Kampala international university

Brandon

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
336
5
Jamani wakuu salaam,

kun hiki chuo kinaitwa kampala int university kipo gongo la mboto,kinatoa mafunzo kuanzia ngazi ya certificate hadi masters. Mnakionaje? Nilifanikiwa kucheki timetale ya masters program, wana lecturer mmoja tu ambaye n doctor,waliosalia ni mr au ms. Hamna prof hata mmoja.
Sasa nauliza hivi mmnadhani watatoa quality education kweli? Au ndo bora cheti?
 
Kazi kweli,maana kwa sasa naona watu wengi wanasoma pale. Nimeuliza nimesikia pia kuna watu wanasoma phd pale.
 
wadau hawajaona hili bado? Tutegemee product za aina gani toka ktk 'taasisi za hovyo hovyo' zinazojali mapato kuliko kujali ubora wa taaluma..hii ni kansa ya fikra..Brandon attach prospectus yao km ushahidi!
 
hapa tanzania kuna vyuo vingi tu vinafanana na kampala international University,kimojawapo IFM(Institute of Finance Management)hiki chuo kinaendeshwa kisanii sana kama husomi pale huwezi kuamini ukiambiwa ingia uone,hakuna Quality wanajali pesa
 
hapa tanzania kuna vyuo vingi tu vinafanana na kampala international University,kimojawapo IFM(Institute of Finance Management)hiki chuo kinaendeshwa kisanii sana kama husomi pale huwezi kuamini ukiambiwa ingia uone,hakuna Quality wanajali pesa

Yaani hichi chuo cha KIU hata kukisikia sitaki matapeli watupu nasikia wana Campus kule gongo la mbali
 
Kama una nduguyo ama jamaa unayemjali, tafadhali ni bora ukampeleka VETA kuliko pale Kampala Int. University. Kwanza hakijapata usajili Tanzania kama Chuo kikuu bali ni study centre tu.

TCU (Tanzania Commission for Universities) hakitambui uwepo wake (hakina accreditation). Nilijaribu kuwasiliana na HESLB kwa ajiri ya kujua kama wanatoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma palw KIU (Gongo la Mboto), jamaa jibu walilonipa kuwa HAWATOI. Walifika mbali na kusema hata lecturers wa pale ni uchwara na wanaokoteza rejects zenye PASS bachelor degrees!!

Sikuishia hapo wakuu, nikachoma mafuta mpaka Campus hiyo ya Gongo la Mboto, jamaa wana majengo takribani 6 hivi (single storey buildings) yenye ukubwa wa kawaida huku hawana hata hostel moja. Hostel iliyopo humo ndani inamilikiwa na shule moja ya sekondari (jina nimesahau) ambayo inapakana nayo upande wa kulia. Kifupi study centre hii haina infrastructure za kutosha kukidhi mahitaji ya chuo kikuu.

Nilipatwa na mshtuko pale nilipoongea na wanafunzi wa pale, hao walikuwa wanasomea Human resources (degree), nilipowahoji entrance qualification zao, mmoja (jina kapuni) akasema ni form IV na amemaliza St. Mary DSM, mwingine ni certificate ya HR toka CBE wakati wa tatu alisema ni form six Div Four. Baati mbaya mwanafunzi wa nne alikataa kunieleza.

Ingawa nakiri mazingira (location) ya chuo ni nzuri compared na IFM au CBE.

Cha mwisho wakuu, hakuna application yoyote itakayotumwa na mwanafunzi kuomba udahili pale KIU ikakataliwa kwa misingi ya entrance qualifications!!

Wadau labda mtaniuliza nilikuwa na interest gani kufuatilia details zote hizi, nina mtoto wa kaka yangu kafanya vibaya sana form six (ana Div 0) tough form 4 alifanya vizuri sana, lakini kapata admission KIU kozi ya BBA. Kwa sababu alikuwa anamshawishi sana baba yake kuanza kusoma hapo chuoni, mi nikamtahadhalisha kwamba asubiri kidogo nifanye utafiti mdogo wa kuangalia suitability ya chuo hicho. Mtoto wako akisoma chuo hicho hata kuajirika katika soko la ajira la sasa itakuwa ngumu sana!!
 
Afadhali nime elimika kuna mtoto wa shangazi yangu anakwenda hapo kuanza masomo - kumbe ni bomu
 
Hivi TCU ipo wapi?? Inafanya nini? Nauliza kwa sababu wao ndiyo wanapaswa kusimamia vitu vyote vinavyoitwa "Vyuo vikuu" hapa Tz, na wanatakiwa kuwapa wananchi taarifa sahii punde inapobidi. Nadhani kuna harufu ya UFISADI!:A S angry:
 
Na hao wanaojiunga na vyuo fyongo kama hivi nadhani ni watu wazima wenye akili timamu..hivi wanajisikiaje? just thinking aloud.
 
jamani msiseme hicho chuo tu,hata hivi vya kwetu havina tofauti na hicho,mshangai kwanini wakina chenge, makamba, wanawapeleka watoto wao ulaya kusoma, wanajua kuwa vyuo vyetu vya kisanii
 
kuna rafiki yangu anasoma postgraduate pale IFM mambo anayonieleza siamini,mapinduzi yanahitajika kila sehemu
 
Mkuu swala la uhalali unauliza Tanzania? huyo mtu mwenyewe anayetoa kibali ana degree na Phd za Mafungu hata reasoning hakuna, hii nchi inahitaji ukombozi katka kila idara

jamani sasa tulitegemea nini ikiwa hata rais wa ccm ana PhD ya mitaala aliyoipata anjuan Comoro
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom