Kambi Rasmi ya Upinzani yapinga mradi wa bomba la gesi

Kasema hilo hivi punde katika hotuba yake ya kambi rasmi ya upinzani bungeni...

Tunashukuru sana Upinzani hususani chadema na mnyika kwa ujumla...


HUKU MABOMU BADO YANAENDELEA NA KUNA VURUGU KALI SANA MAENEO MBALI MBALI,

KAULI YA MNYIKA IMEPOKELEWA KWA SHANGWE YA HALI YA JUU SANA...

TUTAKUJA NA PICHA BAADAE KIDOGO....

Thanks Mnyika,Thanks a lot,KUSINI INATAMBUA MCHANGO WA CHADEMA NA UPINZANI KATIKA HILI...
 
Amesema mradi usitishwe mpaka pale katiba mpya itakapokuwa tayari,sera na sheria na mikataba iwekwe wazi kwa sababu hata mwaka jana waliagiza wizara isingie mkataba wowote kwenye sekta ndogo ya gesi na mafuta mpaka kuwe na sera
 
Kambi rasimi ya bungeni imedai kuwa ili serkali ijenge bomba la kisafirisha gesi kutoka mtwara ni sharti iwape maelezo wakazi wa mtwara watafaidika nini? na ipeleke mkataba bungeni na ujadiriwe.
 
mnyika pia ameongelea swala ya serikali ya chadema itakayokuwa ikiwashirikisha wananchi kwenye kuendeleza rasimali za taifa ikiwemo madini gesi na mafuta, katika ngazi ya wilaya,mkoa,kanda na taifa,wamesema wasitishe raundi ya nne ya utafutaji wa gesi na madini
 
Safi sana
Nadhani jioni kwenye uchangiaji patakuwa
patamu sana hapo.
 
Tunataka watu kama akina Mnyika(chadema) wanaowakilisha matakwa ya wananchi na sio akina Mulongo(ccm) wanaotaka % zao na mikataba ya kificho
 
Msimamo wa Kambi Rasmi ni huu kuhusiana na ujenzi wa Bomba la Gesi, ninanukuu hotuba ya Kambi Rasmi.

3.4 BOMBA LA GESI TOKA MTWARA HADI DAR ES SALAAM


Mheshimiwa Spika, Pamoja na ushauri wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wakati wa kuwasilishwa kwa bajeti ya wizara 2012/2013 kuitaka Serikali kuwasilisha Bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili Bunge liweze kuishauri na kuisimamia Serikali kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63; kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji huo mkubwa lakini bado serikali haikutilia maanani ushauri huu. Matokeo yake siyo tu kusababisha mkanganyiko kwa wakazi wa Lindi na Mtwara bali pia kuacha maswali mengi kwa watanzania juu ya nini hasa nia ya serikali kwa kuficha mikataba inayohusu rasilimali hizi za Taifa kwa wananchi wake na hata kwa chombo cha kuwakilisha wananchi kama Bunge.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali isiendelee na ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar Es Salaam hadi kwanza; Mosi, iweke wazi kwa Bunge mikataba yote inayohusu uendelezaji wa gesi asilia ikiwemo ya ujenzi wa Bomba hilo. Pili, ikutane na wananchi kuwashirikisha na kuhakikisha manufaa kwa taifa na kwao.

Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA imeshangazwa na hatua ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo tangu kuibuka kwa mgogoro huo amejikita zaidi katika kutoa kauli kupitia vyombo vya habari badala ya kwenda kukutana na wananchi hatua kwa hatua na kuwezesha ufumbuzi kupatikana. Aidha, manufaa kwa wananchi wa Lindi na Mtwara ambayo taarifa yake imechapwa kwenye vyombo vya habari yaletwe kama taarifa rasmi bungeni ikiwa na ulinganisho baina ya shughuli za kijamii zilizofanywa na makampuni tajwa pamoja na miradi iliyotekelezwa na Serikali kufuatia mapato katika sekta hii tangu mwaka 2004 na thamani halisi ya mapato ambayo makampuni tajwa na Serikali wamepata.

that is official
 
Nimepiga picha kwenye vurugu za hapa COCOBEACH ila katika harakati za kurupushani nimeangusha camera na askari wameichukua,hali ni mbaya,

Nimeskia tetes kuwa kuna askari na raia mmoja kafa,tukipata uthibitisho tutaiweka hapa,


Natembea na laptop lakin nafungua na kuifunga kwa ajili ya kuwapa updates tuh,hali tete sana,,


Nipo maeneo haya haya ya vurugu cocobeach,mabom bado yanapigwa
 
sababu ya serikali kulazimisha hii project bila kuweka wazi mkataba wake ni kipi kuwapiga na kuwatisha kwa mabomu sio suluhisho la matatizo ya watanzania ipo siku uvumilivu utaisha
 
Kasema hilo hivi punde katika hotuba yake ya kambi rasmi ya upinzani bungeni...

Tunashukuru sana Upinzani hususani chadema na mnyika kwa ujumla...


HUKU MABOMU BADO YANAENDELEA NA KUNA VURUGU KALI SANA MAENEO MBALI MBALI,

KAULI YA MNYIKA IMEPOKELEWA KWA SHANGWE YA HALI YA JUU SANA...

TUTAKUJA NA PICHA BAADAE KIDOGO....

Thanks Mnyika,Thanks a lot,KUSINI INATAMBUA MCHANGO WA CHADEMA NA UPINZANI KATIKA HILI...
Imeshapigwa muhuri...Full stop.Huwa mnyika anaamuru Serikali ya CCM.Tena humuamuru rais.Mengine huwaachia wacheze ngoma, mipasho, etc wakimaliza wanarudi wenyewe kwenye amri.
 
Nimepiga picha kwenye vurugu za hapa COCOBEACH ila katika harakati za kurupushani nimeangusha camera na askari wameichukua,hali ni mbaya,

Nimeskia tetes kuwa kuna askari na raia mmoja kafa,tukipata uthibitisho tutaiweka hapa,


Natembea na laptop lakin nafungua na kuifunga kwa ajili ya kuwapa updates tuh,hali tete sana,,


Nipo maeneo haya haya ya vurugu cocobeach,mabom bado yanapigwa

Ugomvi wa nini tena ama ndio wanatafuta sababu ya kuwaweka wananchi selo,mimi nilidhani wananchi wamekaa nyumbani duh ,laptop ungeiacha nyumbani watakupora hao polisi poleni sana gesi haitoki hata kwa bomba la peni
 
Back
Top Bottom