BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,109
Date::7/12/2008
Kambi ya upinzani wafurahia waziri kuitosa serikali bungeni
Na Kizitto Noya
Mwananchi
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha kwamba, Kampuni ya Deep Green Finance ilifunguliwa na kufungwa kwa agizo la serikali, imefungua ukurasa mpya wa mjadala wa ufisadi nchini.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Slaa alisema, kauli hiyo imeondoa utata kuhusu mmiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa imeeleza wazi kuwa, serikali ndiyo iliyohusika kuchota mabilioni ya fedha za wananchi kupitia akaunti hiyo ya Deep Green Finance.
Alisema, anamshukuru Waziri Masha kwa ujasiri wake wa kuitosa serikali na kusema ukweli, jambo ambalo litamsaidia (Dk Slaa) kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na wizi huo unaochangia umaskini wa Mtanzania.
"Sisi tumeipokea kauli hiyo vizuri na tumemshukuru Waziri Masha kwa kuitosa serikali na kutuonyesha mlango sahihi wa suala hilo ambao hatukuujua," alisema Dk Slaa.
Alisema, Chadema haina shaka kwamba kauli hiyo ni sahihi, kwani haijakanushwa na serikali na hivyo kuichukulia kwa uzito unaostahili katika harakati zake za kutaka fedha hizo zirejeshwe.
"Kimsingi, sina shaka kwamba kauli hiyo ni sahihi, kwani haijakanushwa wala kutolewa ufafanuzi mwingine, hivyo nitaichukua kama ilivyo ili inisaidie katika vita vyangu dhidi ya mafisadi," alisema.
Alisema, kauli hiyo imemwonyesha adui halisi katika mapambano dhidi ya ufisadi na hivyo kurahisisha mapambano hayo kwa kiasi kikubwa, tofauti na zamani ambapo kazi ilikuwa ngumu kutokana na kutomjua mhusika halisi wa suala hilo.
Wiki iliyopita, baada ya kubanwa na wapigakura wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alisema kampuni yake ya Uwakili wa Immma Advocate, iliifungua na baadaye kuifunga Kampuni ya Deep Green Finance kwa agizo la serikali.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Sokoni, Butimba nje kidogo ya Jiji la Mwanza, wapigakura hao walimtaka Masha ambaye ni mbunge wao, kueleza sababu zilizomfanya akubali kuisajili Kampuni ya Deep Green Finance Company, ambayo inadaiwa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kinyemela na baada ya kutekeleza ufisadi huo kuifunga ghafla.
Mmoja wa waliohudhuria mkutano huo, Peter Charles, mkazi wa Kata ya Butimba wilayani Nyamagana, alitaka kujua endapo Waziri Masha ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya uwakili ya Immma, ambayo imetoa jaji kwenye serikali ya awamu ya nne.
Baada ya Waziri Masha kukubali, mwananchi huyo alimtaka waziri amhakikishie kwamba ni msafi na kwamba hahusiki na wezi wa mabilioni ya fedha za BoT wakati kampuni aliyoifungua imetajwa kuhusika na upotevu wa fedha hizo za EPA.
"Nashukuru kwa kuuliza swali hilo katika wilaya hii, ingawa swali umelipamba sana, lakini najua umelipata katika vigazeti, mimi ni Mkurugenzi wa Immma, lakini kwa sasa nipo likizo bila malipo, nalipwa posho na Immma. Kuhusu ujaji wa Mheshimiwa Mujulizi, yeye ameteuliwa na rais kutokana na taaluma yake ya sheria.
Ni kweli kampuni yangu ilisajili Deep Green na tukaifunga kwa maelekezo ya serikali. Immma haikuchota mabilioni, naomba ieleweke. Na hili, sijawahi kuficha ni kweli. Kampuni hiyo ya Deep Green baada ya kusajiliwa, ilifungwa kwa maagizo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano," alisema Masha katika majibu yake.
Kampuni ya Deep Green Finance Co. Ltd ilianzishwa Machi 18, 2004 na kwa kipindi cha miezi minne, kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 inadaiwa kupokea jumla ya Sh 10,484,005,815.39 kutoka BoT. ??Kipindi hicho kilikuwa cha mchakato au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 14, 2005 na kwamba kuanzia Desemba 11 mwaka huo, hakuna fedha iliyoingizwa katika akaunti ya kampuni hiyo hadi Februari 27, 2007 ilipovunjwa kwa hiari ya wanahisa wake. ?
Wakurugenzi wake (majina tunayo), ambao wanadai kupokea fedha hizo katika mazingira ya kutatanisha mmoja ni kutoka New Zealand na wawili ni kutoka Afrika Kusini. ?
Wakurugenzi hao wote ni wakazi wa Afrika Kusini na ni maofisa au wafanyakazi wa Nedbank Ltd ya Afrika Kusini. ?
Kwa mujibu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wanahisa wa awali wa kampuni hiyo, walikuwa ni mawakili wawili Watanzania ambao pia ni mawakili wa Kampuni ya Tangold ambayo nayo imo kwenye orodha ya wanaotajwa kuchota fedha BoT. ?
Taarifa za kibenki zinaonyesha kwamba, Mei 1, 2004, Deep Green Finance ilifungua akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam. ?
Siku ya ufunguzi wa akaunti hiyo ilikuwa Siku Kuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa mapumziko na kwamba, kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua akaunti bila kuingiza wala kutoa fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja, kuanzia Mei Mosi, 2004 hadi Julai 31, 2005. ?
Kampuni hiyo haikuwepo kwenye orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na Benki Kuu Agosti 21, 2007 ili kuonyesha kwamba imesajiliwa. ?
Kampuni nyingine ya Tangold, kama ilivyo kuwa kwa kampuni ya Deep Green Finance ilifunguliwa siku ya Sikukuu ya Mwaka Mpya ambayo ilikuwa mapumziko, Januari Mosi, 2003 kwa akaunti Na. 011103024852 NBC tawi la Corporate.