Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu mikoa ya Singida, Tabora na Shinyanga

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
Wakuu bado tunaendelea kuwaletea taarifa za Mh Tundu Lissu kutoka popote anapopita kuomba kura.

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika.

Ratiba ya Mgombea Urais. ( 640 X 640 ).jpg

=========

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tundu Lissu, akiambatana na mkewe, Bi. Alicia Magabe, akimjulia hali Ndugu Wilfred Enock anayejulikana pia kwa jina la Chaijaba ambaye ni maarufu mjini Singida kutokana na kutembea na toroli la kubebea mizigo likiwa na bendera ya Chadema kila aendako. Ndugu Chaijaba alivamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali mwilini na watu ambao hadi sasa hawajakamatwa, waliokuwa wakimhoji sababu za mapenzi yake kwa Chadema.
IMG-20201012-WA0009.jpg
IMG-20201012-WA0008.jpg
IMG-20201012-WA0007.jpg
IMG-20201012-WA0005.jpg
IMG-20201012-WA0004.jpg

"Msafara wa Mheshimiwaa Tundu Lissu umesimamishwa na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Tumuli, wilayani Mkalama Mkoani Singida.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Tumuli amewakumbusha kuhusu umuhimu uchaguzi mkuu, miaka mitano ya Magufuli imekuwa ya shida na vurugu. Watu watekwa, wameuliwa, wamenyanyaswa, wamekosa mishahara na kudhulumiwa kila mahali. Mfano halisi mmeona kwangu nimepigwa risasi 16. Nchi imekuwa ikiogopeka nakila mtu sasahivi ni rahisi kumtaja Mungu kuliko kumtaja Magufuli. Ndomaana nasema uchaguzi mkuu huu ni muhimu, tukishindwa tumekwisha.

Na katika kuhakikisha yote haya yanakuwa sawa ndo maana Chadema ilani yetu inazungumza kuhusu Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Najua wote tunataka Uhuru, Haki na maendeleo. Kukiwa na haki hata Taifa huinuka. Basi mchague viongozi wa Chadema wasimamie nakutekeleza ilani ambayo kila mmoja itamgusa.

Ili yote haya tuyakomeshe tarehe 28 nawaomba wananchi wa Tumuli mjitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wa Chadema.

Mgombea udiwani wenu hapa Tumuli ni Haruna Khamis

Namgombea Mbunge Oscar Alex Kapalale
IMG-20201012-WA0017.jpg
IMG-20201012-WA0016.jpg
IMG-20201012-WA0015.jpg

Mapokezi na mkutano Igunga Uwanja wa barafu. Huyo aliyeshikana naye mkono ni Mgombea Ubunge wa Chadema Jimbo la Igunga, Ngasa Mboje. Wananchi walikuwa na bashasha na mapenzi makubwa, wakampokea Mgombea Urais kwa kusafisha, kudeki barabara na kuosha gari lake.
IMG-20201012-WA0037.jpg
IMG-20201012-WA0038.jpg
IMG-20201012-WA0039.jpg
IMG-20201012-WA0053.jpg
IMG-20201012-WA0052.jpg
IMG-20201012-WA0049.jpg
IMG-20201012-WA0040.jpg
IMG-20201012-WA0041.jpg

Wananchi wa Kahama wakiwa wamejipanga barabarani kumpokea Mgombea Urais Mh. Tundu Lissu eneo la Kagongwa.
IMG-20201012-WA0058.jpg
IMG-20201012-WA0056.jpg

*TUMULI*

"Msafara wa Mheshimiwaa Tundu Lissu umesimamishwa na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Tumuli, wilayani Mkalama Mkoani Singida.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Tumuli amewakumbusha kuhusu umuhimu uchaguzi mkuu, miaka mitano ya Magufuli imekuwa ya shida na vurugu. Watu watekwa, wameuliwa, wamenyanyaswa, wamekosa mishahara na kudhulumiwa kila mahali. Mfano halisi mmeona kwangu nimepigwa risasi 16. Nchi imekuwa ikiogopeka nakila mtu sasahivi ni rahisi kumtaja Mungu kuliko kumtaja Magufuli. Ndomaana nasema uchaguzi mkuu huu ni muhimu, tukishindwa tumekwisha.

Na katika kuhakikisha yote haya yanakuwa sawa ndo maana Chadema ilani yetu inazungumza kuhusu Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Najua wote tunataka Uhuru, Haki na maendeleo. Kukiwa na haki hata Taifa huinuka. Basi mchague viongozi wa Chadema wasimamie nakutekeleza ilani ambayo kila mmoja itamgusa.

Ili yote haya tuyakomeshe tarehe 28 nawaomba wananchi wa Tumuli mjitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wa Chadema.

Mgombea udiwani wenu hapa Tumuli ni *Haruna Khamis*

Namgombea Mbunge *Oscar Alex Kapalale

=====

IRAMBA

"Mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Mheshimiwa Tundu Lissu Wilayani Iramba, katika kata ya Kiomboi, Mkoania Singida.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Kiomboi Iramba amewasalimu nakuwaambia kuwa anafahamu kilichotokea hapa, katika kata 20 wagombea wote wameenguliwa na Tume ya uchaguzi ambayo ni tume ya CCM. Aliyebaki ni Mbunge pekee tena baada ya rufaa. Ilikuwa sio ajabu tusiwe na mgombea hata mmoja kwasababu ya mapenzi ya tume ya CCM.

CCM na mwenyekiti wake na Mgombea wao ndo adui namba moja wa nchi hii. MaCCM ndo wameteka wananchi bila sababu wameua Wananchi wasio na hatia. Wakaendelea kuwafilisi wafanyabiashara na hata kuminya uhuru wa watu na vyombo vya habari.

Hii serikali ya CCM ikaendelea kuwauzia watu vitambulisho vya ujasiriamali ambavyo havina picha wala jina tena wamewalazimisha nchi kuvinunua, Chadema tulipoanza kuhoji uhalali Magufuli akasema vitambulisho sio lazima, wakati walishavitungia sheria chini ya wizara ya fedha na wakaweka kwenye Ilani yao ya uchaguzi wakimaanisha kuwa bado wataendelea kuwaibia wananchi.

Magufuli na serikali yake imewaumiza hadi Mapolisi wetu, miaka mitano bila nyongeza ya mishahara wala kupanda vyeo.

Sasa kama tuliwachagua wenyewe kwa kura basi tunaweza kuwaondoa Sisi wenyewe kwa kura, tutumie uchaguzi mkuu huu kuwaondoa hawa watu. Watu wa Iramba mkipiga kura ya haki tutapata haki, nawaombeni mpige kura ya haki kuchagua viongozi watakaosimamia haki. Tarehe 28 tupige kura ya haki ili tumuondoe Magufuli. Tupige kura ya haki tutibu Watu walioumizwa, tufungue milango ya magereza kwa waliofungwa bila hatia, tupige kura ya haki kukataa uonevu wa kila hali. Siku zote haki uinua taifa, basi chagueni haki ili taifa liinuke.

Nawapa Ujumbe : Mwambieni Mwigulu Kuwa afanye kampeni zake kiustaarabu.

Mwisho watu wa Iramba naomba mchagueni Mbunge wenu Jesca Kishoa.'

Ahsanteni sana Iramba.

=====

IGUNGA

"Maelfu ya Wananchi wamejitokeza kwenye mkutano wa kampeni za Mheshimiwa Tundu Lissu katika viwanja vya Barafu Wilayani Igunga, Mkoani Tabora.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Igunga amewashukuru kwa mapokezi makubwa.

Kwenye Uchaguzi mkuu naomba muanze na madiwani wote waliosimamishwa na Chadema. Wagombea wetu 13 Kati ya 16, hawahawa tukiwachagua wanatosha kuchukua halmashauri nakushugulikia kero zote za wafanyabiashara. Kura ya pili ni Kwa Mbunge Bwana Ngassa Ganja Mboje. Nakura ya tatu hapo ndo pakukazia kati yangu Tundu Lissu na jiwe, sasa watu wa Igunga mnapigiaje kura jiwe. Mnapigiaje kura mtu aliyekura hadi rambirambi, mtu ameomba asuguliwe sasa unampaje kura.

Miaka mitano yauonevu mkubwa, miaka mitano ya maumivu kwa wakulima, miaka mitano ya kesi zauongo. CCM ndo wameteka wananchi bila sababu wameua Wananchi wasio na hatia. Wakaendelea kuwafilisi wafanyabiashara na hata kuminya uhuru wa watu na vyombo vya habari.

Watu wa Igunga ngoja niwaambie kuhusu hivi vitambulisho vya Magufuli (ujasiriamali) ambavyo havina picha wala jina tena wamewalazimisha nchi nzima kuvinunua, wanaviuza bila risiti. Chadema tulipoanza kuhoji uhalali Magufuli akasema vitambulisho sio lazima, wakati walishavitungia sheria chini ya wizara ya fedha na wakaweka kwenye Ilani yao ya uchaguzi wakimaanisha kuwa bado wataendelea kuwaibia wananchi.
Sasa tangu lini raisi akafanya biashara au mkurugenzi akafanya biashara. Sasa ukiona hiyo misafara ya rundo la magari ni hizo pesa za vitambulisho ndo anafanyia kampeni.

Magufuli na serikali yake imewaumiza hadi Mapolisi wetu, miaka mitano bila nyongeza ya mishahara wala kupanda vyeo.

Sisi Chadema kwenye Ilani yetu imezungumzia kuhusu Uhuru, haki na maendeleo ya watu. Tunaposema maendeleo ya watu sio uwanja wa ndege wa Chato na Mandege yasiyo na tija ambayo hayaendi popote na ukiuliza unatafuta ubaya.

Kwahyo watu wa Igunga kila mtu anasababu kuipigia kura Chadema kukataa uonevu tuliofanyiwa kwa miaka mitano.

Sasa kama tuliwachagua wenyewe kwa kura basi tunaweza kuwaondoa Sisi wenyewe kwa kura, tutumie uchaguzi mkuu huu kuwaondoa hawa watu. Watu wa Igunga mkipiga kura ya uhuru na haki tutapata uhuru na haki, nawaombeni mpige kura ya haki kuchagua viongozi watakaosimamia haki. Tarehe 28 tupige kura ya haki ili tumuondoe Magufuli. Tupige kura ya haki tutibu Watu walioumizwa, tufungue milango ya magereza kwa waliofungwa bila hatia, tupige kura ya haki kukataa uonevu wa kila hali. Siku zote haki uinua taifa, basi chagueni haki ili taifa liinuke.

Wimbo mnaotakiwa kuuimba wiki mbili hizi kuwa hatutaki kuibiwa kura, zingatieni haya moja mawakala wote wameapishwa na mkurugenzi, mkurugenzi akikataa nasisi tumkatae. Lapili lazima muhakikishe mawakala wanakuwepo kwenye vyumba vyakupigia kura kama mawakala hawapo basi zoezi lakupiga kura lisianze bila mawakala. Latatu Mawakala Wetu kupewa hati za matokeo, tusikubali mawakala wetu wasitoke bila kupewa fomu za matokeo. Na mwisho mkishajua mmeshinda ingieni barabarani kuijulisha dunia kuwa umeshinda.

Maombi yangu kwa Madaktari na Waganga wa nchi hii mtuambie Magufuli yuko sawasawa au La maana anayoongea haeleweki. Na anafanya uchaguzi leo anapumzika siku nne.

Nawashukuru sana Igunga na Mungu awabariki.

=====

*NZEGA*

Maelfu ya wananchi wa Nzega wamiminika kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi mkuu Kwenye viwanja vya stendi ya zamani kumshuhudia Mheshimiwa Tundu Lissu.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na watu Nzega amesema haya..

Hongereni watu wa Nzega, na nashukuru sana kwa mapokezi makubwa.

Sasa uchaguzi mkuu huu ni muhimu sana kwenye maisha yetu, ni hiari yetu kuchagua mitano tena au mitano kwanza. Tukisema mitano tena maana yake tuendelee kuteswa, kuuliwa, kunyanyaswa, kuibiwa na kupotea kwa watu au Mchague mitano kwanza kwa kupigia kura Chadema ili ije iondoe mateso nakuleta Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Sasa kwakuanzia watu wa Nzega pigia kura madiwani wote wa Chadema ili wakaongoze halmashauri. Kura ya pili pigieni mbunge wa Chadema *Merry Atonga.*

Nakura ya mwisho ni kati yangu mimi Tundu Lissu mwenye kuamini Uhuru, Haki na maendeleo ya watu na yule anayejiita jiwe. Jiwe amesababisha msiba mkubwa kwenye nchi yetu, Magufuli amekuwa akidharau akina mama nchi hii. Sasa watu wa Nzega kwenye uchaguzi wa raisi mnajua mchague Kati ya mitano kwanza au mitano tena.

Ndugu zangu wa Nzega mjini tarehe 28 naomba mkapige kura kukataa hivyo vitambulisho vya wajasiriamali. Vitambulisho haina jina, picha, anuani wala sign. Hii misafara inayofanywa na Magufuli na Magari kibao ni hizi pesa Za vitambulisho. Sasa tarehe 28 tukapige kumalizana na Magufuli, tupige kura tukae ndugu zetu kufungwa kwa kesi zauongo. Watu wa Nzega naomba tarehe 28 mkapige kura tumuondoe muovu. Nzega mkapige kura na kulinda kura, msiogope askari awa nao ni wameumizwa na Magufuli, miaka mitano hawajaongezewa mishahara lazima watasimamia kwenye haki.

Ahsante sana Nzega na Mungu awabariki.
IMG-20201012-WA0067.jpg
IMG-20201012-WA0065.jpg
IMG-20201012-WA0068.jpg
IMG-20201012-WA0069.jpg
IMG-20201012-WA0062.jpg
IMG-20201012-WA0063.jpg
IMG-20201012-WA0060.jpg
 
Wakuu bado tunaendelea kuwaletea taarifa za Mh Tundu Lissu kutoka popote anapopita kuomba kura

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika

View attachment 1597566

=========

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tundu Lissu, akiambatana na mkewe, Bi. Alicia Magabe, akimjulia hali Ndugu Wilfred Enock anayejulikana pia kwa jina la Chaijaba ambaye ni maarufu mjini Singida kutokana na kutembea na toroli la kubebea mizigo likiwa na bendera ya Chadema kila aendako. Ndugu Chaijaba alivamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali mwilini na watu ambao hadi sasa hawajakamatwa, waliokuwa wakimhoji sababu za mapenzi yake kwa Chadema.
View attachment 1597674View attachment 1597675View attachment 1597676View attachment 1597677View attachment 1597678
"Msafara wa Mheshimiwaa Tundu Lissu umesimamishwa na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Tumuli, wilayani Mkalama Mkoani Singida.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Tumuli amewakumbusha kuhusu umuhimu uchaguzi mkuu, miaka mitano ya Magufuli imekuwa ya shida na vurugu. Watu watekwa, wameuliwa, wamenyanyaswa, wamekosa mishahara na kudhulumiwa kila mahali. Mfano halisi mmeona kwangu nimepigwa risasi 16. Nchi imekuwa ikiogopeka nakila mtu sasahivi ni rahisi kumtaja Mungu kuliko kumtaja Magufuli. Ndomaana nasema uchaguzi mkuu huu ni muhimu, tukishindwa tumekwisha.

Na katika kuhakikisha yote haya yanakuwa sawa ndo maana Chadema ilani yetu inazungumza kuhusu Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Najua wote tunataka Uhuru, Haki na maendeleo. Kukiwa na haki hata Taifa huinuka. Basi mchague viongozi wa Chadema wasimamie nakutekeleza ilani ambayo kila mmoja itamgusa.

Ili yote haya tuyakomeshe tarehe 28 nawaomba wananchi wa Tumuli mjitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wa Chadema.

Mgombea udiwani wenu hapa Tumuli ni Haruna Khamis

Namgombea Mbunge Oscar Alex Kapalale
View attachment 1597688View attachment 1597687View attachment 1597686
Hakuna supporters hata kidogo,kachokwa huyu puppet
 
Back
Top Bottom