Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,062
- 731
Anatembea taratibu mikono mfukoni.
Uso umejaa soni.
Anatazama chini huku kichwa kimeinamia upande .
Midomo imetengeneza umbo la kutabasamu pia yapiga miluzi ya kujikonga
Miguu yaenda ikipiga maganda makavu ya miwa njiani kwa namna ya kujiliwaza.
Macho yamejaa malengelenge
koo limemkauka.
Na nyimbo zimemwishia.
Amebakia na miluzi
Huyoo
Taratibu ajikongoja kurudi mawiyoni mwake.