ya kiwango ikiwemo muonekana wa wazi wa nyufa kama inavyoonekana pichani!.

Katika baadhi ya maeneo ya mradi huo usanifu umekiuka angalizo kwenye njia za maji na kuzifunga jambo ambalo linahatarisha usalama wa matumizi ya mradi huo pale utakapokamilika.Athari za jambo hili zinaelezwa kuwa zitailetea nchi maafa makubwa zaidi kama ajali na hasara za ukarabati wa mabilioni pale ambapo mradi huo utakamilika.

Katika tuhumu hizo imeelezwa kwamba serikali imeunda timu ya uchunguzi huku timu nyingine ya siri ikihakiki shughuli na rushwa katika mradi huo kabla ya kutoa ripoti rasmi

Je, ujasusi wetu hupo bize na kulinda ccm mpaka haya yanatokea
 
Back
Top Bottom