Serikali legelege ....yapewe masaa 24 ijieleze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali legelege ....yapewe masaa 24 ijieleze

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MWananyati, Aug 6, 2011.

1. M

MWananyati Senior Member

#1
Aug 6, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 154
Likes Received: 12
Trophy Points: 35
Ama kweli sasa ndo utajua kama tumeshauzwa na kuwa serikali yetu inamilikiwa na watu ambao inawaita 'wawekezaji'. Jamaa hawa wamefikia hatua hata ya kuitusi na kuitishia hadharani Serikali kwa sababu ya nguvu waliyonayo (wanapata wapi hio nguvu??). Nyerere alikua akiwatimua watu kama hawa ndani ya masaa 24, lakini serikali ya saiv inagombezwa na ipo kimyaaaa, au kwa kuwa tunaenda kuomba misaada kwao then wanakwambia utaombaje msaada wakati kuna watu wamehifadhi ma-trilioni ya kifisadi benki za nje?

Hebu angalieni hapa: Source Tanzania daima 6/8
[TABLE]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
[TR]
[TD]
Engen imeidhalilisha serikali kuipa saa 24
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE]
[TR]
[TD]WIKI hii vyombo mbalimbali vya habari vilitawaliwa na habari za wamiliki wa vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam kuamua kwa makusudi kufunga vituo vyao kwa madai ya kuishiwa mafuta.
Katika sakata hilo ambalo lilisababisha tafrani kubwa kwa wakazi wa jiji hili kutokana na kushindwa kupata bidhaa hiyo huku vituo vichache vikiuza kwa bei kubwa na si zaidi ya lita tatu.
Vituo hivyo ambavyo vilikuwa na msongamano mrefu wa magari huku baadhi ya watumishi wakilazimika kugombana na wale waliofika na vidumu kwa kuhitaji kujaziwa mafuta kutokana na magari yao kuzima kutokana na kukosa mafuta.
Hatua hiyo ilisababisha Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), pamoja na makampuni zaidi ya 14 yanayoagiza mafuta nchini kukutana ili kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo.
Makampuni hayo yalikuwa hayakubaliani na bei elekezi iliyotangazwa na Serikali ya kushusha kwa bei za mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa.
Katika mkutano huo ambao ulihitimishwa juzi ilionyesha wazi kuwa makubaliano yaliyofanyika hayakuafikiwa na makampuni hayo.
Hilo linatokana na kauli iliyotolewa na mkurugenzi wa Kampuni ya Engen ambaye ni mwenyekiti wa chama cha makampuni yanayoagiza mafuta ya kuamua kuipa Serikali saa 24 ya kuangalia namna ya kufidia hasara watakayoipata pindi wakiuza mafuta kwa bei hiyo elekezi.
Mwekezaji Selan Naidoo ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo kutoka nchini Afrika Kusini alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kampuni yake ilifika nchini kwa ajili ya kutengeneza faida na si kupata hasara.
Anasema kuwa kama Serikali itashindwa kutafuta njia ya kudhibiti hasara hiyo basi kampuni yake italazimika kuachana na biashara hiyo na kuondoka nchini.
Sisi Tanzania Daima tumesikitishwa na kauli hiyo ambayo imeonyesha kwa kiasi kikubwa kuwa mwekezaji huyo hana uzalendo na serikali wala wananchi wa Tanzania.
Tunaamini kuwa kauli ni sawa na kueleza kuwa mwekezaji huyo ameiweka Serikali mfukoni kutokana na kuipa saa 24 jambo ambalo tunajua kuwa yenye uwezo wa kutoa kauli kama hiyo ni serikali pekee na si mwekezaji.
Kauli hiyo inatukumbusha katika kipindi cha utawala wa awamu ya kwanza wa Hayati Julius Nyerere ambapo Mgiriki mmoja aliitusi serikali ya Nyerere na kudai kuwa ameiweka mfukoni.
Kitendo cha Mgiriki huyo kutoa kauli hiyo kilimfanya Mwalimu Nyerere kuchukua uamuzi wa haraka na kumpa saa 24 kutakiwa kuondoka nchini kitendo kilichoonekana ni cha kishujaa kwa uongozi wa Mwalimu.
Hivyo tunaona kuwa kauli aliyotoa mwekezaji wa Engen kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete ni ya udhalilishaji tena ni kashfa kwa serikali iwapo itaamua kumwacha aendelee na biashara yake.
Tunajua kuwa hatua ya mwekezaji huyo ni kuonyesha vitisho kwa serikali akijua au kufikiria kuwa ni legelege ambayo itakubaliana na hatua ya kuangalia hasara itakayopata kampuni yake kwa vile amefika kwa ajili ya faida.
Sisi Tanzania Daima tunaiomba serikali iwadhibiti wawekezaji kama hawa maana iko siku watafikia hatua ya kushawishi na makampuni mengine kuweza kutoa kauli kama hizo ambazo zinatoa taswira mbaya kwa nchi na hata serikali kuonekana haina mamlaka juu yao.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

2. F

FJM JF-Expert Member

#2
Aug 6, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
Kabla hata serikali haijajibu (kama itajibu) nadhani WATANZANIA wote bila kujali tofauti zetu tungesusia kabisa kabisa kununua mafuta kwa hawa ENGEN. Huu ni udhalilishwaji wa hali ya juu.

Wakati mwingine consumer power inaweza kuleta mabadiliko kama ilivyotekea wa Rupert Mudorch na News of the World.Tuhamasishane watanzania wote hakuna kusogelea kutuo cha ENGEN.

3. Tangawizi

Tangawizi JF-Expert Member

#3
Aug 6, 2011
Joined: Jun 25, 2009
Messages: 2,835
Likes Received: 927
Trophy Points: 280
Guys,
Is it true that Engen gave the government 24 hours to revise their pricing template or oil industry through TAOMC (Tanzania Association of OIl Marketing Companies said that? I heard Engen's MD is the current chairman of the association and the views of the association should not be taken as the view of Engen alon, vinginevyo kauli kama hiyo inakuwa siyo ya haki. Inasemekana kwenye hii statement kuna chumvi inaongezwa ili maandiko yatimie, lol!
Upande mwingine, kuna mtu anajua namna ya price ya mafuta inavyofanywa na components zake? i mean price build up because Ewura's changed template has caused all these problems. Kuifahamu kutasaidia kutoa hukumu ya haki kuliko kukimbilia kuhukumu based on the information from media ambazo zinaweza pia zikawa sio sahihi sana.

4. Nyambala

Nyambala JF-Expert Member

#4
Aug 6, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 4,470
Likes Received: 21
Trophy Points: 135
Kabla ya kwenda huko tungeanza kwanza kususia huduma za vodacom ya Rostam!!!!!

5. Michael Scofield

Michael Scofield JF-Expert Member

#5
Aug 6, 2011
Joined: Jul 30, 2011
Messages: 1,218
Likes Received: 5
Trophy Points: 135
Hapa si mtalii wala anaejifanya mtoto wa mkulima, anaeweza kuinua mdomo na kulikemea hilo. Wao wamekalia kuvuana magamba, nchi tayari ina wenyewe.

6. Shark

Shark JF-Expert Member

#6
Aug 6, 2011
Joined: Jan 25, 2010
Messages: 20,059
Likes Received: 7,279
Trophy Points: 280
Tuacheni ushabiki usio na maana, muwekezaji huyu bwana seelan naidoo namjua vizuri tu, na jana tumeongea kwa kirefu tu juu ya hili sakata.
Alichodai ni kua EWURA ndio waliotoa saa 24 kwa wawekezaji kukubaliana na bei ya EWURA lasivyo watanyang'nywa leseni, nae akajibu hayo masaa 24 yafike tu wachukue hiyo leseni afunge biashara kuliko afanye biashara ya hasara.
Tuna tatizo waandishi kutokujua kiengereza, ila kwa swala hili tusimhukumu bwana Seelan Naidoo,
Ikumbukwe pia alikua akiongea kama Mwenyeketi wa TAOMAC na sio Mkurugenzi wa ENGEN,
Mbona mwenzie Bw. Salum Bisarara hasakamwi?

7. Tanganyika1

Tanganyika1 JF-Expert Member

#7
Aug 6, 2011
Joined: May 10, 2011
Messages: 396
Likes Received: 27
Trophy Points: 45

8. Tanganyika1

Tanganyika1 JF-Expert Member

#8
Aug 6, 2011
Joined: May 10, 2011
Messages: 396
Likes Received: 27
Trophy Points: 45

9. Shark

Shark JF-Expert Member

#9
Aug 6, 2011
Joined: Jan 25, 2010
Messages: 20,059
Likes Received: 7,279
Trophy Points: 280
Seelan ni mwenyekiti wa TAOMAC ambayo Bisarara ni Mkurugenzi wake,
Serikali ilipunguza kodi yake kwa karibia Tshs 100 lakini hapohapo inataka Makampuni ya ya mafuta yapunguze bei yake kwa Tshs 200, hii inakujaje?
Sumatra inaopewaga stock available ya kila kampuni karibia kila wiki, TRA wanajua kiasi cha mafuta makampuni wanachoingiza, wanashindwaje kukokotoa stock available wakawaachia waimalizie kwa old (higher) price kisha ndo waanze kutumia new price (lower)?
Mfano dhahiri leo Jumamosi kuna kampuni nafikiri ni hao hao Engen walikua wapokee Mafuta bandarini, lakini kutokana TPA kuendelea ku-charge higher/old rate (wakati tunadanganywa zimeshuka) imebidi meli isishushe mzigo na kuamua kugeuza, Huku ni kufanyana watoto

10. FaizaFoxy

FaizaFoxy JF-Expert Member

#10
Aug 6, 2011
Joined: Apr 13, 2011
Messages: 58,102
Likes Received: 22,141
Trophy Points: 280
Mnaijuwa biashara au mko hapa kuponda tu kila kitu?

Muandishi kasema hivi: "kauli iliyotolewa na mkurugenzi wa Kampuni ya Engen ambaye ni mwenyekiti wa chama cha makampuni yanayoagiza mafuta ya kuamua kuipa Serikali saa 24 ya kuangalia namna ya kufidia hasara watakayoipata pindi wakiuza mafuta kwa bei hiyo elekezi."

Hiyo ni kauli ya muandishi na hamna quotation mark hata moja. Kwa hiyo hatujui context ya aliyoyasema. Tusikurupuke.

Kwani kuna mfanya biashara yupi? awe Mtanzania au mgeni ambae anataka hasara?

Ni kawaida kabisa kwa mfanya biashra kuiambia Serikali namna itavyofidia hasara watakayoipata wakipunguza bei itafidiwa vipi? Tena bora hao wametoa saa 24, kawaida mpo mezani mna discuss inatakiwa majibu yawepo hapo hapo.

Wacheni zenu hizo. Hamjui hata maana ya biashara? mnanshangaza!

11. Safety last

Safety last JF-Expert Member

#11
Aug 6, 2011
Joined: Mar 24, 2011
Messages: 4,224
Likes Received: 164
Trophy Points: 160

futari ya nguruwe !

12. t

tusichoke JF-Expert Member

#12
Aug 6, 2011
Joined: Apr 2, 2011
Messages: 1,286
Likes Received: 8
Trophy Points: 135

Ndugu yangu kumbuka ili uwe muwekezaji kwa chochote tanzania ni lazima ule na mafisadi,bahati mbaya mafisadi hao ni viongozi hivyo tusitegemee lolote hapo,wataendelea kutukamua tu kwani kauli za punguzo la bei wanatuzuga tu

13. Tuyuku

Tuyuku JF-Expert Member

#13
Aug 6, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 3,149
Likes Received: 1,405
Trophy Points: 280
jamani pamoja na kuwa nami ni muathirika wa moja kwa moja wa ukosefu wa mafuta naomba niwatetee wafanyabiashara wa mafuta. Sote tunajua vitu gani vimepelekea mafuta kupanda bei pamoja na bidhaa zingine. Serikali inakwepa wajibu wake makusudi na kuamua kuwatwisha mzigo waagizaji wa mafuta. Ni mfanyabiashara gani anapenda kufanya biashara kwa hasara? Serikali isiwalazimishe wafanyabiashara kubeba mzigo usiokuwa wao wakati viongozi wanauyumbisha uchumi wa nchi. Kama shilingi haipo stable kwa nini mafuta yasipande bei?

Loading...