Kampuni ya Dubai kuendesha Tanzania Airways | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya Dubai kuendesha Tanzania Airways

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sulphadoxine, Jun 23, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KAMPUNI ya Glasgow International GT LLC ya Dubai imekubali kuwekeza
nchini kwa kuanzisha shirika jipya la ndege linalotarajiwa kuanza
kutoa huduma zake katika kipindi cha miezi sita ijayo kuanzia sasa.

Makubaliano hayo yalifanyika jana jijini hapa baada ya kufanyika
kikao baina na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu na Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Glasgow International General Trading LLC ya Falme za
Kiarabu, Bahram Taherian.


  Mwenyekiti huyo akiwa ameambatana na ujumbe wa Maofisa wa Kampuni
hiyo alieleza nia yake ya kuwekeza nchini kwa kuanzisha Shirika la
Ndege litakaloitwa Tanzania Airways.


  Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika kikao hicho, ndege za kampuni hiyo zitakuwa zikifanya safari zake hapa nchini ili
kuongeza ushindani katika huduma hiyo ya usafiri wa anga na baadaye
litafanya safari za nje ya nchi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri Nundu alipozungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kikao hicho, viongozi wa Kampuni hiyo wamekubali kuanzisha shirika jipya la ndege katika kipindi cha miezi
sita ijayo ili kuboresha upatikanaji wa usafiri wa anga.


  Nundu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga alisema kuanzishwa kwa
shirika hilo jipya kutakuwa kumefungua ukurasa mpya katika ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga hapa nchini ambapo hata bei ya nauli
itakupungua kutokana na kuongezeka kwa ushindani katika utoaji wa
huduma hiyo.


  Alisema katika makubaliano hayo shirika hilo litakuwa na makao yake
hapa nchini pamoja na kufuata sheria zote za nchi ikiwa ni pamoja na
kulipa kodi ambapo Serikali haitakuwa na ubia na shirika hilo

Hizi ni miongoni na hatua zinachokuliwa na Serikali ya awamu ya nne katika kuboresha huduma ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi na utoaji wa huduma hiyo kwa maendeleo ya
Taifa.
   
 2. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu na nini hatma ya Air Tanzania?
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Imebakia kuwa Kampuni ya Mfukoni..
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanaanzia na ndege aina gani?
   
 5. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu Air Tanzania wana ndege mbili na raslimali nyingine kama majumba n.k, huu mfuko itabidi uwe mkubwa sana mkuu.
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hata huyo waziri Nundu sio Creative.

  Air Tanzania ingeuza Shares kwa watanzania. Air tanzania wauze shares za 51% kwa watanzania na hivyo management ikakuwa na mix of people. hivyo ubadhirifu hautakuwepo na kutakuwa na efficiency. Pia litakuwa shirika la Watanzania.

  Angalia kenya Airways, Serikali ya kenya ina some % na watu wa kenya wana some % na ni heshima kwa kenya.

  Hata Uganda Air na Rwandese Airlines.

  OOh poor Tanzania, Tanzania is poor because of poor minds of leaders.

  OOh Tanzania leaders, selfishness thinking of 10% is killing Tanzania softly.
   
 7. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Siku hizi ni 20%.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  A step in the right direction!
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa hakika ni hatua sahihi - kwani wakijaribu kuifufua ATC mambo yatakuwa yaleyale ya kumaliza resources za umma bila tija.
   
 10. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Waache waanzishe lakini jina libaki air tanzania, tanzania airways ndo nini sasa???????????
   
 11. C

  Chumbageni Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mbona hata website yao ni tabu kupata...mhh!
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Magamba kwa nini wasi-give up tu kwene kumiliki shirika la ndege? is it neccessary kuwa na shirika la ndege la umma na kuendelea kufuja ela ya walipa kodi kwene shirika ambalo lilishakufa kitambo sana?
   
 13. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mawazo mazuri, ngoja tusubiri matokeo
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  the problem we have kama watanzania ni kutangaza mambo tunayoongea kwenye chai au kahawa... we had the chinese here, then we were told tunanunua ndege nyingi tu, now dubai etc. wakati fly 540 never trumpeted anything but they brought ndege...

  there is something wrong with our business model and communication tactis, everything is sooo political and utopic that one find it unrealistic

  I hope Nundu understands where he is in terms of realism otherwise his name will really mean the nundu rather than Nundu
   
 15. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nyie bwana hivi unadhani shares zinauzwa tu. Yaani air Tanzania wakianza kuuza shares kwa hali ya sasa hakuna atakayenunua. Na atakayenunua naye lazima atakuwa hafaham anachofanya au anahitaji kupimwa akili. Unanunua share kwenye kampuni ambayo ni loss making??? Huu utakuwa wizi wa wazi. ukinunua shares unakuwa mmiliki that means ile loss pale na wewe una mgawo. Shirika lile kwa sasa ni gumu saana kuuzika angalau liwe kwenye break-even. Otherwise madai ya kwamba shirika limeuzwa ni kwamba litauzwa kwa bei ya ajabu. Ndio maana unasikia kila siku Wachina mara wananihii.
  Hapa tatizo ni kuoneana aibu katika kufanya maamuzi. Shirika lile lingeachana kwanza na habari ya kuweka mtaji. Wangeanza kufumua ule mfumo. Wanahitaji wafanyakazi wachache saana. Halafu waangalie mali zinazomilika na shirika kwa hali ya sasa ya kibiashara. Waangalie incentives za wafanyakazi na wazibe mianya ya wizi. Walipe madeni yao yote. Kisha wakodi ndege 2-3 tu. Wauze shares kwa Watanzania na mashirika ya kueleweka ya ndege yenye uzoefu ndipo biashara ianze. Na watu wa serikali waache kupanda ndege zao kwa mkopo.
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha shea zangu nilizonunua tz oxygen limited mwaka wa kumi na kitu sijaambulia hata nilu ya kupiga kwenye kibanda changu. Unanitia uchungu maana zile noti za blue nazikumbuka kama nazitoa sasa hivi pale nbc mazengo branch dom mkuu usinikumbushe machungu.
   
Loading...