Kampuni ya Silent Ocean China hawapokei tena lose cargo, wanapokea makontena tu

Kweli wakumbuke wanamitaji midogo na huu utaratibu mbona watu wengi tu umewatoa na mpaka kufikia kuwa na uwezo wa kuagiza kontena peke yako!
.
Ila kimeeleweka kumbe wengi bado mitaji ipo chini alafu tunataka ulimbukeni

Unakuta mtu ana million 20 nae anataka kuruka kwenda kufunga mzigo China.. Sasa hapo ukipiga nauli, accomodation si bora hiyo pesa aiongezee hapo kwenye mtaji.. Alichokuwa anakifanya Silent Ocean hakina tofauti na ambacho wao sasahivi wanatakiwa kukifanya, yeye alikuwa anawakusanyia mizigo anajaza kontena then anaituma na sio kwamba alikuwa anatuma hizo CBM 5 kama zilivyo.. Kamfano maduka ya Stationeries yamefuatana pale mtaa wa Uhuru, wajichange wampe mmoja awe ndiye anaenda huko na sio kila mmoja kwenda kufunga mzigo kivyake..
 
20ft-container-approximately 26-28-CBM; 40ft-container.

Hamna container la CBM 200.

Labda tumuulize Waziri Mkuu Majaliwa anaweza kutusaidia.-

Wapi nimesema kuna kontena la CBM 200??

Kwahiyo lipo kontena la CBM 5??
 
Watanzania,

Baada ya sakata la makontena kupamba moto leo hii nipo China nimepeleka mzigo wangu kwenye kampuni ya usafirishaji mizigo ya Silent Ocean iliyopo Guangzhou China.

Wamesema hawapokei lose cargo kwa sasa wanapokea makontena wameniambia kama unaweza kujaza kontena tuletee tutakusafirishia mpaka Dar es Salaam.

Hili ni pigo kubwa kwa wafanya biashara amabao hawana uwezo wa kujaza kontena zima nimerudi na mzigo wangu hotelini sijui cha kufanya.

Wafanya biashara wadogo wadogo tutafanyaje ili mizigo yetu ya lose cargo iweze kufika Tanzania.

Nendeni kwa Eliasi mchina na boss wenu kwa mara nyingine awe Mzee Damasi
 
20ft-container-approximately 26-28-CBM; 40ft-container.

Hamna container la CBM 200.

Labda tumuulize Waziri Mkuu Majaliwa anaweza kutusaidia.-

Cubic Meter 200 zinakaa kwenye Kontena 4 za foot 40..

Cubic Meter 200 zinakaa kwenye Kontena 8 za foot 25..

Tatizo mnakalili mno wazee..
 
Mkuu hawa wasikuumize kichwa.. kwani zamani walikuwa wanaagizaje??

Tatizo walishazoea safari za China na kwenda kupiga selfie wazitume kwenye mitandao.. Logic ndogo tu, kama unaagiza CBM 5 mkikusanyika watano tu wa aina hiyo mnajaza Kontena.. Na uzuri pale Kariakoo maduka yao huwa yanafuatana, sasa sijui wanashindwaje kushirikiana waagize pamoja..
Haya mambo yalishafanyika zamani na watu wakawa wanashindwa kuelewana yule mwenye jina la bill ndiyo anawapangia bei mzigo utakapofika na yeye ndiyo anamtafuta Clearing-Forwarding-Agent, wanapanga bei anaongeza na zake kisha anapita na bill kwa kila mtu mnamlipa anakula chake watu walikuwa wanakwepa haya mambo.
 
Mkuu Ritz wewe ni mtu mwenye uelewa ebu shughulisha akili yako... Ina maana akitumwa mmoja mzigo wa kujaza kontena, akaenda China akafunga then akaenda kuutuma kwa hao Silent Ocean kutakuwa na usumbufu?? Mzigo unasafirisha kama ni wa mtu mmoja na sio kama umechangwa na wengi..

Tatizo la hawa wafanyabiashara letu linalowakwamisha hapa ni kutokuaminiana na kurushana hakuna kingine hapo mkuu..
 
Last edited by a moderator:
Nendeni kwa Eliasi mchina na boss wenu kwa mara nyingine awe Mzee Damasi
Ndugu yangu Eliasi kakata watu miguu wengi sana watu walimpelekea bills zao pesa yote kaingiza kwenye kamali kaliwa mizigo kaikimbia wear house yake usitukumbushe machungu.
 
Hakuna anayetaka kukwepa kodi, lakini tunalazimishwa kukwepa kulipa kodi. Na nina uhakika 99% ya Watanzania kwa njia moja ama nyengine keshawahi kukimbia kulipa kodi, kwa kujua ama kutokujuwa. Mifano ni mingi lakini natowa mfano mmoja.

Jee Health insurance, sitting and travelling allowances, fuel allowances zinakatwa kodi kutoka kwa anayepewa huduma hizi kutoka kwa muajiriwa wake?

Jee unalipa income tax kutoka kwenye kipato chako cha ziada kama vile unamiliki taxi, bodaboda ama bajaji wakati huku ni muajiriwa katika sector nyengine?

Kwa sasa rates zetu za kodi ni kubwa mno ukilinganisha na matakwa na umasikini wa Mtanzania. Vyakula vizuri vyenye siha kama olive na sunflower oil vina VAT wakati mafuta ya OKI/Korie hayana. Ina maana Serikali wanatulazimisha masikini tule vyakula vibovu. Lakini kwa kuonesha upendo wake Serikali yetu kwa wananchi wake, ukisha kuumwa kwa kutokula vyakula bora vyenye kodi zote ikiwemo VAT, wanakuonesha upendo wa kukuondolea kodi zote kwenye dawa. Ni mapenzi baada ya kifo.
 
Mkuu Ritz wewe ni mtu mwenye uelewa ebu shughulisha akili yako... Ina maana akitumwa mmoja mzigo wa kujaza kontena, akaenda China akafunga then akaenda kuutuma kwa hao Silent Ocean kutakuwa na usumbufu?? Mzigo unasafirisha kama ni wa mtu mmoja na sio kama umechangwa na wengi..

Tatizo la hawa wafanyabiashara letu linalowakwamisha hapa ni kutokuaminiana na kurushana hakuna kingine hapo mkuu..
Ahahaha!!! Yaani mfano mimi nauza kiatu Timberland najua soko lake ambalo bei zipo chini na ubora wake nimtume mtu anayeuza madera akaniniulie Timberland.

Kuna mtu anauza jeans za kiume jeans za kike hajui utamtuma jeans za kike.

Kuna mtu ananunua mzigo wake department store zile death stock ni chimbo lake akifika hapo anachagua pc moja moja unadhani atamtuma nani.

Kumbuka wachina wahuni sana bila kusimamia mzigo wako watakufungia size moja items zote wewe unataka watu watoane roho.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania,

Baada ya sakata la makontena kupamba moto leo hii nipo China nimepeleka mzigo wangu kwenye kampuni ya usafirishaji mizigo ya Silent Ocean iliyopo Guangzhou China.

Wamesema hawapokei lose cargo kwa sasa wanapokea makontena wameniambia kama unaweza kujaza kontena tuletee tutakusafirishia mpaka Dar es Salaam.

Hili ni pigo kubwa kwa wafanya biashara amabao hawana uwezo wa kujaza kontena zima nimerudi na mzigo wangu hotelini sijui cha kufanya.

Wafanya biashara wadogo wadogo tutafanyaje ili mizigo yetu ya lose cargo iweze kufika Tanzania.

Wapo wachina wanasafirisha loose cargo.

Pia wapo watanzania wanasafirisha loose cargo pia.
 
Unakuta mtu ana million 20 nae anataka kuruka kwenda kufunga mzigo China.. Sasa hapo ukipiga nauli, accomodation si bora hiyo pesa aiongezee hapo kwenye mtaji.. Alichokuwa anakifanya Silent Ocean hakina tofauti na ambacho wao sasahivi wanatakiwa kukifanya, yeye alikuwa anawakusanyia mizigo anajaza kontena then anaituma na sio kwamba alikuwa anatuma hizo CBM 5 kama zilivyo.. Kamfano maduka ya Stationeries yamefuatana pale mtaa wa Uhuru, wajichange wampe mmoja awe ndiye anaenda huko na sio kila mmoja kwenda kufunga mzigo kivyake..
Stationery unaweza kufanya hivyo lakini siyo vitu vya fashion kama nguo na viatu mikoba, watu wanasafiri na dola 500 na bado wanapata faida nzuri tu.
 
Ahahaha!!! Yaani mfano mimi nauza kiatu Timberland najua soko lake ambalo bei zipo chini na ubora wake nimtume mtu anayeuza madera akaniniulie Timberland.

Kuna mtu anauza jeans za kiume jeans za kike hajui utamtuma jeans za kike.

Kuna mtu ananunua mzigo wake department store zile death stock ni chimbo lake akifika hapo anachagua pc moja moja unadhani atamtuma nani.

Kumbuka wachina wahuni sana bila kusimamia mzigo wako watakufungia size moja items zote wewe unataka watu watoane roho.

Hapa naongelea watu wanaoagiza mzigo unaofanana.. Wa hayo madela waagize kivyao na hao wa nguo za kiume kivyao na kadhalika.. Au kuliko muende watu 5 au 6 ni bora muwatume wawili.. Hivi wafanyabiashara wa Rwanda, Burundi, Malawi na Kongo mbona wanafanya hivi na wala hakuna tatizo..
 
Stationery unaweza kufanya hivyo lakini siyo vitu vya fashion kama nguo na viatu mikoba, watu wanasafiri na dola 500 na bado wanapata faida nzuri tu.

dola 500?? Sasa mbona hiyo ni pesa ya mtu wa mkoa anayefunga mzigo hapo K/koo wa kwenda kuuza mwezi tu kule mkoa..

Sasa dola 500 si bora uagize kwa eBay tu
 
Mkuu Ritz wewe ni mtu mwenye uelewa ebu shughulisha akili yako... Ina maana akitumwa mmoja mzigo wa kujaza kontena, akaenda China akafunga then akaenda kuutuma kwa hao Silent Ocean kutakuwa na usumbufu?? Mzigo unasafirisha kama ni wa mtu mmoja na sio kama umechangwa na wengi..

Tatizo la hawa wafanyabiashara letu linalowakwamisha hapa ni kutokuaminiana na kurushana hakuna kingine hapo mkuu..

Kama sheria ya cargo forwarding ifatwe huko China na clearance hapa Tanzania, basi kila mtu mwenye mzigo, consignee, anatakiwa awe na BL yake. Mzigo wa namna hii unagunguliwa Warehouse ya anayeitwa, consolidator, ambaye appointed na TRA na kila mtu analipishwa kodi kutokana na asili na idadi ya mzigo alopakia.

Kuchanga na kutumia BL moja ina athari zake kisheria ya kodi, tutupilie mbali kutoaminiana. Unapotia mzigo kwa jina lako, mwisho wa mwaka TRA wanajuwa wewe ndiye ulotia mzigo wa thamani ya container kadhaa. Sasa unapoenda kulipa kodi ya Mil 1 mwisho wa mwaka wakati umeingiza container 1,2 ama tatu na stock huna, unakuwa hueleweki kama uli share na kina Mushi na Masawe container moja. Vile vile consignee anaweza kufaidika kwenye VAT return kutoka kwenye import VAT, ataweza kuidai na kulipa difference ya katika mauzo yake. Wenzake itakula kwao. Itabidi walipe yote walokusanya kutoka kwa wateja kwa bidhaa walizo import

Hiyo ni kwa ufupi tu. Inapokuja suala la kodi, kila mtu abebe msalaba wake
 
Last edited by a moderator:
Ahahaha!!! Yaani mfano mimi nauza kiatu Timberland najua soko lake ambalo bei zipo chini na ubora wake nimtume mtu anayeuza madera akaniniulie Timberland.

Kuna mtu anauza jeans za kiume jeans za kike hajui utamtuma jeans za kike.

Kuna mtu ananunua mzigo wake department store zile death stock ni chimbo lake akifika hapo anachagua pc moja moja unadhani atamtuma nani.

Kumbuka wachina wahuni sana bila kusimamia mzigo wako watakufungia size moja items zote wewe unataka watu watoane roho.

watu hawajui wanaandika tu,, china kule kuna machimbo na usiposimamia mzigo wako unafungiwa kituko,, na pia vitu hatununi sehem moja, ni unakusanya vichochoro tofauti then unapak ndio unapeleka silent,,

kampuni za loose cargo zipo nyingi,, ila tatizo ma agent wengi bongo longo longo na wanaiba mizigo,,

silent watu wengi tuliwapenda sababu mizigo haipotei, wana customer service nzuri, wana trcaking system nzuri,, na automatic sms update via system yao kila stage ya mzigo unapofikia mpaka unapotoka bandarini,, hakuna usaniii wala usumbufu kwa mteja,, ambapo ma agent wengine mizigo inapotea na uzembe mwingi wa ma storage bandarini,,

pia loose cargo ina high risk ya kupotea than FCL,, so kutumia agents wa kibongo kwenye loose cargo ni kujitafutia kilio,, bora silent alikuwa tofauti na more serious kwenye loose cargo na hakuna cases za mtu kupoteza mzigo wake wala storage
 
Pole mkuu wangu wenye nguvu ambao wanafunga makotena wanaendelea kupeta Silent Ocean, jamaa wameamua kuachana na lose cargo zinaleta maneno kuwa wanakwepa ushuru basi tuone hizo kampuni kama zitaweza kusafirisha lose cargo.

Nyie wezi wa kodi tu, na mtakoma sana mwaka huu. Hapa kodi tu Mpaka muisome namba kisawasawa
 
dola 500?? Sasa mbona hiyo ni pesa ya mtu wa mkoa anayefunga mzigo hapo K/koo wa kwenda kuuza mwezi tu kule mkoa..

Sasa dola 500 si bora uagize kwa eBay tu
Hiyo dola 500 akimwaga mzigo wake anauza wiki unaisha tena anapata super profit drip mbili tatu ya tatu anasafiri na dola 900 mpaka 10,000.

Mkuu game ya kariakoo huijui jaribu kufanya research kiduchu.

Nimecheka sana mtu wa kariakoo unamwambia anunue mzigo online eBay.
 
hakuna mfanyabiashara mwehu wa kununua mzigo kwa e bay.

kwanza ni more cost na a crazy decision ever eti unune mzigo e bay,

watu wanajiandikia tu hata hawajui lolote kuhusu biashara.

ununue kitu e bay ukajaze dukani,, hiki ni kituko cha mwaka,he he he kimenifanya nicheke sana,, ndio maana nasema ubishe kitu unachokijua kwanza sio unabisha tu
 
Back
Top Bottom