Kampuni 4 za mafuta zapewa masaa 24. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni 4 za mafuta zapewa masaa 24.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jaguar, Aug 9, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kampuni za OILCOM,CAMELOIL,BP na ENGEN zimepewa masaa 24 kusitisha mgomo wao na kuanza kuuza mafuta kwa bei rasmi iliyotangazwa na Ewura.Endapo watakaidi amri,Ewura imetishia kuziburuza mahakamani.Wakati huo huo mheshimiwa Zito Kabwe ameshauri endapo kampuni hizi zitaendeleza mgomo,JWTZ iingilie kati kwa kuvamia vituo vya mafuta kinguvu na kuuza mafuta kwa wananchi.
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Sometime when diplomatic means doesn't work, use devil's altenative!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,549
  Likes Received: 5,757
  Trophy Points: 280
  Takataka tu ewura ni uchafu wa kupitisha hela za kikwete na michango ya chama cha mapinduzi katika taakataka nisiotaka kuwasikia ni ewura na tanesco kama una uwezo unatangaza sudden death viende zao vikafie mbali kabisa
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,136
  Likes Received: 7,384
  Trophy Points: 280
  Serikali iekeze ukweli,
  Haiwezekani wauzaji mafuta wakagoma bila sababu,
  Serikali inabidi ikae nao katika mjadala wa wazi wachambue kipengele kimoja baada ya kingine katika vile ambavyo wafanyabiashara wanavilalamikia, itaonekana tu mbivu na mbichi ni zipi.
  Kutishiana na kutunishiana misuli hakusaidii, bali ni kuzidi kumuumiza mteja,
  Wafanyabiashara wanaweza kukubali kufuata bei za Ewura, but kama kweli watapata hasara hatujui wataifidia vipi,
  Wanaweza kupunguza wafanyakazi, kuchakachua mafuta, kufunga biashara n.k.
  Ubabe hausaidii katika hili
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  hii inapendeza.........
   
 6. L

  Listener92 Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora wafutiwe vibali tujue moja. This is a mixed economy, when free market economy fails, command economy should take lead. Hatuwezi kuendeshwa na kikundi cha watu tu wanaokaa chini na kusema tugome. Bora serikali iingilie kati tupate mafuta.
   
 7. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyo meya wa Dar aliyesema wabunge (serikali) wanatumia makalio kufikiria hakukosea, ina maana Tanzania ni Dar peke yake?, hivyo vituo vilivyotajwa hapo vingi vipo Dar, je wamefikiria na hivi vilivyopo mikoani? Total, Oryx, n.k, kwa sababu hata wao wamegoma, au wa mikoani tuje tujazie mafuta Dar?, mipuuzi sana hii mijitu
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  na huyo aliyeshauri JWTZ wavamie vituo na kuuza mafuta kwa nguvu nadhani sijamuelewa vizuri (masaburi anahusika hapo)!

  Mungu yupo!
   
 9. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nahisi ni kwa kalio moja tu!
  Maana kuna GBP,GAPCO,KIPENDA ROHO,NJAKI!
   
 10. g

  godbiy Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Hata mie nimeshangaa eti wametaja vituo vinne pekee.Katika pitapita yangu leo Karibu vituo vingine vyote navyo vimefungwa. kama Oryx,Total,Gapco n.k Lakini wenyewe wameona tu hivyo...
  Tetesi zinasema kwamba Oil market companies wanaelekea dodoma kwa mazungumzo zaidi.Ila ni kweli hakuna aja ya kutumia ubabe.kuna tatizo la msingi ambalo sidhani kama wananchi tumelezwa.

  Kimsingi,kama serikali ilitakiwa kuwa na "National Reserve" yake ya mafuta hii ndiyo kinga kwa wakati wa dharulakama huu.Kama serikali inategemea wafanya biashara ndiyo waagize pekee yao hii hatari kwa uchumi na usalama wa nchi.Fikiria nchi iingie kwenye vita(ambacho hatutegemei) ,nchi itakuwa kwenye wakati mgumu sana.

  Angalia Zambia wanapitishia mafuta kupitia kwetu hapa lakini wana national reserve yao ya kutunza mafuta mpaka mwezi.hili linabidi liwe fundisho kwa watawala.Tuche siasa
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sikubaliani na Zitto hiyo ni temporary soln, kifupi serikali ijipange nayo kupitia kampuni yake tuone nini kitatokea.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wazo la zito ndio ,muendelezo wa kufikiria kwa MAKAL!o
   
 13. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mnyika kaongea vizuri sana bungeni, serikali inamiliki 50% za share BP, hii jeuri ya wao kugoma wameipata wapi? na serikali imenyamaza kimya, hapa tunapigwa changa la macho. Tunaposema Ewura iwanyang'anye leseni wamiliki wa vituo hivyo, mbona ndio hao hao mabosi wa Ewura,TRA na mafisadi ndio wenye vituo vya mafuta? watajinyang'anyaje leseni? Tushtuke jamani, bila nguvu ya umma hapa tutazidi kulialia kila siku
   
 14. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  wewe unafikiri hali hii ikizidi nini iwe solution?
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Serikali na ewura wao wanacheza mchezo mmoja,ambao ni kupeana saa 24
   
 16. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  &lt;br /&gt;<br />
  &lt;br /&gt;<br />
  Upumbavu huo! Serikali ilishajitoa kwenye biashara, kwa nini iwashinikize wafanya biashara kuuza kwa hasara. Kwa nini serikali isifanye biashara ya mafuta kama ina faida?
   
 17. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Makosa makubwa ylifanyika kwa serikali kuanzisha wakala wanaotegemea wafanyabiashara kwa malipo ya kujiendelesha. Bila makampuni ya mafuta, gesi na maji EWURA haitajiendesha na itakufa. Kwa maneno mengine EWURA inategemea mkampuni hayo 100% ili iwepo, na tusitegemee kamwe kwa hali ilvyo EWURA iweze kudhibiti makampuni ya mafuta.
  Serikali inaanzisha wakala kuongeza urasimu, kuzidi kuwanyonya wananchi na bahati mbaya sana ni njia ya kuwanufaisha au kuwatafutia vitengo vya kujipatia kipato zaidi baadhi ya watu na kuwaongezea mzigo wananchi wa kawaida.
  Kuna haja kabisa ya serkali kuangalia upya utendaji wa wakala wa serikali na mapato ya wakala hao ili yasitegemee moja kwa moja wafanyabiashara wanaodhibitiwa kisheria na wakala husika.
  Ingekuwa pia vizuri zaidi kwa tozo za taasisi mbalimbali zikajumuishwa kwenye kodi na baadye kurejeshewa na TRA ili kuondoa uduni au utegemezi wa taasisi hizo kwa wafanyabiashara au makampuni ya kibiashara.
  Haiwezekani leo utoe adhabu kwa mkosaji halafu kesho uende kuomba malipo ya kutoa huduma ya adhabu!
  Wakati mwingine unaweza kupata hasira ukaongea kama Masaburi pamoja na kwamba yeye ni mmojawapo wa watuhumiwa!
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na hoja nzito ya Comrade Zitto Kabwe!
   
 19. M

  Mwera JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli nikwamba hapo hata serikali ina makosa,ilipotoa bei mpya ilikurupuka,wamepunguza sh100 yakodi katika diesel tu mafuta yataa na petrol hawakutoa punguzololote,nawaliposhusha bei wakashusha kwamafuta yote,nawakati huohuo walishatozakodi zote ktk mafutayote badae wakashushabeì,huo ndio ukweli halisi,tusiwalaumu wauza mafuta peke yao tuangalie naupande wapili washilingi,je wewe umenunua kitu kwa sh 1000 kwamfano badae unalazimishwa ukiuze 700 namtajiwako wote umewekezahapo je utakubali kujifilisi mwenyewe?? Si bora ufungie maliyako stoo mpaka mambo yakae sawa,serikali nayo inastahili lawana,tuwe wakweli japokua tunaumia.
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  JWTZ ya nini? Nguvu ya umma yatosha!
   
Loading...