Kampeni ya kuikataa Vodacom

Voda ndio vinara, mwaka huu tu kwa taarifa yao wenyewe kwa msukumo wa dola wamedukua simu za wateja wake mara 1000! Shame on them and you too.
 
Sidhani kama ni voda tu, mitandao yote kwa sasa imeunganishwa kwa ajili ya usalama,na ukitoka toka kimya kimya sio mpaka sisi huku tujue,Me binafsi natumia voda na nitaendelea kutumia kama kawaida na daima tusikubali kuongozwa na hisia fulani,fikiria kabla ya kutenda
 
Voda ndio mtandao namba moja Tanzania acheni kudanganyana nyie vijana.
Sheria inawalazimisha mtandao wowote kuingilia mawasiliano ya mteja kama yanatia shaka kiusalama popote mtapokimbilia mtanyooshwa kama mnaleta upumbavu.
 
Nilisha wakimbia siku nyingi
 
Voda ya nini sasa! Kwenye vifurushi hawafai na kila sekta hawafai. Me shavunja line kwa ghadhabu kitambo sana.
 
Kwa kitendo chenu cha kudukua mawasiliano ya akna Membe mmejitia KITANZI wenyewe . Watu maelfu wanaendelea kuwaacha, hamfai na mko hovyo.Mimi nimeshaweka chip yenu pembeni.
 
Kwanza hii ni kampuni ya chama kama alivyosema Cyprian Musiba. Hivyo inafanya kazi za chama kwa maelekezo ya Mwenyekiti.
 
Mpaka juzi nineshaitupa laini mkr wangu pia nimemshawishi naye kaitupa, hawataona jata senti moja kutumika kupitia laini zangu kule vijijini najipanga kuwashawishi wazazi.na ndugu zangu nao wazitupilie mbali.
 
Umejuaje kama ni voda?
Kwa kitendo chenu cha kudukua mawasiliano ya akna Membe mmejitia KITANZI wenyewe . Watu maelfu wanaendelea kuwaacha, hamfai na mko hovyo.Mimi nimeshaweka chip yenu pembeni.
 
TCRA ile huduma ya kuhama mtandao na namba yako kama ilivyo sasa ndio wakati wake
 
Im in, nafkiri voda haipo kwa ajili ya watanzania wa kawaida iko kwa ajili ya watu wenye fedha zao. Vodacom Tanzania nawafananisha na DSTV endeleeni kuwauzia matajiri vifurushi vyenu laini yenu nshatupa.
 
Watanzania wanashangaza sana.

Vodacom inamilikiwa na Ccm kama mwanahisa, kwa hali yoyote, Vodacom haiwezi kukubali mmiliki wake ahenyeshwe wakati wanaweza kutoa taarifa kwa chama kuhusu mambo mbalimbali yanayofanyika kupitia mtandao wa vodacom yanayokidhuru chama.

Binafsi nawapongeza vodacom kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa chama tawala.

Wale wenye nongwa, kuna mitandao mingine wala hamjalazimishwa kubaki vodacom, nendeni mjiunge na mitandao ya mabeberu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…