Kampeni meneja na Mbunge wa Chadema washikiliwa na polisi Igunga

Hivi vitu vya kawaida tu mkuu katika mapambano. Msilegeze chochote endeleeni kupamabana maana kama mtaikomboa Igunga basi hakuna kitu cha kuwazuia tena!

Tunawatakia kila la heri na hao wapiganaji watarejea Jtatu ngoja wakapate na siri zingine huko walikowapeleka.
 
huko kuatmu ssa..................yale yale ya kupigwa na kukamatwa lakini mwisho wa siku sisiem hatuna chetu
 
Leo asubuhi zaidi ya polisi 50 walimshika Kampeni meneja ambaye pia ni Mbunge wa Maswa mashariki,mh Kasalamboi pamoja na mbunge wa viti maalum Suzan Kiwanga, baada ya kuwashikilia kwa muda na kutoa maelezo kwenye kituo cha polisi hapa Igunga.

Wanatuhumiwa kumpiga DC wa Igunga, baada ya kuandika maelezo wamewahamishia Tabora mjini, hadi Jumatatu watakapofikishwa mahakamani.

Hii ni ishara nyingine ya jeshi la polisi kutumiwa na CCM, DC aliingilia mkutano wa Chadema, tukaenda kushitaki, halafu Wabunge wetu ndio wanakamatwa,huu ni uhuni mkubwa.

Kamwe haturudi nyuma wala kukata tamaa, tutasonga mbele na kamwe haki haikuwahi kushindwa

Freedom is coming tomorrow.....for those who are dreaming on Tanzania which provides honey and milk,do not be discourage this is the good sign of freedom..and for sure haki uwa inacheleweshwa tu,lakini ipo na inakuja...Together we will stand...!!!
 
Tukio Igunga na kesi kwenda Tabora mjini ? Mh haya wacha tuone inakuwaje hapo .Lini watarudi kwa DC na kesi yao kuingilia mkutano wa Chadema ? Wacha tusikie watasemaje kwenye kampeni .
 
Nilisema kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawakutumia busara kuwaongoza vijana wenye jazba kwenda kumfanyia fujo DC kwani walikuwa wanawapa CCM nafasi ya kubadilisha suala la fujo hizo kuwa ajenda yao kuu ya kampeni Igunga. Na hilo litawaathiri CHADEMA watake wasitake kwani sasa kazi yao kubwa itakuwa ni kujitetea kuwa chama chao siyo cha vurugu badala ya kuuza sera za kuchaguliwa. Any way huo ni muono wangu tu tuangalie kitakachofuata.
 
Iko siku nchi itakombolewa na siku hiyo kutakuwepo na kilio na kusaga meno kwa wote wate walioshiriki kwa namna yeyote ile kutufikisha hapatulipo.mafuta ya taa sh 2000 sukari 2500,sembe 1000, umeme hakuna ,maji ndio usiseme ndoo sh 300.mnaacha kuangalia matatizo yetu mnahamia igunga siku ipo inakuja na wala haipo mbali. Halitasalia jiwe juu ya jiwe .
 
Dah! Inasikitisha.kumbe hata na wabunge wa CDM wanatumiaga masaburi kufikiria?.Nimepata jibu ktk tukio la kumshambulia DC kuwa hawafikirii kabla ya kutenda na wabunge hawa wameaibisha padre na CDM kwa ujumla.Walaaniwe kumshambulia DC!
<br />
<br />
Huo ndio ulinzi shirikishi
 
Kwanini Tabora? au ndio ya kumpereka Mbowe na Ndege ya Jeshi Arusha! Polisi Maskini akili kidogo matumbo makubwa.
 
Kazi ya ukombozi si rahisi, tupo nao tunawaunga mkono hiyo ni sehemu ya historia ya ukombozi ujao
 
Trust me ccm atamfanye njama za Gadaffi na Mubarak hii generation yetu haikubali tena. Time imefika kuwachapa viboko ccm ....
 
Tumekuwa tunahubiriwa kuwa cdm ni chama mbadala kwa ccm, ngoja tuone viongozi wake watafanya nini katika mazingira kama haya. Tuone ni jinsi gani nyie ni tofauti na hawa wa ccm ya leo.
 
Hata kama wamekamatwa na kuhamishiwa Tabora,ambapo nadhani huko ndiko watafikishwa mahakamani,lakini kwa mujibu wa sheria na kosa wanalodaiwa kutendwa-shambulio la aibu,hawapaswi kushitakiwa Tabora mjini isipokuwa Igunga.Na km polisi,kwa sababu ya jaziba wakawafikisha mahakamani huko Tabora mjini basi huo ni ushindi kwa CDM kwa kuwa mahakama hiyo haitakuwa na jurisdiction.Aidha kosa wanalodaiwa kutenda bado lina dhamana na mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kuthibitisha kama mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
 
Back
Top Bottom