Kambi ya Lowassa yachanganyikiwa

Kambi ya Lowassa yachanganyikiwa

.Washambulia kila anayetajwa kwenye urais
.Magazeti ya Mtanzania, Rai yapewa maagizo maalum

KAMBI ya mbunge wa Monduli Edward Ngoyai Lowassa, imeanza kutetereka na tayari hofu ya mgombea wao kupitishwa na vikao vyenye maamuzi ndani ya CCM imetanda.

Inaelezwa, nafasi ya Lowassa kupenya na kuteuliwa katika kinyang’anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, ni finyu ukiachilia mbali udhaifu wa afya yake, sifa zinazotajwa kwa mgombea anayehitajika nazo zinamkwaza.

Taarifa kutoka ndani ya kambi hiyo, zinasema kutajwa kwa Waziri wa Miundombinu, John Magufuli, Jaji mstaafu Agustino Ramadhani, kumemtisha Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND na kukwamisha zoezi lake la kutangaza nia ya urais kama ilivyoelezwa kwamba angefanya hivyo 19, Februari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha, baadhi ya watu wanaomuunga mkono mbunge huyo wa Monduli wakiwemo baadhi ya vijana wa CCM, tayari waliingia mjini Arusha kuanzia 18 Februari kwa ajili ya kuhudhuria zoezi hilo lililotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Kusema ukweli hali ni mbaya, mzee ameanza kukata tamaa ya urais kutokana na watu wanaotajwatajwa, kuwa na sifa zinazohitajika na chama ikiwemo uadilifu, sasa mzee wetu hana hiyo sifa na inajulikana hilo kwa watanzania wote”

“Ndio maana kuna ukimya fulani, hata kwenye mitandao wengine tumeanza kupunguza mashambulizi maana hali haieleweki kamanda na unaweza kumtukana mtu kumbe ndiye rais ajaye halafu ikawa tabu” alisema kijana mmoja kutoka mkoani Mara, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni mmoja wa wasuka mipango wa kambi hiyo.

Kijana huyo ambaye mara zote amekuwa akijitambulisha kuwa ni Mkuu wa Wilaya mtarajiwa wa wilaya moja Mkoani Mtwara kwenye serikali ya Lowassa, hivisasa anadaiwa kutafuta ukaribu na makada wengine wa CCM wanaotajwa kwenye mbio za urais.

Taarifa zaidi zinasema, katika kuhakikisha Lowassa anabaki kwenye chati ya urais, msemaji wake Hussein Bashe ambaye anaonekana kupambana kuhakikisha anaokoa jahazi, ametoa maagizo kwa gazeti la Mtanzania na Rai, linalomilikiwa na Rostam Aziz, kuhakikisha waandishi na wahariri wa gazeti hilo wanashambulia watu wanaowadhani ni kikwazo kwa mgombea wake (Lowassa).

Inaelezwa waandishi wanaopeleka habari zinazomsaidia Lowassa, mbali na mshahara wanaolipwa, wameongezewa posho kwa ajili ya kazi hiyo, hivyo imewapa hamasa waandishi wengi kutafuta habari za watu hao na wakati mwingine wamekuwa wakitengeneza habari za uongo ili wapate chochote.

“Bashe ametoa maelekezo kwamba, tumpiganie bwana mkubwa maana hali imeanza kuwa mbaya, anasema mabosi wake wamempa maagizo ya kuhakikisha kila anayeonekana kikwazo kwenye harakati zao, ashambuliwe na kila anayefanya kazi hiyo aongezewe maslahi” alisema mmoja waandishi ambaye pia ni kiongozi wa CCM anayedaiwa kuwa njiani kuhamia kwenye kambi ya mbunge wa Mtama, Bernard Membe anayetajwa kwenye mbio za urais.

Mwandishi huyo alisema, tayari gazeti hilo limemshambulia Jaji Agustino Ramadhani siku chache baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa warithi wa Rais Kikwete, mwingine ni John Magufuli na mara kadhaa wamekuwa wakiandika habari mbaya juu ya Waziri Membe.

Inaelezwa, hata chanzo cha Lowassa kushindwa kuhudhuria msiba wa mama wa Jaji Ramadhani, ni kukwepa aibu baada ya gazeti hilo kumshambulia jaji huyo mstaafu na minong’ono msibani hapo ikadai yalikuwa ni maelekezo ya Lowassa.

“Maagizo yaliyotolewa hivisasa ni kumshambulia Prof. Muhongo na kuna mwandishi anaitwa Evans amepewa kazi maalum ya kuhakikisha anapata taarifa za Muhongo baada ya akina Bashe kudhani pengine anaweza kujitosa kwenye urais”

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini tayari kambi hiyo ya Lowassa imeishiwa mbinu za kumsaidia mgombea wao kupenya kwenye kinyang’anyiro cha urais, na kazi iliyobakia ni kufanya vurugu na kushambulia makada wa chama hicho wanaotajwa kwenye urais.

Hivi karibuni, kambi hiyo imepata pigo kubwa kufuatia kukanushwa kwa kila taarifa ambazo zinasambazwa na vyombo vya habari kwa lengo la kumjenga Lowassa, ambapo habari iliyokanushwa kwa nguvu kubwa ni madai ya wabunge 150, kumuunga mkono mbunge huyo wa Monduli.

Habari nyingine ni ile iliyodai wanachuo wa IFM kumuunga mkono Lowassa, madai ambayo yamekanushwa na serikali ya wanafunzi wa chuo hicho.

Inaelezwa, watu wanaohusika na masuala ya kusuka propaganda ndani ya kambi hiyo, wamekuwa na uwezo mdogo wa kufanya kazi hiyo na kujikuta wakimpotosha Lowassa kwa taarifa za uongo ili waendelee kulipwa mishahara minono wanayolipwa, na badala ya kumsaidia, wanammaliza.

“Hawa jamaa akina Hemed (Hemed Ally) na wenzake wameshindwa kazi kabisa, wanasambaza propaganda za kitoto kabisa wanadai eti kuna wabunge 150 wanamuunga mkono Lowassa wakati ukweli ni wabunge 15 tu na wengine wameshamkana, huu ni utoto, tatizo wanalipwa hela nyingi sana, sasa hawataki kuzipoteza ndio maana wanatunga hata uongo ili waonekane wanafanyakazi” alisema kada wa CCM ambaye alizungumza na mwandishi wa habari hizi jirani na ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, kwa upande mwingine baadhi ya wapambe wa Bashe, ambao bado wanaamini Lowassa anaweza kuwa rais, wamekuwa wakijigamba kwamba hakuna ‘mpuuzi’ yeyote anayeweza kukata jina la Lowassa na wamekuwa wakitoa matusi ya nguoni dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na familia yake.

Aidha, wapambe hao wamekuwa wakitishia baadhi ya watu wanaomshambulia Lowassa.

Chanzo: ...

Wewe elezea sifa za huyo mpuuzi mwenzio aliyekutuma kuandika hii takataka humu ndani.. Je ni sifa zipi anazomzidi kiongozi mahiri na shupavu Edward Lowassa, na kwa taarifa yako sisi watanzania tunaona hata hiyo october ni mbali, kwani tunamuhitaji Lowassa wetu ili atuletee maendeleo tunayoyahitaji katika taifa letu!
 
sijawahi ona ujinga kama huu ..team Lowassa wanaenda sehem magazeti hayafiki nyie mmekazania siasa za mjini..tujipange jamani Naskia hawa jamaa mjini washamaliza sasahv wapo Bush ,Bashe na Hemed wabaya sana !!
 
In 40 days and 40 nights all will believe...those who criticise and curse will abstain...those who don't believe will believe...Lowassa will make history and just like rain he can't be stopped
 
sijawahi ona ujinga kama huu ..team Lowassa wanaenda sehem magazeti hayafiki nyie mmekazania siasa za mjini..tujipange jamani Naskia hawa jamaa mjini washamaliza sasahv wapo Bush ,Bashe na Hemed wabaya sana !!

Mkuu josh Hawa jamaa siasa Zao ni kung'oa kucha
 
Hii mada kaianzisha makonda nini?WATASHINDANA SANA LAKINI HAWATASHINDA KAMWE!!! LOWASSA YU NA MUNGU[/QUTE

Kweli hawatashinda maana walisema Makonda haendi kokote lakini mwishowe kawa DC tena wa wilaya anamoishi Mh Lowassa.
Big Up brotherKaka Makonda ...watashindana lakini hawatashinda...wacha wamalize nguvu
 
HATA YESU ALIPOKUJA WENGI WALIPINGA LAKN WALEWALE WALIOPINGA NDO WAKAWA MITUME WA YESU... Nafurahi kuwaona mitume wa LOWASA mnaompinga kwa sasa ...naamin mtamkubali akitangaza nia bado hajasema kama atagombea lakin nyie mmeshaona ...Basi namim naungana na nyie kumsapoti kwakuwa mmeonyesha sapoti ya kumtangaza kila siku kwenyE mitandao.... KAZI NZUR MNAFANYA YA KUMUOMBA LOWASA AGOMBEE ...Asemwaye sana ndiye anayejua....LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASAAA LOWASAAAA LOWASAAAAA LOWASAAAAAAA LOWASAAAAAAAA njooo utangaze nia wanakuhitaji hawa maana wanatumia njia za pemben hawatak kusema direct......AMINA
 
wabunge wenyewe tunawaona kila kukicha wakijipendekeza kwa lowasa
 
Hii mada kaianzisha makonda nini?WATASHINDANA SANA LAKINI HAWATASHINDA KAMWE!!! LOWASSA YU NA MUNGU[/QUTE

Kweli hawatashinda maana walisema Makonda haendi kokote lakini mwishowe kawa DC tena wa wilaya anamoishi Mh Lowassa.
Big Up brotherKaka Makonda ...watashindana lakini hawatashinda...wacha wamalize nguvu

Ila Kikwete kafanya jambo la maana sana Sababu huyu kijana wangemtumia tu mpaka October alafu angestaafu na umri mdogo
 
Ndugu zangu, tusitikisike na propaganda hizi. Hii habari hata mwenda wazim atajua hii ni propaganda na imesukwa kw maksudi kinyume na lowassa.hakuna mvua wala jua litakalo itikisa kambi ya lowassa.
 
Ukiona mtu anamtetea Lowassa ujue ni mmasai au ni njaa tu inamsumbua

Illogical conclusion! unatumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja! aya twambie na wewe umetokea kambi ya nani? maana huu ndo mda wa watu kutumwa!
 
Mnaanzisha thread afu mnajijibu wenyewe.
Nyie kweli majuha!
 
Hhii kumwita mtu anajaa usie mjua ni Stress .maana humu tunekuta a tu kila mtu na intrest zake .sasa watu washindwe kuwasemea wadombea wao kisa wataambiwa nijaa hhmmm
 
Hapa naona ccm wa mm ataka wapoteze kabisa wakiweka mtu mwingine. Tunajua wanamwogopa Lowasa atawalipua maovu yao mana kujihuzuru kwake ilikua ni mbuzi wakafara wakasahau kua hawajamchinja ila wamemchoma sindano ya usingizi atazinduka.

Magufuli sawa ila anamaamuzi magumu hafai kuwa kiongozi wa juu mwenye kauli ya mwisho ye abaki kwenye wizara tata azinyooshe kama vipi wampe wizara ya elimu.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom