Mtoa mada je una ushahidi na unachokisema? au ni kama yale ya magazeti ya udaku wanaandika habari wanakuambia chanzo cha habari ni jirani na mpita njia?
Tukiacha suala la ada kubwa KIU ni mkombozi wa elimu ya juu Tanzania.Nitakutolea mfano,Kijana kasoma shule ya serikali ambayo ina mwalimu 1 tu wa biologia,kajitahidi kamalia f6 PCB ana EDD,kijana amefaulu anataka kuomba B Pharm,Muhimbili wanachukua wanafunzi 60,akienda CUHAS(Catholic university)wanachukua wanafunzi 15,lakini akija KIU chuo kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 550 kwa mwaka kozi ya BPharm.
Kwa hiyo ukiangalia kwa jicho makini KIU haichukui vilaza ila wana uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi ambapo hata Muhimbili wangeweza kuchukua BPharm wanafunzi 800 basi cutpoint ingekuwa 4.5 kama ya KIU je tungewaita Muhimbili vilaza?
Suala la KIU hakijasajiliwa na TCU sithani kama ni kweli mana nina mdogo wangu yuko pale anaingia mwaka wa pili BPharm na anamkopo.
Jaribuni kuingia website ya TCU download undergraduate admissions guidebook for higher education institute in Tz,nenda page no 70 utawakuta KIU utakuta kozi nyingine wanachukua wanafunzi 600 tena za ualimu ukiwa na EEE utaachwa kweli.