Kamchape wanachafua taswira ya Serikali

Omolo

New Member
Jan 31, 2021
2
0
Kutoka Kata ya Rungwe Mpya Kasulu Kigoma.

Hivi karibuni kumezuka watu wanaojiita kamchape katika Mkoa wa Kigoma na viunga vyake, watu hawa wanadanganya wananchi kwa kutumia mazingaombwe kwamba wanatoa uchawi kitu ambacho si sahihi, mbali na jamii ya watu wa Kigoma kuamini hayo mambo, kikundi hicho kimeenda mbali zaidi mpaka kuingia kwenye taasisi za serikali kama vile Shule na hospitali kwamba wanatoa uchawi kitu ambacho kinaashiria kwamba serikali inaamini uchawi.

Hivyo natoa rai kwa Serikali kuangalia hilo jambo kwa undani zaidi kwani watumishi kama sisi walimu tunapokataa jamii inatuona kama sisi pia wachawi. Pili watu hao wamekuwa wakitoza elfu tano kila kaya na ukisema huna hiyo hela wanafanya mazingaombwe ili jamii waamini zaidi kwamba wewe ni mchawi.
 
Back
Top Bottom