Serikali yawasilisha Bungeni mapendekezo ya Bajeti ya 2024/25 iliyofikia Tsh. Trilioni 49.39

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.39.

Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu.
IMG_20240311_165532_323.jpg
Screenshot_2024-03-11-16-52-55-006_com.instagram.android-edit.jpg
 
Ongezeko la t4.95sawa na bil 4950 Ukigawa Kwa 12 unapata 412.5 million.

Wafanyakazi wa umma hamtapata "additional" na Kuna uwezekano wa kukosa "increments".

Hata madaraja aka vyeo watapanda wachache sana pungufu ya 20,000 Kwa kada zote.

Pesa nyingi itaenda kwenye uchaguzi wa sm 2024, & uchaguz mkuu 2025.

Poleni sana.
 
Back
Top Bottom