Kambi ya Lowassa yaibuka kidedea UVCCM Arusha

Napata wasiwasi sasa....
Huyu bwana huenda kweli akashinda urasi, maana nilidhania watu wanatambua makosa yake kumbe wanamsherehekea.
Sina la kusema but nimehamini jamaa anaweza kuchukua dola yetu hapo nchini.
Yangu macho....ngoja nisubiri na kuona nini kitajiri.
 
Hashikiki ndani ya hicho chama cha mafisadi, tunamsubiri huku nje tumtie shinikizo la damu kwa matokeo ya ajabu ambayo hajawai kuyafikiria.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

kabisa. wao ccm si wanajifanya nchi ni ya kwao sasa wasubiri 2015 tutakapo waonesha watanzania tunataka nini kwa maendeleo yetu.
 
Napata wasiwasi sasa....
Huyu bwana huenda kweli akashinda urasi, maana nilidhania watu wanatambua makosa yake kumbe wanamsherehekea.
Sina la kusema but nimehamini jamaa anaweza kuchukua dola yetu hapo nchini.
Yangu macho....ngoja nisubiri na kuona nini kitajiri.
wewe unadhani huyu akisimama na Dr wa ukweli Mh wilbrod Slaa ataambulia kura ngapi? amini usiamini hata mil 1 hatapata. hao ccm wenyewe siku hizi wana kadi 2, moja ya huko wanachumia tumbo na nyingine ya CHADEMA. wanajua yeyote atakaye gombea na SLAA lazima achezee kichapo.
 
Fisadi Lowassa nani ataweza kumshika wakati nchi yote inanuka rushwa!? Nchi ingekuwa na utawala bora huyu hata asingethubutu kutamka kama anataka kugombea ubalozi wa nyumba kumi kumi!!! achilia mbali kutaka kuwa Rais.
 
Hashikiki ndani ya hicho chama cha mafisadi, tunamsubiri huku nje tumtie shinikizo la damu kwa matokeo ya ajabu ambayo hajawai kuyafikiria.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

wasiwasi wangu na wale wa kule sigimbi mkuu. wanaelewa unacho kiseam? wanapata kusikia sauti yako? jitihada zetu zipo hapa JF, lakini kule kwenye root bado kabisa
 
Acheni kumsulubu mtu bila ushahidi.ufisad wa lowasa ni upi?hebu tajeni kwa ulinganifu na jk na riz,membe na sita
 
Hivi Mary Chatanda bado yupo Arusha?yule mwanamke ni jasiri na katili sana!!anakomaa sana!!kweli njaa kitu kibaya sana!!ataishia pabaya sana huyu mama
 
Fisadi Lowassa nani ataweza kumshika wakati nchi yote inanuka rushwa!? Nchi ingekuwa na utawala bora huyu hata asingethubutu kutamka kama anataka kugombea ubalozi wa nyumba kumi kumi!!! achilia mbali kutaka kuwa Rais.
Mkuu BAK, nakushukuru kuanza kuukubali ukweli mchungu!. Kwa vile Tanzania ni nchi ya wala rushwa, inamaa kiongozi bora wa nchi yetu ni yule anayejua kutumia vizuri hii rushwa na bingwa wa matumizi ya fedha anafahamika!. Nawaombeni sana, tuipuuzie kabisa ile kauli ya Baba wa Taifa kuhusu hawa watu wa "kuogopwa kama ukoma". Sasa ndio tuwapende kama mboni za macho yetu!.

Na maadamu Tanzania tumekubali kuwa ni nchi ya ufisadi!, then, kiongozi bora wa taifa hili, shurti awe pia ni bingwa wa ufisadi!, hivyo kuelekea 2015, Watanzania watanchagua kiongozi mwenye ubora wa vigezo hivyo!, wewe jiulize jee mgombea wako anavyo vigezo vya kuchagulika?.

Kama CCM ilipiga vuvuzela la kuchafuliwa na mapacha watatu!, kwa ni nini wasingeweka vigezo ile kuchafuliwa tuu, ni sababu tosha ya kutothubutu hata kuomba fomu ya kugombea, achilia kuijaza, kuirejesha, kupitishwa bila kupingwa na sasa ntu kama Chenge anasubiri tuu kutangazwa rasmi ndie mjumbe wa NEC!.

2015 ni CCM Tena!.
P.
 
na Grace Macha, Arusha

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amezidi kuwatimulia vumbi wapinzani wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutokana na wajumbe wanaounga mkono kambi yake kuzidi kupeta katika uchaguzi. Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha uliomalizika jana, kambi mbili zinazowaunga mkono Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe katika mbio za urais 2015, zilionekana kutifuana vikali.

Msuguano huo ulianza kujitokeza tangu juzi kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa huo, ambapo juhudi za Katibu wa Mkoa, Mary Chatanda kutaka kuihujumu kambi ya Lowassa, ziligonga mwamba na kunusurika kipigo.
Chatanda ambaye alikuwa akifanya juhudi za kuhakikisha mshindi anakuwa Dk. Harold Adamson, aliambulia patupu baada ya Robinson Meitinyiku anayedaiwa kuungwa mkono na Lowassa, kushinda kwa kura 247 dhidi ya 188 za mpinzani wake.

Katika mwendelezo huo huo wa msuguano wa kambi hizo mbil, jana Katibu huyo CCM Mkoa wa Arusha, Chatanda, alijikuta akiaibishwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa chama baada ya kujifanya amesahau kumtambulisha Lowassa. Chatanda aliufanya ukumbi mzima kupiga kelele kubwa wakisema bado! bado! Bado Eddo! Eddo! Eddo! Na ndipo kwa aibu kubwa, katibu huyo akameza mate na kumtambulisha Lowassa.

Hata hivyo, hatua hiyo ilitafsiriwa tofauti na baadhi ya wajumbe ambapo wengine walisema ni tukio la bahati mbaya, lakini wengi wao wakidai kuwa Chatanda alifanya makusudi kutokana na kundi analoliunga mkono kuanguka kwenye uchaguzi wa UVCCM. Katika mkutano huo mkuu wa mkoa uliohudhuriwa na wajumbe 833, nafasi ya Mwenyekiti ilirudi tena kwa Onesmo ole Nangole ambaye anadaiwa kuunga mkono na Lowassa, akiwaacha kwa mbali washindani wake wawili.

Nangole alijizolea kura 604 huku akifuatiwa kwa mbali na Adam Choro wakati Dk. Salash Toure aliyedondoshwa na Lowassa kwenye uchaguzi wa ujumbe wa NEC Taifa kupitia wilayani Monduli akiambulia kura 13. Akitangaza matokeo hayo, msaimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, alisema kura zilizopigwa ni 833 ambapo kura halali zilikuwa 830 na tatu ziliharibika.

Mapema akifungua mkutano huo kabla ya uchaguzi, Prof. Maghembe, aliwataka wajumbe kuacha kuzomea au kushangilia wagombea pindi watakapofika mbele yao kujinadi. Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi watakaojenga chama kwa kuhakikisha wanavunja makundi na kuwaunganisha wanachama wote ili kuvirejesha viti vya udiwani na ubunge walivyovipoteza mkoani humo.
"Msichague viongozi watakaobweteka na kutugawa, hawa hawatufai, tuepuke viongozi wa aina hii, tuchague watakaokisaidia chama," alisema Maghembe.

Naye Lowassa, akizungumza baada ya kuchaguliwa na wajumbe kuwa mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, aliwashukuru wote kwa imani waliyompa huku akishangiliwa kwa kishindo. "Wajumbe nimewaelewa na sitawaangusha, nimewaelewa ndugu zangu sitawaangusha, nawashukuru kwa kunishangilia, ila sasa tusishangilie tusije kuharibu utaratibu," alisema Lowassa.

Akijinadi kwa wajumbe hao, Nangole aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia dosari zilizopo na kushughulika na watu wote wanaoleta makundi ndani ya chama kwa mgawanyiko kuanzia wilayani mpaka Mkoa.

Naye Dk. Toure, aliwaomba wajumbe hao kuwa akichaguliwa, atamaliza makundi yaliyopo ambayo yamekiathiri chama hicho kwani wanachama wamegawanyika kila ngazi na kuwasihi wawabwage wagombea waliotumia fedha kuomba kura kwenye uchaguzi huo.
Mgawanyiko ndani ya chama ulionekana kuzungumzwa na kila mtu kwani hata Chora, naye aliwaomba wajumbe wamchague ili tatizo hilo alilodai kuwa limewapotezea majimbo.

Waandishi wetu wa habari bado wanasafari ndefu sana,sasa ukisoma habari hiyo unashindwa kuelewa membe anaingiaje arusha kikubwa hapo ni hisia tu na umbea kutoka kwa magamba walioko katika kambi ya EL lakini kikubwa zaidi ushahidi wa mazingira hapo lazima kambi ya mzee iliwatumia ipasavyo waandishi wa habari kwa bei nafuu-safari bado ndefu kwa vyombo vya habari
 
Hashikiki ndani ya hicho chama cha mafisadi, tunamsubiri huku nje tumtie shinikizo la damu kwa matokeo ya ajabu ambayo hajawai kuyafikiria.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

hilo nalo neno waache wadanganyane tukutane 2015
 
Napata wasiwasi sasa....
Huyu bwana huenda kweli akashinda urasi, maana nilidhania watu wanatambua makosa yake kumbe wanamsherehekea.
Sina la kusema but nimehamini jamaa anaweza kuchukua dola yetu hapo nchini.
Yangu macho....ngoja nisubiri na kuona nini kitajiri.

Mmmhh! Hata mimi sichelewi kusema lowassa is a next president, hapa ndipo nisipowaelewa watanganyika, maneno mengi vitendo hakuna. Pamoja na kashfa zote za rushwa za lowassa, lakini kila anapopita anashangiliwa kwa nguvu na anashinga kwa kasi, watu hao hao ndio wanalamika kuwa lowassa ni fisadi, akitokea lowassa mbele yao wanamshangilia na kumsujudu.kwa kasi hii lowassa ni rais 2015. Je watanganyika tumelogwa na nani aliyetuloga?
 
Waandishi wetu wa habari bado wanasafari ndefu sana,sasa ukisoma habari hiyo unashindwa kuelewa membe anaingiaje arusha kikubwa hapo ni hisia tu na umbea kutoka kwa magamba walioko katika kambi ya EL lakini kikubwa zaidi ushahidi wa mazingira hapo lazima kambi ya mzee iliwatumia ipasavyo waandishi wa habari kwa bei nafuu-safari bado ndefu kwa vyombo vya habari

Mkuu usitoe mapovu, huo ndio ukweli wenyewe.

Karibu kila ngazi ya uongozi ndani ya CCM iliyokuwa ikigombaniwa lazima makundi makuu matatu ya kambi za wagombea urais ndani ya CCM yalijitokeza. Sasa Arusha kambi ya Lowassa imezinyoa kambi zingine vipara!!!
 
kwa bahati nzuri nilishushiwa hizo ndoto mapema kuwa the next prezda ni lowasa ndo mana kwa sasa siumizi kichwa,.kuna mkuu hapo anahoji ushndi wa lowasa arusha kuwa ni wa kiduchu vp liwale? ni jikumu lake kufanya tafti kwa msaada tu ni kuwa awana mdogo aliempiga chini chikawe ni mtu wa edo damdam,pili alieshnd mkt uvccm lindi ni wa edo damdam kwa hayo unasemaje?
 
Back
Top Bottom