Kamati za harusi Dom Acheni Ushamba na Uroho

Kamati za harusi Dom Acheni Ushamba na Uroho

Stayfar

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
1,097
Reaction score
2,312
Wana kamati za harusi,Dodoma mnatia aibu.Kwamba Ile siku ya harusi anayehudumia Chakula mnataka awaletee Chakula chenu Special wakati wa mchana,kwamba mnakagua Ukumbi kabla ya Sherehe.Mlivyo washamba mnadai Ugali na filigisi za kuku.Nilichogundua baadhi ya wakazi wanaoishi mkoa huu ni Waroho na Washamba mno.

Siku ya sherehe ya harusi mçhana, wanaacha kula kwao kwamba waletewe Chakula, hasa Ugali na filigisi walie ukumbini.

Mwana kamati anafunga safari toka Nkuhungu kuja hadi Royal Garden,ambapo ni umbali usiopungua Km 18 au 20 kuja kula Chakula kilichoandaliwa na mtendaji wa Chakula,Aliye pewa hiyo tender kama hatatekeleza asitegemee kupata kazi sehemu nyingine Dodoma.

Kibaya kingine mwenyekiti na Bwana harusi wanataka humo ndani ya pesa Ya Chakula uhakikishe unawapa fedha kama shukrani baada ya sherehe,wakati kwenye kikao cha kupitisha badjet ya chakula wanakuwa wakali kupitisha gharama husika.Dodoma Acheni hizo
 
Hahahahhahha....." Ugali na firigisi" hahaha..daah umenichekesha sana jinsi ulivoiwasilisha maada yako
 
huku ushirombo unawapiga dadii na mbege ya kutosha fasta waanze kuangukiana, wakija kushtuka ushafunga harusi na mke ushabeba, wanarud makwao kula ndizi
 
Kwamba unawachana huku kama wamo vile !!!
Kweli wanaume wa dar waoga kweli kwel si ungewaface moja kwa moja mkuu wanaume wa mkoani wakuonyeshe kazi wangekuoshea ushindwe kuamini
 
Kamati nyingine zipo Moshi Mkuu,usitegemee kuikuta ndafu kwenye bufee.Tuacheni utani,kuna kamati zina uroho uliopitiliza.Cha kushangaza unakuta ni wasomi na wenye uwezo.
 
Sasa mkuu kwani hiyo kazi unaifanya tu kiholela bila makubaliano?

Kama mlikubaliana kuwa mchana utawapikia ugali na firigisi sawa wapikie. Kama makubaliano hayo hayapo basi temana nao.


Ila wabongo wajanja, wanapigia hesabu ya kuku mzima wanajua firigisi, utumbo, vichwa, shingo, na speed hazitakuwemo kwenye bufee.

Wanaona bora wazidake hata hizo firigisi wale na ugali mchana wa harusi. Wanakamati Mungu anawaona. [emoji23] [emoji23]
 
Acha kuwatania wagogo,hiyo tabia wanayo wasukuma...kamati lazma ile vzr tena nyama nyingi mpaka wengine wanatapika!
 
Wana kamati za harusi,Dodoma mnatia aibu.Kwamba Ile siku ya harusi anayehudumia Chakula mnataka awaletee Chakula chenu Special wakati wa mchana,kwamba mnakagua Ukumbi kabla ya Sherehe.Mlivyo washamba mnadai Ugali na filigisi za kuku.Nilichogundua baadhi ya wakazi wanaoishi mkoa huu ni Waroho na Washamba mno.

Siku ya sherehe ya harusi mçhana, wanaacha kula kwao kwamba waletewe Chakula, hasa Ugali na filigisi walie ukumbini.

Mwana kamati anafunga safari toka Nkuhungu kuja hadi Royal Garden,ambapo ni umbali usiopungua Km 18 au 20 kuja kula Chakula kilichoandaliwa na mtendaji wa Chakula,Aliye pewa hiyo tender kama hatatekeleza asitegemee kupata kazi sehemu nyingine Dodoma.

Kibaya kingine mwenyekiti na Bwana harusi wanataka humo ndani ya pesa Ya Chakula uhakikishe unawapa fedha kama shukrani baada ya sherehe,wakati kwenye kikao cha kupitisha badjet ya chakula wanakuwa wakali kupitisha gharama husika.Dodoma Acheni hizo
Wenyewe wana uroho wewe unaroho mbaya..
 
Ulitaka wakuachie firigisi ukapigie dili kwingine Eeh
 
Kuku labda za harusi ni 50 kila kuku ana firigisi kuziweka kupika na ugali kwa tender yenye m.3.5 kupika ugali na frigisi ha h aha au wewe ulitaka hizo firigisi ule wakati wa honeymoon? una roho ya uchoyo sana mpk watu wanakusaidia kazi bila hata kuwalipa mia unaona uchungu wakila firigisi
 
Back
Top Bottom