Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 782
- 1,831
“Ukitumia mitandao vibaya sheria ipo na mamlaka na vyombo vipo vitakupata, sasa wakati mwingine unaona vikampeni havina mbele wala nyuma nikisema mnasema Msigwa ametusemea maneno makali, lakini ninachosema ni kwamba vijana tutumie mitandao kwa njia za kimanufaa kwasababu ukifanya makosa tutakupata…
Sheria inakataza kutukana, sheria inakataza kuzua taharuki, sheria inakataza kudhalilisha na tumeshaanza kuona kwenye mitandao watu wanafanya makosa haya sasa naomba niwaambie vijana hakuna anayefanya makosa haya akabaki salama tutawakamata tuu…
Soma Pia: Msigwa: Mihemko imekuwa mingi, uhamasishaji wa kijinga Mitandaoni umekuwa mwingi, Vijana mjitazame
Ukifanya makosa ya mtandao haya niliyosema tukikupata iwe unajua au hujui sheria itafuata mkondo wake na ukithibitika na mahakama kwamba kweli umefanya hayo utapigwa faini ya shilingi Mil. 5 au zaidi au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja.” Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano maalum alioufanya Jijini Dodoma June 11, 2025