Kampuni mbili mpya za simu za mkononi zaingia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni mbili mpya za simu za mkononi zaingia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mag3, Nov 22, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Profesa John Nkoma (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni mpya ya simu ya Mycell, Bw. Yusuph Manji leseni ya biashara katika hafla iliyofanyika, Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia ni Ofisa Mawasiliano wa TCRA, Bw. Victor Nkya.

  Je, ni huyu kijana mdogo ndiye anaitikisa serikali ya Tanzania ama mwingine ? Je, ni huyu ndiye mfadhili mkuu wa Yanga ? Je ni huyu kweli ? Kweli pesa kiboko.
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hizi hafla hafla hizi zimezidi. Kwani kuna ulazima gani wa kufanya hafla ili kukabidhiwa leseni?
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Yaani kitu ambacho kinatakiwa kitumwe kwa posta au kiende kuchukuliwa ndani ya mfuko wa kaki kinafanyiwa sherehe na viongozi wanaenda kusherehekea...... Naona amekosa mkasi tu kukata ribbon ya uzinduzi!!!

  Tanzania tuanze kulipwa kwa masaa!!! Mtu uki clock-out ndani ya masaa ya kazi unaenda unpaid.
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Mwanangu wazo zuri sana. Ni feasible kwa Tanzania?
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hapo cha kilichotiliwa mkazo kwenye hizo sherehe sio kutolewa kwa hiyo leseni, bali ni "mtu" anayepewa leseni.

  Mimi nimefurahi thou..wacha wafungue makampuni ya simu lukuki, washindane weee sie walala hoi tutanufaika na gharama nafuu za kupiga simu.

  Ila I wish kama wangekuwa wanatumia minara ya kurusha mawimbi ya simu kwa kushirikiana, badala ya kila kampuni kujenga minara yake.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 22.11.2008 0003 EAT

  • Kampuni mbili mpya za simu za mkononi zaingia

  Na Eben-Ezery Mende
  Majira

  KAMPUNI mbili mpya za simu za mkononi zimepewa leseni kwa ajili ya kutoa huduma hizo na kuungana na nyingine kubwa nne zilizopo hivi sasa.

  Zilizopewa leseni hizo jana na Mkurugenzi wa Mamlaka Mawasiliano nchini (TCRA), Profesa John Nkoma, ni Mycell na Egotel.

  Pamoja na kampuni hizo, kampuni nyingine ya Zain ilipewa leseni ya kutoa huduma zake kimataifa baada ya kuwa na leseni ya huduma za ndani tangu mwaka jana.

  Akikabidhi leseni hizo Dar es Salaam Profesa Nkoma alisema Zain imefikia hatua hiyo ya kuingia katika ushindani wa kimataifa baada ya kujiimarisha kimasoko.

  Alisema kuwapo na ongezeko la kampuni za mawasiliano kumeongeza ushindani wa kibiashara na utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa leseni hiyo, Mkurugenzi wa Mycell, Bw. Yusuf Manji ambaye pia ni Mkurugenzi Mrendaji wa kampuni ya Quality Group, alisema kampuni yake imejizatiti kutoa huduma ya mawasiliano kwa kiwango bora kinachokubalika katika tasnia ya mawasiliano.

  Naye Mkurugenzi wa Egotel, Bw. Mohamedi Ali, alisema soko la ushindani la mawasiliano ni kubwa nchini, lakini bado linahitaji uwezo mkubwa wa huduma hiyo.

  Kampuni zingine zinzotoa husuma hiyo ya simu za mkononi ni pamoja na Tigo, Vodacom na Zantel.


  [​IMG]
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA),
  Profesa John Nkoma (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi
  wa Kampuni mpya ya simu ya Mycell, Bw. Yusuph Manji
  leseni ya biashara katika hafla iliyofanyika, Dar es
  Salaam jana. Anayeshuhudia ni Ofisa Mawasiliano wa
  TCRA, Bw. Victor Nkya. (Picha na Charles Lucas)
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Manji kweli kiboko mpaka anafungua kampuni ya simu?
  Au wapo share na vibopa wa serikalini?Ngoja tusubili tutapata news.
   
 8. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Hivi Wakulu,

  Hawa TALK TELL toka wamepewa licence hamna jipya hata hawajafunga switch board.
  Kuna jamaa aliniambia kwamba ni matapeli hawa,hasa kwa wale suppliers vilaza mnawahonga ili kuingizwa kwenye list ya suppliers wao, alafu wao wanajilipa posho na kulipia pango pale quality plaza.
  Kila siku hadithi kazi hazianzi,sasa wanasingizia matatizo ya kiuchumi ya Ulaya na America
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  sasa hapo manji na mengi nani mzalendo
   
 10. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wacha wajenge na minara kila mtu ya kwake maana wanaongeza ajira kwa mgambo wa kulinda.
   
 11. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Eti nasikia Biashara ya simu ndio pekee yenye profit 1000% kwa kushirikiana na wakulu??? naomba nielimishwe kidogo
   
 12. K

  Kwayus Member

  #12
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni Vema kabisa Kuongeza Ushindani katika Sekta ya Mawasilino ili Huu Unyonyaji Uishe Je Watakuja na Staili gani ya Matumizi yasiwe ya haya ya Kuiga kama Voda kuiga CHIZIKA.Kumbe lengo lao ni Kukusanya tuu Vijsentvya wabongo na Kishia Kutoa kwa Siku Moja.Niafadhali wangetoa tujue moja hamna CHIZIKA
   
 13. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Minara haina deal tena, mwakani tutakuwa tunazungumzia fibre optic cable panapo majaliwa
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  kenge tuu hawa, wakaanzishe miradi endelevu ya kuondoa umaskini vijijini...upuuzi mputu!!
   
 15. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Muhimu watu kujua kuwa maana taa hafla ni sehemu yamatangazo. Matangazo huwa muhimu sana kupata ideas za stakeholders kwenye hiyo biashara. Ndiyo maana kukabidhiana kama biashara ni kubwa ni muhimu sana kuweka hafla.
  Kuna issue kama Kenya kutangaza alhamisi ya week ile kuwa sikukuu ya Kitaifa. Wahuni wengi walishangaa sana na kutoelewa. Issue hapa ilikuwa ni kuitangza nchi kimataifa. Vyomba vingi vya habari viliweka habari hiyo kama main news! Hata wale wanaojifanya hawajui Africa sasa walijua. Na kwa kweli ilikuwa very effective maana hata hapa jamaa wanatuuiliza maswali mengi sana kuhusu Africa sasa kuliko wakati mwingine.....

  It is about business. Naona watu wana Kama stevB na Mama wenyewe hawako kabisa Duniani!
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,764
  Trophy Points: 280
  sasa hapo manji na mengi nani mzalendo

  MANGI!!ULIKUWA HUJUI
   
 17. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mukulu,hii FIBRE OPTIC CABLE ni kitu gani unaweza kulete msaada hapa kwa sisi tusio jua tafadhali.
   
 18. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nilishawahi kulifikiria hilo wazo before mkuu, kumbe siko pekeyangu. Zile Lunch zoote za saa sita mpaka saa nane mchana wakati huo huo ulikuwa na breki fupi ya supu asubuhi, halafu ikifika saa tisa na nusu huyooo kibegi kwapani siku imekwisha huu mchezo wa kizembe na ufe......
  Lakini hold on, utakuja kushtukia watu hawapo kazini halafu mtu ame-clock masaa 70 kwa wiki, hayo yanawezekana pia.....
   
 19. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu ukienda kuuliza kule kwenye 'saa ya hansi na teke linalokujia' utapata tu ma-nerd watakaokuchambulia ni cable ya aina gani. For the time being jielimishe hapa kwanza.
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  mimi sina tatizo na kuja kampuni zaidi za simu, tatizo ni pale miradi kama hii inapo tumika kusafishia fedha chafu( yaani zile hela ambazo hazikupatikana kwa njia halali)
   
Loading...