Kampeni chafu zaanza UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni chafu zaanza UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KadaMpinzani, Oct 18, 2007.

 1. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  UVCCM yasema maandamano ya wapinzani hayana jipya

  *Yawafananisha na kikundi cha uzushi na propaganda

  Na Gladness Mboma - Majira

   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naona Bwana Makalla ameishiwa hoja na sasa anakuja na cheap politics ambazo kwa hapa tulipo sidhani kama inasaidia.

  Hiyo Ilani ya Uchaguzi anayoiongelea kwamba serikali ya JK ilikuwa inaitekeleza kwa kasi iko wapi? Maisha bora kwa kila mtanzania? Kupaa kwa ndege ya Lowassa na kugawana kisungura bungeni? Tangu lini sungura akashibisha watu walio na njaa?

  Amedai kwamba hoja za ufisadi ni uzushi na uongo, ina maana anapingana na report ya CAG? Kama ni hoja za uzushi na uongo kwanini hao waliozushiwa including Rais na Waziri Mkuu hawajaenda mahakamani kudai haki? Asitufanye sisi ni mazuzu na kwamba hatuelewi, watanzania wa leo si wale wa miaka ya CCM kushika hatamu ambapo hata news tulizokuwa tunapewa ni zile tu ambazo CCM na serikali yake walitaka tuzisikie. Leo hii tuna access ya sensitive information zinazoigusa serikali.

  Hivi amesoma news za kuvuja kwa mkataba wa Richmond na akaona serikali ya CCM ilivyoingilia swala zima la huo mkataba?? Jamani hizi cheap politics zitatufikisha pabaya, kesho na keshokutwa same person ukimuuliza kauli yake anaweza kuiruka.
   
 3. M

  MC JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hana hoja huyo mwandishi, anajua CCM ikianguka na yeye hana chake; anatetea maslahi yake tu, kwa kuwa kauli yake inapingana hata na ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wake wa chama, Rais amesema madai yanafanyiwa kazi, yeye anasema madai yapuuzwe, kwa hiyo anampinga Mwenyekiti wake, CCM bwana Kazi kujichanganya tu,
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  nani ana e-mail ya makala nimtumie mkataba wa Richmond?
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...huyu hata kujibiwa hafai!
   
 6. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  JK inabidi akae kimya na awaache vijana ( Makalla ) wawajibu viongozi wa dini turned into politicians ! JK is way far ahead in politics with this newly political recruits !
   
 7. m

  mwewe Senior Member

  #7
  Oct 18, 2007
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 125
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu Makalla si ndiye yule bwana aliyebwagwa kwao na Mwarabu wa kuja kwenye mchakato wa ubunge jimbo la Mvomero. Kama wanakijiji wa Turiani, Mgeta, Dumila, Mlali, Changarawe (MU) etc. walimuona hana maana na wakamnyima kura - unategemea nini kutoka kwake!
   
 8. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  uliyosema hapao juu mwewe siyafahamu kiundani, lakini nasema hivi, hao viongozi wa upinzani watadebate na vijana, JK is busy working for the people !
   
 9. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Natamani sana ITV wangerudisha kipindi cha malumbano ya hoja, nadhani wananchi tungeyajua mengi zaidi ya haya tunayoyajadili hapa JF. Tungepeleka takwimu kibao na pia tungepata na nyngine zaidi.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  For sure Jk is busy! Only bad side of it, he is not busy working for the people but: 'Vascodagamaring' allover the world bedding in five star hotels and protecting all Big FISADI with all his mighty!

  What an absurd?
   
 11. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  watu wengine mnachekesha na nadhani uchekeshaji wenu is part of your system, sasa unatakarais akae 2 star hotel ?

  mambo mengine yaani ni kuongea ili mradi kuongea ! hata kama kungekuwa na scale ya 25 star hotel, still ingekuwa vizuri angekaa huko kama rais !

  kama utaangalia upande mbaya tu wa JK then nadhani hautokuwa na matumaini yoyote so wewe endelea kuangalia upande wake mbaya tu, na usiniambie hana mazuri !
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,193
  Trophy Points: 280
  Wapuuzi wengine hawa ambao hawana cha kusema, lakini na wao lazima wabwabaje tu, hivi hawaoni alama za nyakati ili waache kujibaraguza!?
   
 13. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ?????????????????? am lost !
   
 14. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bubu,

  Acha waendelee kupagawa. Kila mara nafananisha majibu ya hawa jamaa na yule waziri wa habari wa Iraqi aliyekuwa anasema kuwa majeshi ya marekani hayapo Iraq wakati wao wako nyuma yake.

  CCM watasema sana mwaka huu. Wananchi wamechoshwa na hali ngumu ya maisha, ujenzi, usafiri vyote vimekuwa ghari, nchi inauzwa kwa bei chee tu, na wao wanadai kuwa ni uzushi tu.

  Masikini Tanzania!
   
 15. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uzuri ni kuwa watanzania wameamka,kwa hiyo akina UVCCM siwatofautishi na waigizaji wa michezo ya kitoto.Mwaka huu mtakoma ubishi.
   
 16. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ccm Oyeeee !
   
 17. p

  princejafari Member

  #17
  Oct 18, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa vijana wa CCM ni aibu tupu. Nilitegemea kwamba UVCCM ndicho chombo ambacho kingeongoza harakati za kuwango'a na kuwatupilia mbali viongozi wabadhirifu ndani ya CCM. Hii ndiyo inatakiwa kuwa mission ya UVCCM, yaani kukisafisha chama, kuondoa uozo (ama ni uvundo?)na kulinda maadili. Hii ndiyo maana ya kuwa kijana, na siyo kuwa bendera fuata upepo, na kurudia kama kasuku yale yanayosemwa na viongozi wa juu wa CCM (repeater, relay station!)

  Tulitegemea UVCCM ingewasha moto ndani ya CCM kwa kuunga mkono hoja ya Mh Zitto Kabwe. Strategically thinking this would have stolen the 'thunder' out of chadema na kuifanya CCM ionekane kuwa ni chama ambacho kinajali maslahi ya wananchi.

  Lakini kwa vile UVCCM ina ufinyu wa fikra, wanakubali tu kulishwa makombo ya wezi na wafujaji wa mali za umma. sasa kama CCM inategemea ku-draw uongozi wake siku za mbeleni kutoka katika kundi hili la mambumbumbu wa UVCCM basi wajue chama kimekufa.

  Walikuwa ni vijana wa ANC walioanzisha 'Umkhonto we Sizwe' baada ya kuona wazee wanasuasua kuwakomalia makaburu! Hivi hii UVCCM inawakilisha maslahi ya nani? Naifananisha UVCCM na 'Hitler Youth'...given their low IQ i doubt whether anyone at UVCCM has ever done a comparative study of mass youth movements.

  Shule Kidogo : Hitler Youth or Hitler - Jugend..was established since 1922 as an organisation that paid 100% allegiance to Hitler na ndio waliomsadia kufanya mauaji ya kimbari pamoja na vitendo vingine vingi vya kinyama. Atakachosema JK, basi UVCCM wataufyata! Atakacho sema Kingunge tawile! Pamoja na kuwa utamaduni wa kulazimisha uanachama UVCCM haupo, utamaduni wa utii kwa viongozi wa juu hata kama hawastahili bado umeshamiri. Utamaduni wa kujikomba (butt licking) huo ndio usiseme. Vijana wanashindana kuonyeshana nani damu yake ni kijani zaidi! Well in medical terms it is all contaminated blood. Haifai! Hakuna hata mmoja katika UVCC mwenye uthubutu wa kumwambia mfalme yuko uchi.. Vijana wa enzi ya Jenerali Ulimwengu mko wapi?


  Ukiangalia Who's Who katika safu ya uongozi wa UVCCM utaona bayana kwamba ni watoto wa viongozi ama wa sasa ama wa awali wa CCM. Hivi kweli watanzania tunategemea jipya kutoka kwa uongozi wa UVCCM, uongozi ambao unaundwa na watoto wa 'wakubwa wa ccm'? Hata siku moja huwezi kumpelekea nyani kesi ya tumbili kuchoma msitu. Mwalimu wetu Professor Shivji would have said..'UVCCM provides a platform for the ruling class to reproduce itself'! how true! Like father like son......mtoto wa nyoka sio njiwa ni nyoka!

  Kwa kifupi, UV-CCM ya kufikirika na kusadikika ( asante Shaaban Robert!) ingeshafanya mambo yafuatayo:
  1. Kuandaa maandamano ya vijana nchi nzima, kupinga ubadhirifu, rushwa na ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na viongozi wa ccm.
  2. Kupeleka hoja ndani ya Halmashauri ya CCM, kuwafuta uanachama, mawaziri na watendaji wote mafisadi ( kwa lugha ya mtaani we call this 'the purge')
  3. Kuaandaa rasimu ya marekebisho ya sheria zinazohusiana na rushwa, maadili ya uongozi, na taasisi za uchunguzi/usimamiaji. si wabunge mnao bungeni? ama mnaishia tu 'sikubaliani na maelezo lakini naunga mkono mia kwa mia?'

  kama kweli UVCCM iko kwa ajili ya maslahi ya watanzania watatekeleza hayo mapendekezo haraka! Uwezekano upo? Mh labda katika ndoto. Kwa hili chances are that China will invite the Dalai Lama to give the keynote speech at the opening ceremony of the forthcoming Olympic Games in china.

  Na chansi ya mimi kuwa mwanachama wa UVCCM? well after i am dead for a century!
   
 18. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  unataka kadi ya uanachama UVCCM? sema. you like any other tanzanian can join UVCCM.
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mafisadi wote Duniani wanafanana.
  Hiltler alisimama kidete na kupigana na majeshi ya kitimu ya nchi za magharaibi mpaka siku ya mwisho, japo mapema kabisa alijua hawezi shinda vita hata akizikwaa nguvu zote za ibilisi.

  UVSISIEMU wanaelekea kuzimu wakiwa wametinga Tai zao nadhifu za Kijani kwa Utii mkuu.

  Kila Sentensi za mabosi wao Fisadi ni Amri isiyo pingika wala kujadiliwa na inatekelezwa mara moja.
  Vijana hawa wako mstari wa mbele kulinda Maslahi ya wachache ndani ya Chama chao kwa imani ya kusubiri zamu yao ifike waushike mwenge wa Ufisadi na kuendeleza utamaduni wa ukengeufu.

  Wamesahau kabisa kwamba Mwasisi wa mapambano ya kujikomboa kutoka katika makucha ya kuonewa kudharauliwa kupuuzwa na kunyonywa na mfumo wa ubepari duniani,MWalimu JK Nyerere, alianzisha mapambano hayo akiwa kijana tena kwa kujenga hoja ambayo kwa wakati ule haikuwa maarufu kabisa ndani ya TAA, Hoja ya kudai Uhuru kutoka kwa Waingereza bila woga.

  Leo hii vilembwe wake ndani ya chama alicho saidia kukianzisha wanaunga mkono mambo kwa kuangalia ukubwa wa Vinywa, Matumbo na Makalio yao na kusahau kwamba chama ni mali ya wanachama ambao ni wananchi wa kawaida.
  Wamesahau kabisa kwamba Uhuru Haki Usawa na Amani ni mambo ambayo siku zote yatalindwa kwa gharama yeyote ile hata kama ni kupoteza umaarufu ndani ya chama.

  Vijana kwa kuzingatia kwamba wengi wao wataishi muda mrefu zaidi kuliko wazee waliowatangulia, wanategemewa kuiona kesho na keshokutwa kwa kutathmini kinachoendelea sasa na historia nzima tangu awali.

  Matatizo siku zote yana kanuni zifananazo na kanuni za viumbe hai yanazaliwa, yanakua pia yanakufa.

  Kimsingi, tatizo lisiposhughulikiwa siku ya kufa ni lazima life na watu walizungukao.

  Nionavyo mimi UV SISIEMU wanajitoa Muhanga kufa na matatizo ya wazee wao.

  Kifo chema UV SISIEMU!
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  tunahitaji kiburudisha barza kama wewe hapo ^^^^^^^^ !
   
Loading...