Kampeni meneja na Mbunge wa Chadema washikiliwa na polisi Igunga

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,185
1,639
Leo asubuhi zaidi ya polisi 50 walimshika Kampeni meneja ambaye pia ni Mbunge wa Maswa mashariki,mh Kasalamboi pamoja na mbunge wa viti maalum Suzan Kiwanga, baada ya kuwashikilia kwa muda na kutoa maelezo kwenye kituo cha polisi hapa Igunga.

Wanatuhumiwa kumpiga DC wa Igunga, baada ya kuandika maelezo wamewahamishia Tabora mjini, hadi Jumatatu watakapofikishwa mahakamani.

Hii ni ishara nyingine ya jeshi la polisi kutumiwa na CCM, DC aliingilia mkutano wa Chadema, tukaenda kushitaki, halafu Wabunge wetu ndio wanakamatwa,huu ni uhuni mkubwa.

Kamwe haturudi nyuma wala kukata tamaa, tutasonga mbele na kamwe haki haikuwahi kushindwa
 

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
406
125
leo asubuhi zaidi ya polisi 50 walimshika kampeni meneja ambaye pia ni mbunge wa maswa mashariki,mh kasalamboi pamoja na mbunge wa viti maalum suzan kiwanga, baada ya kuwashikilia kwa muda na kutoa maelezo kwenye kituo cha polisi hapa igunga. Wanatuhumiwa kumpiga dc wa igunga, baada ya kuandika maelezo wamewahamishia tabora mjini, hadi jumatatu watakapofikishwa mahakamani. Hii ni ishara nyingine ya jeshi la polisi kutumiwa na ccm, dc aliingilia mkutano wa chadema, tukaenda kushitaki, halafu wabunge wetu ndio wanakamatwa,huu ni uhuni mkubwa. Kamwe haturudi nyuma wala kukata tamaa, tutasonga mbele na kamwe haki haikuwahi kushindwa
aliingilia mkutano mkaenda kumshitaki eeeeh..! Haya nendeni mkamtoe tena na huko polisi......!! Yote hii inatokana na (mob schology)
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Polisi watangulie kumshikilia Kibaka Mwigullu Mchemba na wana-CCM wengine wanaosambaza UKIMWI kwa makusudi Igunga hivi sasa laa sivyo vijana tutafanya uzuri sana kazi hiyo; saa, wakati na mahala popote pate.
 

Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,282
5,721
makamanda wamewahamishia mkoani kisa wanaogopa vurugu kutoka kwa wapenzi wa cdm! Ova!
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
20,412
26,565
hatutishwi na kushikiliwa polisi na hiyo haitarudisha nyuma nguvu ya umma.kukamatwa kwao ni kisiasa.polisi walishakatazwa kuingilia siasa.mwisho wa siku polisi watafyata mkia.mia
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,940
Mkuu poleni kwa mikasa ya polisi. Hapo lazima muweke mezani plan B kwa ajili ya kampeni za igunga. Kwenye uwanja wa mapambano magamba wamebaini kabisa kwamba hali yao ni mbaya sana wameamua kulitumia jeshi la polisi kuwavuruga.

Mnatakiwa kutuliza akili na kuteua haraka watu wengine kuongoza mapambano huku mkifuatilia kwa karibu mwenendo wa hao vibaraka wa magamba.

Kwanini wamewahamishia tabora?
 

superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
51
polisi walipata barua ya spika kuwaruhusu wawakamate? Tanzania imefika wakati sheria zinaanza kuwekwa kando na maamuzi yote yanafanyika through masaburi , dc mlinzi wa amani anapovuruga amani tena kwenye eneo lake inakuwaje? Anataka ananilea amtetee kwa kuharibu kuminya demokrasia? !
 

Wemba

Member
Jul 14, 2011
62
21
Kweli itashinda, kwa namna tunavyoishi,
Kweli kitu aushi, haiogopi nguvu ya JESHI.
Kweli itashinda KESHO, KAMA LEO HAITOSHI.

Source: Masomo yenye Adili - Shaaban Robert.
 

Daffi Jr

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
3,829
905
Nataman niwatukane mapolisi vilaza wanaotumiwa kuukandamiza demokrasia na haki za binadamu!ni uhuni wanaufanya bila kuangalia upande wa pili(ccm),hivi ukiwauliza wanapata manufaa na faida gani kufanya hivyo?wako sahihi kweli!yaani basi tu!shame upon them na magamba yao!the day will come!
 

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Hilo tulilitegemea wengi kwamba watawakamata na kweli yametimia,ila CCM kwa maana ya polisi,magamba yote yaliyomo na ccm B kwa maana ya CUF watake wasitake siku zinahesabika na wao ndo wanazidi kuishiwa na kwa hali hii CDM wanazidi kuwapa umaarufu.hivi kwa nini huyo DC wa magamba asingekamatwa kwa kuingilia mkutano wa kampeni?kwani alikuwa hajui kama kuna mkutano wa kampeni?na kwanini alikuwa anaendesha mkutano wa kisiasa maana alikuwa na makada wa ccm pamoja na watendaji wa kata na vijiji na wengineo walikuwa wamevaa kabisa nguo zao,sasa nani hapo alifanya fujo?
Wanajaribu sana kuwavunja nguvu lakini mashine za CDM bado ziko nyingi sana najua zitakwenda Igunga na mambo yatanyooka tu.na hao CCM na polisi wao wanashangaza sana na wakumbuke Mungu haja lala.
Niwakumbushe kisa kimoja:mwaka jana kwenye kampeni za uchaguzi jimbo la Maswa Magharibi mchuano ulikuwa kati ya Shibuda na Robert Kisena huyu alonunua UDA,Ikumbukwe kwamba Robert alikuwa mgombea wa CMM aliwahi KUMPIGA OCD WA MASWA PALE PALE KITUO CHA POLISI.Alifanywa nini?au kwa kuwa alikuwa ni wa CCM?leo DC ameingilia mkutano akaondolewa haijaonekana kama alifanya kosa na ndio amekuwa chanzo cha vurugu.
Haturudi nyuma hata wakitujaza magereza yote poa lakini mpaka kieleweke.
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,940
kwani tabora hakuna nguvu ya umma, cdm kweli ni kelele na mikwara mingi vitendo ZERO.

Katika zile kura 11,000 mlizopata katika uchaguzi mkuu mwaka jana tayari kura 8,000 zimeshaota mbawa kuelekea chadema.

Utumieni vizuri muda uliobaki kuzihifadhi hizo kura zilizobakia vinginevyo nazo zitakwenda na maji.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,579
25,246
move hiyo ina hasara kwa ccm, ni faida kubwa kwa cdm. wananchi wanazidi kuamini kuwa serikali ya ccm ni ya kikandamizaji. wako tayari kutumia helicopta kumpeleka mbowe arusha kwenye kesi kana kwamba wanatekeleza majukumu kuwatumikia wananchi hapo hapo wanakosa helikopta kuokoa wenye nchi na kuwaacha wafe maji nungwi. wachina wakimpiga ocd hakuna hatua, mbunge kumzuia mkuu wa wilaya asivunje sheria na taratibu za uchaguzi serikali inakuwa kinyume cha jamii. hayati Kolimba enzi za uhai wake alipata kusema CCM IMEPOTEZA DIRA NA MWELEKEO, huku ndiko kupoteza hiyo dira, na mwelekeo wa wananchi utakuwa kinyume na ccm.
 

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,696
781
polisi walipata barua ya spika kuwaruhusu wawakamate? Tanzania imefika wakati sheria zinaanza kuwekwa kando na maamuzi yote yanafanyika through masaburi , dc mlinzi wa amani anapovuruga amani tena kwenye eneo lake inakuwaje? Anataka ananilea amtetee kwa kuharibu kuminya demokrasia? !
<br />
<br />

Du! Mheshimiwa msomi sana wa Kitanzania, ni sheria gani? Inayoruhusu Mbunge afanye makosa alafu kukamatwa kibali atoe spika. Someni sheria kwa undani...najua umekurupuka sheria haisemi upige mtu baa alafu hushikwi mpaka kibali cha spika. Sheria anamlinda mbunge wakati yuko kwenye vikao rasmi vya bunge au akiongelea jambo lolote akiwa bungeni hawezi shitakiwa kwenye mamlaka nyingine yoyote.
 

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
513
Safi sana wamekamatwa haiwezekani wamkamate DC wao ni nani wana mamlaka gani achenio uxhabiki sheria ichukue mkondo wake!!
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,786
Dah! Inasikitisha.kumbe hata na wabunge wa CDM wanatumiaga masaburi kufikiria?.Nimepata jibu ktk tukio la kumshambulia DC kuwa hawafikirii kabla ya kutenda na wabunge hawa wameaibisha padre na CDM kwa ujumla.Walaaniwe kumshambulia DC!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom