Kama una nduguyo ama jamaa unayemjali, tafadhali ni bora ukampeleka VETA kuliko pale Kampala Int. University. Kwanza hakijapata usajili Tanzania kama Chuo kikuu bali ni study centre tu.
TCU (Tanzania Commission for Universities) hakitambui uwepo wake (hakina accreditation). Nilijaribu kuwasiliana na HESLB kwa ajiri ya kujua kama wanatoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma palw KIU (Gongo la Mboto), jamaa jibu walilonipa kuwa HAWATOI. Walifika mbali na kusema hata lecturers wa pale ni uchwara na wanaokoteza rejects zenye PASS bachelor degrees!!
Sikuishia hapo wakuu, nikachoma mafuta mpaka Campus hiyo ya Gongo la Mboto, jamaa wana majengo takribani 6 hivi (single storey buildings) yenye ukubwa wa kawaida huku hawana hata hostel moja. Hostel iliyopo humo ndani inamilikiwa na shule moja ya sekondari (jina nimesahau) ambayo inapakana nayo upande wa kulia. Kifupi study centre hii haina infrastructure za kutosha kukidhi mahitaji ya chuo kikuu.
Nilipatwa na mshtuko pale nilipoongea na wanafunzi wa pale, hao walikuwa wanasomea Human resources (degree), nilipowahoji entrance qualification zao, mmoja (jina kapuni) akasema ni form IV na amemaliza St. Mary DSM, mwingine ni certificate ya HR toka CBE wakati wa tatu alisema ni form six Div Four. Baati mbaya mwanafunzi wa nne alikataa kunieleza.
Ingawa nakiri mazingira (location) ya chuo ni nzuri compared na IFM au CBE.
Cha mwisho wakuu, hakuna application yoyote itakayotumwa na mwanafunzi kuomba udahili pale KIU ikakataliwa kwa misingi ya entrance qualifications!!
Wadau labda mtaniuliza nilikuwa na interest gani kufuatilia details zote hizi, nina mtoto wa kaka yangu kafanya vibaya sana form six (ana Div 0) tough form 4 alifanya vizuri sana, lakini kapata admission KIU kozi ya BBA. Kwa sababu alikuwa anamshawishi sana baba yake kuanza kusoma hapo chuoni, mi nikamtahadhalisha kwamba asubiri kidogo nifanye utafiti mdogo wa kuangalia suitability ya chuo hicho. Mtoto wako akisoma chuo hicho hata kuajirika katika soko la ajira la sasa itakuwa ngumu sana!!